Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Ulichoongea umekielewa kweli?Sasa nani asiyejua mechanism ya gape la 1.5?
Rs Berkane msimu wa jana alikuwa nafasi ya 6 lakini msimu huu ulivyoanza tu hata kabla ya mechi yeyote ya kimataifa kuchezwa nafasi yake tumechukua sisi unajua ni kwa nini?
Nyinyi kufikia hilo gape sio kama kuna kitu mme-earn kuizidi Simba.
Simba amepungua point kufuatia kuondolewa mwaka mmoja wa rank aliokuwa amekusanya point nyingi.
Kwenye huo mwaka kila timu ambayo ilikuwa imekusanya point nyingi lazima zipungue.
Berkane kawa chini kwasababu ya msimu wa 2022/2023 hakuwa na point.
Unasema hakuna kitu Yanga ime earn kuizidi Simba naomba ujibu maswali yafuatayo.
1) kama hakuna kitu ambacho Yanga imeongeza kuzidi Simba,je imekuaje point za Simba na Yanga zikaribiane kwa tofauti ya 1.5?
2) Huo mwaka ambao unasema point zimeondolewa, je point za Yanga zilihesabiwa? Kama hakuna yeyote aliyehesabiwa maanake hakuna uonevu hapo bali ndio utaratibu kwasababu ranking hufanywa kwa kuchukua performance ya misimu mitano hivyo kama kuna msimu wa hivi karibuni mwenzio kachukua point nyingi kuliko wewe ni lazima gap ipungue. Yaani hata hesabu tu ndogo inakushinda?
Gap ya Simba na Yanga imepungua kwasababu mbili; sababu ya kwanza ni msimu wa 2022/2023 Yanga ilikusanya point 4 kwa kucheza fainali ya CAFCC huku Simba ikipata alama 3 kwa kuishia robo fainali ya CAFCL.
Sababu ya pili ni msimu huu Simba kucheza mashindano ya CAFCC ambayo point zake ni chache kuliko wanaocheza klabu bingwa. Ingekuwa Simba msimu huu wanacheza klabu bingwa wange maintain gap lao kwa Yanga hata ikitokea wameishia hatua sawasawa. Ila kwa sasa Simba inatakiwa iiache Yanga hatua moja zaidi kwenye mashindano ama labda itokee wote Simba na Yanga wameshika nafasi ya mwisho kwenye kundi lao ndio Yanga itazidiwa kwenye rank na Simba.