Kuna mashabiki wa Simba walianza kuishabikia Simba kipindi inafanya vizuri zaidi huku mashindano ya ndani nadhani misimu ya kuchukua ubingwa mara 4 mfululizo.
Hawakutegemea ushindani na hawakuwahi kushuhudia mpinzani wetu ( Yanga) ubora wake.
Iko hivi; Kusingekuwa na Yanga hapa Tanzania hata kwa Sasa hizi pressure za mashabiki wenzangu zisingekuwepo.
Tuweni watulivu, TP Mazembe iliwahi kutikisa Afrika hii, lakini ilifika muda ikashuka, hii ndiyo football.
Football wanaoielewa zaidi ni wazungu, wanatoa moyo kwa club zao hata zinapofanya vibaya, wanatoa maoni chanya ya kujenga.
Washabiki wa Simba SC wenzangu, tuweni waungwana, unakuta shabiki anahamasisha wenzake wasiende uwanjani kuishangilia timu, serious???
Hamjui kuwa hata mashabiki pia huchangia kudorola kwa uwezo wa timu?
Penda chako! Nilianza kuipenda Simba SC kipindi Cha Hali ngumu mpka Sasa nafurahia matunda, droo, kupoteza na kushinda vyote ni viambata (package) vya mpira wa miguu, kwamba ukiupenda lazima uvutarajie,
#SimbaNguvuMoja#[emoji881][emoji881][emoji881][emoji1241]