Girland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2016
- 2,489
- 4,253
Baada ya kichapo tena cha mbwa koko aliyekula mboga ya mchana kutoka kwa mahasimu wetu wa "mabonde kuinama "kwenye mafuriko. Kama mshabiki, mnazi, mkereketwa ninashauri yafuatayo:
1.TATHMINI IFANYIKE KUHUSU MWENENDO WA KLABU YETU NDANI NA NJE YA UWANJA.
Lazima wataalamu watuambie je kila mmoja kwenye uongozi anayafanya majukumu yake ipasavyo?
Je kikosi chetu kina mapungufu yapi kiufundi? Mechi ya watani ni kipimo kizuri cha kuonyesha wapi panavuja
2.USAJILI WA MAANA UFANYIKE
Hatuhitaji tena ngonjera za Mwenyekiti kupiga picha na Manzoki wala kuambiwa eti Eto'o amemkubali Onana, tunataka kuona Simba ikiwa na kikosi kipana chenye Muunganiko.
Tuulizie bei ya Feisal pale Kati atafaa Sana,Na Bangala.
3 MZEE WA OBJECTIVES APEWE MTIHANI,
Haitoshi kutuambia Simba klabu kubwa, tunataka kuiona ikifanya vizuri uwanjani. Wapi Mpira Biriani kocha aambiwe Kama hawezi kuleta muunganiko wa kikosi arudi kwao Brazil.
Vipi Shabiki Mwenzangu tufanye nini kurejea kwenye ufalme wetu maana dozi ya leo si kitoto!