Wakuu tukiacha siasa za maji taka za Usimba na Uyanga. Nataka nichangie huu mjadala kwa namna tofauti, kwa namna ambayo nitaiweka kidogo kisomi na hapa naomba tuache ushabiki.
1. Simba ni kampuni ambayo iko na 2 shareholders, MO and Members on the other hand. Kwa mtiririko huohuo shareholders wako na share 49% na 51% respectively.
Kama ndio hivyo basi SIMBA SC ni Mali ya MO na WANACHAMA kwa upande mwingine. Hata hivyo kama SIMBA ni kampuni na hao ni wabia wake, haitakiwi mbia achangie kiasi fulani katika ujenzi wa ASSETS za Klabu kwa sababu shabiki akichangia ina maana unamwongezea MTAJI MMILIKI.
2. Ilitakiwa ifanyike analysis nzima juu ya gharama za ujenzi kisha gharama zile zigawanywe kwa uzito sawa na SHARES yaani kama ujenzi ni BIL 20 basi MO atapaswa kutoa Bil 9.8 na WANACHAMA Bil 10.2. Yes ni kampuni hivyo Mo hapaswi kusema watu wachangie wakati yeye ni mwanahisa na anapata INCOME through hiyo kampuni. Kwanini aombe michango wakati kampuni ni yake kwa 49%?.
3. Watanzania wenzangu, kabla ya kurukia kitu lazima mkae chini na mtafakari kwa kina juu ya masuala haya. MO anawakosea sana Simba, na always yy hujifanya kama anasaidia lkn ukweli ni kwamba yeye ni Mwanahisa kwanini atake mashabiki wamchangie? Kama ndio hivyo basi ajitoe kuwa mmoja wa wamiliki ili watu wachangie wakijua yeyote anaweza kuwa kiongozi wa SIMBA.
4. Rai yangu kwa wapenda michezo, haki na wapenzi wa hii klabu kupaza sauti na kugundua UTAPELI wa wazi anaofanya huyu MO DEWJI.
KWA UCHACHE NAWASILISHA.
NB. Kama uelewa wako kuhusu umiliki wa makampuni ni FINYU usiquote huu mchango.