Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Kwani wakati Rs Berkane yupo nafasi ya 6, huo msimu aliokuwa na 0 point si ulikuwepo? Sasa kwanini haikuwa kigezo cha kumfanya a-drop nafasi kwenye viwango vya ubora?Wewe tatizo akili yako inawaza kubishana nasio kuelewa. Ranking ya 2019/2020 hadi 2023/2024 hapo unaongelea misimu mitano ambayo coefficient yake ni kama ifuatavyo;
2019/2020= 1
2020/2021=2
2021/2022= 3
2022/2023= 4
2023/2024= 5
Hizo 0 za USMA zipo kwenye msimu ambao coefficient zake ni ndogo, tofauti na Berkane ambaye yeye kapata 0 msiimu ambao una coefficient kubwa. Berkane hakupata point hata moja katika msimu wa 2022/2023 msimu ambao una coefficient 4 hivyo timu yeyote iliyopata alama kwenye huo msimu lazima awe na point nyingi kwavile coefficient(kizidishio) inambeba.
Kumbuka Yanga tu kwa kupata point 4 kwenye msimu huo wa 2022/2023 zikamfanya awe na jumla ya point 20 ambapo kwa msimu huu huo msimu wa 2022/2023 unakuwa na coefficient 3 ambapo imempa point 12. Ndio maana nikwakwambia huko juu kuwa pata 0 ila sio kwenye coefficient ya 3, 4 na 5
Unaelewa ulichokiandika hapo?
Ni sawa na kusema aliyezidisha 0x1 na aliyezidisha 0x5 hawawezi kuwa sawa kwenye conclusion zao kwasababu kuna ameizidisha 0 kwa namba kubwa.
Kwamba aliyepata 0 kwenye mwaka ambao coefficient yake ina pointi nyingi anakuwa amepoteza sana kuliko yule ambaye aliyepata 0 kwenye msimu wenye pointi nyingi?
Aiseee hili ni tatizo.
Kama hii hauifanyi kwa bahati mbaya basi upo kwenye denial zone.
Mkuu naandika hii ya mwisho.
Haijalishi umeambulia 0 pointi katika msimu wenye pointi ngapi. 0 point itaendelea kuwa na thamani yake ile ile ya 0 hata kama aliyeipata alikuwa kwenye msimu wenye pointi chache.
Hata msimu huu wa 2024-2025 wenye pointi 5 kumbuka ifikapo msimu ujao wa 2025-2026, msimu huu wwa 2024-2025 itakuwa pointi 1 na kuwa 4 ili msimu latest yani 2025-2026 uwe na point 5.
Kwa hiyo Rs Berkane kupata 0 katika msimu wa 2022-2023 sio sababu ya kumfanya ashuke viwango vya ubora, hata ingetokea amepata 0 kwenye msimu wa 2023-2024 bado haikuwa factor.
Kilichomfanya ashuke nafasi ni kutokana na ule msimu wa 2019-2020 ambao alivuna pointi nyingi baada ya kuchukua ubingwa. Msimu huo umeondolewa kwenye mfumo wa 5 year ranking na kufanya zile point 5 alizozipata katika huo msimu kuzipoteza.
Simba imesogelewa na Yanga kwa gape dogo la pointi kwasababu hizi
Simba msimu wa 2020-2021 Simba alifika robo fainali na kuchukua alama 3. katika huo mwaka pointi ilikuwa ni 5. Kwa hiyo ukizidisha 3x5 unapata 15
Msimu uliofuata kabla hata ya mashindano kuanza tayari pointi za Simba hazikuwa 15 kama ilivyokuwa msimu ulioisha, pointi zilikuwa 12 kwasababu ule mwaka ulipunguzwa pointi kutoka pointi 5 hadi pointi 4.
Kwa hiyo ulikuwa ukizidisha ni 3x4=12.
Huo msimu umezidi kurudi nyuma na kila unaporudi nyuma pointi zake zinapungua na mpaka sasa 2020-2021 umekuwa na pointi 1, maana yake zile pointi 3 alizopata Simba zitazidishwa kwa 1 kufuatiwa kupungua kwa pointi kwa huo msimu.