Tuwapongeze Simba kwa pale walipolifikisha taifa letu kisoka, kidemokrasia na kiuchumi. Timu zetu bado ni "feeder clubs" kwa timu za kaskazini lakini tumejotahidi kuivuta Africa na dunia kuelekea Tanzania kisoka.
Simba tusitafute mchawi kulikosa kombe la CAF kwakuwa wachawi tunawafahamu wote. Nguvu ndogo za kifedha kuweza kusajili, kulipa na kutunza wachezaji wakubwa wenye uwezo kwa misimu mingi ni miongoni mwa sababu hizo. Wachezaji wazuri watachukuliwa na timu za kaskazini na Ulaya. Simba haina wachezaji wazuri kama wale wa Berkane na Yanga.
Kadi aliyopata Kagoma ilitokana na malezi ya TFF kwa Simba. Kagoma anachezea wenzake vibaya kwenye ligi lakini marefa wetu wanapeta wakidhani wanaisaidia Simba kumbe wañaitengenezea Simba timing bomb lililowalipukia CAF confederation kwenye mechi muhimu sana. Refa alinyooka na kunyoosha Sheria za mpira.
Uwekezaji nje ya uwanja (ulozi) umekuwa mkubwa sana kwa Simba. Hii inawatoa mchezoni wachezaji pale watakapogundua kuwa uchawi wao umeteguliwa na timu pinzani. Uchawi ni kikwazo kwa wachezaji wanaomtegemea Mungu kutokana na imani zao.
Ligi yetu inazalisha washindi fake na legelege wanaokwenda kushindana wa washindi halisi na imara kutoka ligi nyingine.