Simba Vs Yanga (1-0) | Shirikisho | Lake Tanganyika. Simba yatwaa ubingwa ASFC

Simba Vs Yanga (1-0) | Shirikisho | Lake Tanganyika. Simba yatwaa ubingwa ASFC

Hongereni Simba na poleni yenu Yanga kwani ndio mpira huo mjipange vizuri kwa msimu ujao.

Nilichoshudia leo Kigoma kupitia Azam TV:-
1. Yanga walipaniki sana kipindi cha pili kiasi walianza kucheza mchezo wa ngómbe na sio mpira miguu na refa angekuwa makini basi "red card" zilikuwa ni zaidi ya moja. Bado sijajua ni maelekezo ya benchi la ufundi au ni kwa sababu ya kuzidiwa.
2. Barua ya Yanga kwa TFF ilimtisha sana refa kiasi alishindwa kutoa penalti ya wazi kabisa pale Mwamnyeto alipomkanyaga Miquison ndani ya "box". Lakini mwisho wa siku amejitahidi sana kuchezesha vizuri.
3. Washambuliaji wa Simba walikosa utulivu kwani walikuwa wana uwezo wa kuimaliza mechi mwanzoni kabisa mwa kipindi cha pili.
4. Kama kuna mtu Yanga wanatakiwa wamlaumu sana basi ni Mukoko Tonombe kwa sababu yeye ndiye aliyewamaliza Yanga leo. Haiwezekani mchezaji wa kimataifa akafanya kosa la kitoto kiasi kile na kuwaachia wenzake mzigo mzito kwa kipindi chote cha pili.
5. Kosa alilofanya Adeyum ni la kimchezo la kukosa "concetration" lakini akumbushwe asilirudie tena kwani kwani kwenye matukio yale (kona, krosi na faulo zinapopigwa) alipaswa amweke Thadeo ubavuni mwake na wala si kumweka mbele kama alivyofanya.
6. Pongezi kwa benchi la ufundi la Simba kwa kuwaduwaza Yanga kwa mbinu mliyotumia ya mipira mirefu ili kutafuta matokeo tu na ikafanikiwa.
7. Benchi la ufundi la Yanga limfundishe Tusila kufunga na namna nzuri ya kukata uwanjani kuelekea golini badala ya kukimbia pembeni zaidi kila wakati. Kiukweli anafanya kazi kubwa sana lakini haina faida yoyote kwa timu. Na leo naona Zimbwe alifanikiwa kumdhibiti kwa kiasi fulani nahisi alikuwa anakesha na "clip"zake za mechi zilizopita.
8. Pongezi kwa wachezaji wa Simba kwani leo waliwaheshimu Yanga na kuacha kucheza kifadha fadha. Ni mara chache sana kuwaona Simba wakicheza kwa machozi, jasho na damu kama leo.

Mwisho kama Simba wanataka kuendeleza wimbi lao la ushindi na kuchukua makombe zaidi basi waende kufanya usajili wa maana kweli kweli. Narudia tena waende wakafanye usajili wa maana kweli kweli kwa sababu mwakani ushindani si wa kitoto kwa sababu zifuatazo:-
1. Udhamini wa Azam kwa vilabu huu utazifanya hata timu ndogo ziwe vizuri sana na zitakazana mno.
2. Usajili wa Azam mwaka huu unatisha. Nimeona wameleta wachezaji wazuri sana na kuna mtu mnyama kwelikweli wamemleta pale anaitwa Koola nadhani wabongo wengi hawamjui ila watakuja kumjua vizuri ligi itakapoanza.
3. Usajili wa Yanga wanaofanya sasa hivi kama utaenda kama inavyotangazwa mitandaoni basi sina shaka mwakani shughuli itakuwa pevu kweli kweli. Kwa sasa Yanga wana benchi mahiri la ufundi kwani wamejitahidi sana kutengeneza timu kwa kutumia kikosi finyu kwa hiyo mwakani tutegemee kuwa litafanya makubwa zaidi iwapo halitavunjwa kama kawaida ya Yanga.
 
Tunakwenda kupiga pale pale kwenye mshono [emoji23][emoji23] .. mi nina watu hahaha ..
 
Kuna watu wanasingizia eti walikua pungufu [emoji3][emoji3]

Simba v yanga 2005
Final tusker cup
Victor Costa red card dk ya 38

Mwisho wa game simba 2 -0 yanga

Simba v yanga 2006
Morogoro
Henry Joseph red card dk ya 10

Mwisho wa game simba 1-0 yanga

Mwaka 2017
Simba v yanga

Mkude red card dk ya 28

Mwisho wa game 1-1

Mwaka 2017 tena
Simba v yanga

Bukungu redcar dk ya 59
Mwisho wa game simba 2-1 yanga


Mpaka hapo tuelewane redcard sio kisingizio

Na kwa mpira wa vipesi
Asante kwa kumbukumbu hii.
Yanga wanataka kutupigia kelele, kisa red card.
 
Kama kubebwa wameshabebwa tayari! Hata tukibishana haisaidii chochote, ilikuwa kadi ya njano, yeye mwamuzi kakurupuka na kadi nyekundu, mikia bwana kuifunga yanga mpaka msaidiane na mwamuzi pamoja na TFF?
Mbwa/Nyani (kama alivyosema coach Luc Eymael ) wanasingizia eti walikua pungufu 😀😀 hebu tuwape kumbukumbu

Simba v yanga 2005
Final tusker cup
Victor Costa red card dk ya 38

Mwisho wa game simba 2 -0 yanga

Simba v yanga 2006
Morogoro
Henry Joseph red card dk ya 10

Mwisho wa game simba 1-0 yanga

Mwaka 2017
Simba v yanga

Mkude red card dk ya 28

Mwisho wa game 1-1

Mwaka 2017 tena
Simba v yanga

Bukungu redcar dk ya 59
Mwisho wa game simba 2-1 yanga


Mpaka hapo tuelewane redcard sio kisingizio

Na kwa mpira wa vipesi mtalia lia sana
 
Ili uifunge yanga,lazima mchezaji mmoja umpunguze kwa hiraaa😂😂😂 pamoja nakuwa pungufu kikosi kipana kimehaha na kupotezapoteza mda!!!
Mbwa/Nyani (kama alivyosema coach Luc Eymael ) wanasingizia eti walikua pungufu 😀😀 hebu tuwape kumbukumbu

Simba v yanga 2005
Final tusker cup
Victor Costa red card dk ya 38

Mwisho wa game simba 2 -0 yanga

Simba v yanga 2006
Morogoro
Henry Joseph red card dk ya 10

Mwisho wa game simba 1-0 yanga

Mwaka 2017
Simba v yanga

Mkude red card dk ya 28

Mwisho wa game 1-1

Mwaka 2017 tena
Simba v yanga

Bukungu redcar dk ya 59
Mwisho wa game simba 2-1 yanga


Mpaka hapo tuelewane redcard sio kisingizio

Na kwa mpira wa vipesi Mtaishia kumbeba Hersi wenzenu wanabeba Kombe.
 
Sawa mbeleko FC, timu ya maelekezo na makandokando
Screenshot_20210725-220913~2.png
 
Najiuliza Hadi kampuni za kubeti zimpe Simba 1.50 halafu Yanga 3.30 ,wakati Yanga wametoka kuwafunga Simba, hii mechi inaonyesha live Simba anashinda
Siku nyingine odds zisikudanganye kwenye betting, mechi ya kwanza yanga alikuwa na odds 6 ila akashinda hvyohvyo
 
Back
Top Bottom