Tetesi: Simba yacharuka, yazitaka saini za Pacome, Aucho Msimbazi!

Klabu kongwe nchini, Simba Sports Club imeingia vitani na watani zao Yanga Afrika kwenye kinyang'anyiro cha kuzisaka saini za mastaa wa klabu hiyo yenye makao makuu yake Jangwani jijini Dar Es Salaam Pacome Zouzoua na Khalid Aucho.

Mastaa hao tegemezi katika kikosi cha kwanza cha Yanga, mikataba yao inaelekea ukingoni. Pacome na Aucho ni chaguo la kwanza la kocha Gamondi tokea aingie klabuni hapo, hivyo kukosekana kwao kutaleta athari na pengine mtikisiko katika maendeleo ya klabu kiujumla.

Pacome mguu nje, mguu ndani...
Taarifa za uhakika ni kwamba Pacome tayari ameshapokea 'kishika uchumba' kutokea Simba, pamoja na kupangiwa nyumba ya kuishi ambayo anaishi hivi sasa staa huyo kutokea Ivory Coast.

Pacome ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa klabu hiyo kutokea Msimbazi kila wakutanapo na watani zao wa jadi Yanga, ametengewa fungu 'nono' ambalo kulikwepa itakuwa vigumu.

Hekaheka zote hizo zinachagizwa na mkataba wa profesa huyo wa mpira kuelekea ukingoni, na inaripotiwa anawapa wakati mgumu viongozi wa Yanga kusaini mkataba mpya.

Aucho awindwa, bado njia panda...
Klabu ya Simba imedhamiria mapinduzi katika kuimarisha kikosi chake ambacho bado hakina muunganiko wa kuridhisha kwa kumuweka kiungo punda kutokea Jangwani, Aucho katika rada.

Kiungo huyo aliyepewa hadhi ya udaktari kutokana na shughuli yake awapo uwanjani, ni injini ya kikosi cha Yanga katika kuanzisha na kutibua mashambulizi ya timu pinzani, pengo lake ni vigumu kuzibika kwa haraka ikiwa tu ataondoka klabuni hapo.

Mo Dewj amwaga hela...
Mwekezaji wa Simba Mohamed Dewj, amemwaga hela za kutosha katika kufanikisha usajili huo ambao ukifanikiwa utaacha vilio Jangwani.

Mo Dewj ambaye hapo kabla alikuwa katika wakati mgumu kwa mchakato wa Simba kuelekea katika mabadiliko kusuasua, mchakato huo umefikia pazuri na mwekezaji huyo ameonekana kufurahia hilo kwa kufungua pochi kuwezesha usajili huo.

Fei Toto Plan B...
Viongozi wa Simba wakiongozwa na mwekezaji wao Mo Dewj, wamedhamiria kuwafuta machozi mashabiki wa klabu hiyo kwa kufanya usajili wa maana kabla ya msimu huu kwisha, kwa kuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa misimu kadhaa iliyopita.

Mkakati namba moja ni Pacome na Aucho, ikishindikana kuwapata mastaa hao basi watadondokea kwa kiungo kutokea Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto'.

Kwa msada wa chanzo changu,

Nifah.
Ukitaka ufagiliwe vilivyo na mashabiki wa simba, wewe waletee tu story za aina hii!!
 
Kweli nimeamini Simba na Yanga ni zaidi ya dini nchi hii! Yani mtu anarukwa na akili sababu ya ushabiki!
Kuna mjinga hapa kitaa ni Uto siongei naye na nimejiapiza maisha yangu yote toka ile mechi ya ngao ya jamii uto walioshinda 1-0 alinizimia sigara kwenye tshirt yangu mpaka ikatoboka
 
Pacome na Aucho wakafanye nini Simba?

Yani tumemuacha Chama halafu tuje tumchukue Pacome kweli?

Simba kama itaamua kufanya hivyo ni kwa lengo moja tu kuua chemistry ya Yanga lakini sio kwa mategemeo ya hao wachezaji waje kuwa mchango ndani ya timu.
Chemistry ya Yanga haiwezi kuvurugika kwa kukosekana wachezaji wawili kwenye timu. Nyinyi simba mtaendera kuwa chakula cha Yanga mpaka pale tutakoposema sasa inatosha!
 
