Tetesi: Simba yacharuka, yazitaka saini za Pacome, Aucho Msimbazi!

Tetesi: Simba yacharuka, yazitaka saini za Pacome, Aucho Msimbazi!

Unajipa matumaini siyo! Kwanza kwenye hiyo orodha ya wachezaji niliowataja hapo, amebakia Sure Boy pekee kwenye kikosi cha sasa. Na uhakika wa kuanza tarehe 19 ni 1% tu kwa mtazamo wangu.
Kweli??
1729089499831.jpeg
 
Sasa si tulikubaliana tumeanzisha project. Hao Pacome na Aucho na uzee wao tunawapeleka wapi tena. Kuna watu wameshaanza kumtapeli Mo
 
Sasa si tulikubaliana tumeanzisha project. Hao Pacome na Aucho na uzee wao tunawapeleka wapi tena. Kuna watu wameshaanza kumtapeli Mo
Mo mwenyewe ndio anasimamia show.
 
Klabu kongwe nchini, Simba Sports Club imeingia vitani na watani zao Yanga Afrika kwenye kinyang'anyiro cha kuzisaka saini za mastaa wa klabu hiyo yenye makao makuu yake Jangwani jijini Dar Es Salaam Pacome Zouzoua na Khalid Aucho.

Mastaa hao tegemezi katika kikosi cha kwanza cha Yanga, mikataba yao inaelekea ukingoni. Pacome na Aucho ni chaguo la kwanza la kocha Gamondi tokea aingie klabuni hapo, hivyo kukosekana kwao kutaleta athari na pengine mtikisiko katika maendeleo ya klabu kiujumla.

Pacome mguu nje, mguu ndani...
Taarifa za uhakika ni kwamba Pacome tayari ameshapokea 'kishika uchumba' kutokea Simba, pamoja na kupangiwa nyumba ya kuishi ambayo anaishi hivi sasa staa huyo kutokea Ivory Coast.

Pacome ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa klabu hiyo kutokea Msimbazi kila wakutanapo na watani zao wa jadi Yanga, ametengewa fungu 'nono' ambalo kulikwepa itakuwa vigumu.

Hekaheka zote hizo zinachagizwa na mkataba wa profesa huyo wa mpira kuelekea ukingoni, na inaripotiwa anawapa wakati mgumu viongozi wa Yanga kusaini mkataba mpya.

Aucho awindwa, bado njia panda...
Klabu ya Simba imedhamiria mapinduzi katika kuimarisha kikosi chake ambacho bado hakina muunganiko wa kuridhisha kwa kumuweka kiungo punda kutokea Jangwani, Aucho katika rada.

Kiungo huyo aliyepewa hadhi ya udaktari kutokana na shughuli yake awapo uwanjani, ni injini ya kikosi cha Yanga katika kuanzisha na kutibua mashambulizi ya timu pinzani, pengo lake ni vigumu kuzibika kwa haraka ikiwa tu ataondoka klabuni hapo.

Mo Dewj amwaga hela...
Mwekezaji wa Simba Mohamed Dewj, amemwaga hela za kutosha katika kufanikisha usajili huo ambao ukifanikiwa utaacha vilio Jangwani.

Mo Dewj ambaye hapo kabla alikuwa katika wakati mgumu kwa mchakato wa Simba kuelekea katika mabadiliko kusuasua, mchakato huo umefikia pazuri na mwekezaji huyo ameonekana kufurahia hilo kwa kufungua pochi kuwezesha usajili huo.

Fei Toto Plan B...
Viongozi wa Simba wakiongozwa na mwekezaji wao Mo Dewj, wamedhamiria kuwafuta machozi mashabiki wa klabu hiyo kwa kufanya usajili wa maana kabla ya msimu huu kwisha, kwa kuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa misimu kadhaa iliyopita.

Mkakati namba moja ni Pacome na Aucho, ikishindikana kuwapata mastaa hao basi watadondokea kwa kiungo kutokea Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto'.

Kwa msaada wa chanzo changu,

Nifah.
Hujui chochote...
Naona unaropoka tu...

Ni Bora kukaa kimya kuliko kuongea Mambo ya kufikiria tu.
 
Wewe unawapigia debe hao wachezaji ili Yanga wapande dau katika kuhuisha mikataba yao inayoekekea ukingoni.
 
Level ya Aucho sio ya kuifanyia comparison Simba labda Fountain Gate kushuka chini huko ndio utawapata wachezaji sampuli yake
Hater kwenye moja na mbili. Kwenye swala la Yanga na Simba akili huwa unaziweka kando kabisa unabakia na za kuvukia barabara tu. Uliongea maneno mabovu sana kwenye michuano ya klabu bingwa msimu uliopita kuwa Yanga kutovuka makundi, ukajifanya kama Mungu vile unayepanga nani aende nani abaki. Ila sasa naona swala la point za CAF gap ni 1.5 kati ya Simba na Yanga,sijui kikivyekwa hiki kichaka cha rank mtabakiwa na nini maana ile michuano ya mualiko nayo imefutwa.
 
#NguvuMoja🦁
#YNWA 🐔
Mbona uzi wa Liverpool humu hautembelei
Uzi ule huwa nautembelea mara chache.
Hata uzi mnyama sina mazoea nao kivile.
Ila kuhusu ishu ya shabiki wa yanga kukuzimia sigara daaa🙄🙄sijapenda hiyo😳😳
Usiruhusu ushabiki wa aina hiyo
 
Back
Top Bottom