Simba Yashika Nafasi ya 05 kwa Ubora Yanga Wakiwa 12 Kwa Mwaka 2025

Simba Yashika Nafasi ya 05 kwa Ubora Yanga Wakiwa 12 Kwa Mwaka 2025

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Klabu ya Simba SC imeshika nafasi ya tano kwenye orodha ya vilabu bora Barani Afrika kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Simba SC wamekusanya jumla ya alama 48, wakizidi vilabu vikubwa kama Pyramids FC, Wydad Athletic Club na Zamalek SC ambavyo vimefuata nyuma yao kwenye msimamo huo.

Mafanikio haya yametokana na mwendelezo wa kiwango cha juu cha Simba katika mashindano ya CAF, ambapo wamefanikiwa kufika robo fainali mfululizo na msimu uliopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho.

Simba SC inaendelea kuthibitisha ubora wake na nafasi yake kama moja ya nguvu kubwa za soka la Afrika

Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) inashika nafasi ya 12 kwenye viwango vya ubora Barani Afrika, ikiwa na alama 34, ikizidiwa na wapinzani wao wa jadi Simba SC kwa alama 14, ambao wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 48.

Malengo makubwa ya Yanga SC ni kuwa miongoni mwa vilabu bora zaidi Barani Afrika. Ili kufanikisha hili, wanapaswa kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya kimataifa. Iwapo mwaka huu watafanikiwa kufika angalau robo fainali ya mashindano ya CAF, nafasi yao ya kupenya na kuingia kwenye Top 10 itakuwa kubwa.

Yanga SC inaendelea kuwekeza katika kikosi chenye ushindani na mikakati ya kuongeza uzoefu wa kimataifa ili kutimiza ndoto ya kuwa timu bora Afrika
 

Attachments

  • 1754638812915.jpg
    1754638812915.jpg
    260.2 KB · Views: 108
hivi club iki rank juu kuna kazawadi fulani wanapewa?
Unapata urahisi wa kucheza na wapinzani ambao hawana kiwango kikubwa kwenye mashindano ya CAF kwenye hatua za awali. Na kwenye makundi wanapanga timu kulingana na rank hivyo ukiwa na points nyingi za rank unakuwa kwenye pot nzuri eiza Pot A au Pot B. Mfano hapo kwenye hizo rank, hizo timu ambazo zipo namba 1 mpaka 4 kama zote zitaingia hatua ya makundi watakuwa Pot A na haziwezi kukutana zenyewe labda mpaka robo fainali. Kinyume na hapo hakuna zawadi yoyote unapata.
Ziada! Msimu huu Simba na Yanga kama wote watafuzu kuingia hatua ya makundi basi wote watakuwa Pot B maana kuna timu nne ambazo zipo juu kwenye rank lakini hazijafuzu kucheza CAF Champions league.
 
Halafu wote wawili wanaanzia raundi ya kwanza klabu bingwa pamoja na rank zao
Ndio hivyo upo sahihi kabisa, kuanzia hatua ya kwanza au kutokuanza hatua hiyo inategemea idadi ya timu ambazo zimethibitisha kushiriki kwa msimu husika.
Msimu huu jumla ya timu ambazo zitashiriki CAF champions league ni 62, kwa hiyo timu ambazo hazitaanzia hatua ya kwanza ni mbili tu. Zinabaki timu 60 ambazo wakicheza hatua ya kwanza zinabaki 30, zinaungana na zile mbili kucheza hatua ya pili hapo zitabaki timu 16 ambazo ndio zitacheza hatua ya makundi.
 
Unapata urahisi wa kucheza na wapinzani ambao hawana kiwango kikubwa kwenye mashindano ya CAF kwenye hatua za awali. Na kwenye makundi wanapanga timu kulingana na rank hivyo ukiwa na points nyingi za rank unakuwa kwenye pot nzuri eiza Pot A au Pot B. Mfano hapo kwenye hizo rank, hizo timu ambazo zipo namba 1 mpaka 4 kama zote zitaingia hatua ya makundi watakuwa Pot A na haziwezi kukutana zenyewe labda mpaka robo fainali. Kinyume na hapo hakuna zawadi yoyote unapata.
Ziada! Msimu huu Simba na Yanga kama wote watafuzu kuingia hatua ya makundi basi wote watakuwa Pot B maana kuna timu nne ambazo zipo juu kwenye rank lakini hazijafuzu kucheza CAF Champions league.
Upo sahihi kabisa umeacha tu swala la kupata upendeleo wa kuanzia ugenini kisha kumalizia nyumbani.
 
Nafasi ya 5 ma hata FIFA haikutambui na haujawahi kushiriki CAF Champions 😂😂😂
20250703_103644 (1).jpg
 
Hii Ndiyo 4 Year Ranking inayotambuliwa na FIFA, Hiyo ya kwenu mpatieni Ngunguboy😂😂😂

20250703_103644 (1).jpg
 
Back
Top Bottom