Simba waziponda Sh milioni tatu za GSM, zilikuwa ndogo sana, wataja lengo la mkataba

Simba waziponda Sh milioni tatu za GSM, zilikuwa ndogo sana, wataja lengo la mkataba

Mo ni mdhamnini wa ligi?

Mo ana hisa kwenye club ya simba, yaani kile alichokuwa anakifanya GSM kwa yanga kabla ya mkataba huu ndicho anachokifanya MO kwa kuifadhili simba
Hujajibu swali nililouliza
 
Huyu Ahmedy Ally anazidi kuimarika kwenye apande wa fact.

Simba aijawai kushindwa vita mnatakiwa mlujue hilo.
Amemvua Nguo Gharibu Said Mohamed Nina Hakika Vilabu 15 Sasa Hivi Wanajicheka
 
Unakazwa wewe sio bure, unaelewa nini juu ya masuala ya mikataba! Wewe ni nani ameshakuja kuhoji mkataba wako na mwajiri wako? Mbona umemficha ata mkeo/mmeo mshahara unaopokea? Unapata wapi nguvu ya kuhoji mikataba ya wenzako, funga bakuli kwa vitu usivyovijua utakuja kuvalishwa dela siku moja
zuzu umepaniki. Unaipa Simba million tatu? Uko siriaz?

GSM alitaka Simba imtangaze Africa na misheni ikabuma, ikawa plan B kuvunja mkataba. Hilo kila mtu analijua. Utopolo , mazuzu poleni sana.
 
huwezi kuelewa Ila uelewe tangazo za mo zimepelekea simba kichukua ubingwa Mara 4 mfululizo na bado mwaka huu msimu huu
Analilia Bei gani matangazo kwenye jezi za Simba!?..acha kuharisha harisha na kujibu usichoulizwa
 
TFF ndiyo imefeli usimamizi wa soka hapa bongo,huo mkataba wao na GSM viongozi walitanguliza matumbo yao mbele bila kuangalia maslahi ya vilabu
Siyo mbaya kwa TFF kutafuta wadhamini wa ligi ishu ni kuwa hawakuweka mambo wazi leo yanavurugika inaonekan GSM amefeli kumbe shirikisho letu ndiyo lilikubal masharti ya kinyonyaji na kutaka vilabu visihoji mambo
Me naona Tff wawajibike kulipa vilabu vilivyovaa logo ya GSM..
Kwani hao GSm wameshindwaje kupitia mlango ambao NBC walipitia
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.


Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.


Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.


“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.


“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Back
Top Bottom