John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amefunguka mambo kadhaa kuhusu udhamini uliositishwa.
Ni kuhusu GSM kutangaza kuvunja mkataba wa kuwa mdhamini mwenzake wa Ligi Kuu Bara:
“Simba hatukukubaliana na mkataba huo, tulipambana lakini wenzetu hawakuona kama tuko sahihi, tulionyesha njia, tulionyesha ujasiri wetu, wakati ule hawakutuelewa, hatimaye wametuelewa.
“Tunawapongeza TFF kwa kupambana kutuletea mdhamini, haikuwa jukumu lao ni jukumu la klabu, lakini hiyo isitumike kama fimbo ya kuleta kila aina ya mdhamini, ifike hatua nionyeshe thamani ya kile ambacho tunatakiwa kukipata.
“Kuipa timu shilingi milioni tatu kwa mwezi, timu ya Ligi Kuu ni thamani ndogo, kuna wakati inakulazimu kuonyesha thamani yako.
“Anayetoa hela ndogo anapata nafasi kubwa ya kutangazwa, msimu uliopita hatukuvaa nembo ya mdhamini mwenza.
“Shida ni kwenye klabu zenyewe pia, huu ulikuwa mwezi wa pili unaenda wa tatu lakini hakukuwa na hela zilizoingia, kwa nini klabu hazikulalamika? Kwa nini Bodi ya Ligi yenyewe hailalamiki?
“Walitangazwa na timu zote lakini unavunja mkataba kisa tu Simba, basi lengo lao lilikuwa Simba, unataka kukuza soka kisha unasitisha udhamini sababu ya timu moja!”