Utapendeza sana hata mimi naionaTFF mpya inakuja na mu 40.
Hiyo sawa ila wakati wa mechi wengi tunakusanyika Bar ambako hivyo vinywaji havipo,ndio maana nikasema bia na soda.Timu ikishinda Watu watazungusha round za vinywaji vya timu zao.Tena mkorofi anaweza kuwanunulia Wanywaji wote hapo Bar Bia za timu yake.Ushindi unapagawisha na ndio point yangu ilipo.Gsm, Mo, Azam hao wote wana vinywaji vyao na wanawatumia wachezaji wa timu wanazomiliki au kudhamini kutangaza bidhaa zao.
Upande wa vinywaji naona wapo smart zaidi kudhibiti bidhaa feki ukilinganisha na huko kwenye jersey.Na hili la jersey inasemwa Wahusika wapo humo humo.Ni wazo zuri shida utekelezaji wake ila kariakoo hela nyingi sana hata kupitia jersey fake (low quality) wanapiga hela sana