Klabu kongwe nchini, Simba Sports Club imeingia vitani na watani zao Yanga Afrika kwenye kinyang'anyiro cha kuzisaka saini za mastaa wa klabu hiyo yenye makao makuu yake Jangwani jijini Dar Es Salaam Pacome Zouzoua na Khalid Aucho.

Mastaa hao tegemezi katika kikosi cha kwanza cha Yanga, mikataba yao inaelekea ukingoni. Pacome na Aucho ni chaguo la kwanza la kocha Gamondi tokea aingie klabuni hapo, hivyo kukosekana kwao kutaleta athari na pengine mtikisiko katika maendeleo ya klabu kiujumla.

Pacome mguu nje, mguu ndani...
Taarifa za uhakika ni kwamba Pacome tayari ameshapokea 'kishika uchumba' kutokea Simba, pamoja na kupangiwa nyumba ya kuishi ambayo anaishi hivi sasa staa huyo kutokea Ivory Coast.

Pacome ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa klabu hiyo kutokea Msimbazi kila wakutanapo na watani zao wa jadi Yanga, ametengewa fungu 'nono' ambalo kulikwepa itakuwa vigumu.

Hekaheka zote hizo zinachagizwa na mkataba wa profesa huyo wa mpira kuelekea ukingoni, na inaripotiwa anawapa wakati mgumu viongozi wa Yanga kusaini mkataba mpya.

Aucho awindwa, bado njia panda...
Klabu ya Simba imedhamiria mapinduzi katika kuimarisha kikosi chake ambacho bado hakina muunganiko wa kuridhisha kwa kumuweka kiungo punda kutokea Jangwani, Aucho katika rada.

Kiungo huyo aliyepewa hadhi ya udaktari kutokana na shughuli yake awapo uwanjani, ni injini ya kikosi cha Yanga katika kuanzisha na kutibua mashambulizi ya timu pinzani, pengo lake ni vigumu kuzibika kwa haraka ikiwa tu ataondoka klabuni hapo.

Mo Dewj amwaga hela...
Mwekezaji wa Simba Mohamed Dewj, amemwaga hela za kutosha katika kufanikisha usajili huo ambao ukifanikiwa utaacha vilio Jangwani.

Mo Dewj ambaye hapo kabla alikuwa katika wakati mgumu kwa mchakato wa Simba kuelekea katika mabadiliko kusuasua, mchakato huo umefikia pazuri na mwekezaji huyo ameonekana kufurahia hilo kwa kufungua pochi kuwezesha usajili huo.

Fei Toto Plan B...
Viongozi wa Simba wakiongozwa na mwekezaji wao Mo Dewj, wamedhamiria kuwafuta machozi mashabiki wa klabu hiyo kwa kufanya usajili wa maana kabla ya msimu huu kwisha, kwa kuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa misimu kadhaa iliyopita.

Mkakati namba moja ni Pacome na Aucho, ikishindikana kuwapata mastaa hao basi watadondokea kwa kiungo kutokea Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto'.

Kwa msada wa chanzo changu,

Nifah.
Nimependa ulivyohitimisha simulizi yako Mjukuu,

"Kwa msada wa chanzo changu.."

Kwa kuwa Mimi na Mkwe wangu wote ni Wanyama, na hii habari inatunufaisha zaidi sisi mashabiki wa Simba SC, nitamshauri Mkwe wangu akutafutie Jersey ya Simba kama zawadi yako Mjukuu ili uhamie upande wetu 🤗
 
Uzuri ni kwamba Young Africans ni timu na sio mchezaji mmoja. Kwenye mechi ya Young Africans vs Mamelodi hawakuwepo Pacome, Aucho, na Yao lakini kila mmoja kawa shahidi jinsi gani Mamelod walivyokutana na upinzani mkubwa kutoka Young Africans. Hivyo ni rahisi kuziba mapengo ya hao wachezaji kama lilivyozibwa pengo la Lomalisa, nina imani na scout ya Yanga italeta chuma zaidi ya hao hivyo wachukueni tu wala chemistry ya Yanga haitovurugika kama ilivyoshindikana kuvurugika baada ya kuondoka Mayele, Feisal, Djuma Shaban na Bangala na benchi zima la ufundi.
Sasa Pacome mechi ya Mamelody ambayo timu nzima ilikuwa nyuma ya mpira angekuwa na impakti gani?
 
Back
Top Bottom