Mt. Joseph parokia ya Ivory Coast
Kutoka kwenye ukurasa wa James Sheka
Mfahamu, Joseph Guede Gnadou ambaye ni mchezaji mpya wa kikosi Cha Yanga SC raia wa Ivory coast, huyu ni mchezaji mwenye umri wa miaka 29 ambaye kazaliwa mwaka 1994 huko nchini Ivory coast.
Mchezaji huyu ameanzia soka lake huko kwao Ivory coast katika Klabu ya USC BASSAM FC mnamo mwaka 2017 hii ilikuwa tarehe 01/08/2017 katika msimu wa 2017/2018. Msimu uliofuata wa 2018/2019 tarehe 01/07/2018 akajiunga na Klabu ya soka ya AFAD DJEKANOU FC ya huko huko kwao Ivory coast.
Baada ya kuhudumu katika kikosi hicho Kwa mida wa msimu mmoja tu akaondoka na kwenda nchini Morocco kujiunga na Klabu ya soka ya Far Rabbat FC ambayo Kwa Sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa YANGA SC bwana Mohamed Nabi, huu ulikuwa msimu wa 2019/2020.
Baadae msimu wa 2021/2022 tarehe 07/08/2021 akatolewa Kwa mkopo kwenda kujiunga na Klabu ya soka ya EMIRATES CLUB ya huko nchini Palestina, na baada ya mkopo wake kumalizika akarudi tena Far Rabbat FC ya Morocco tarehe 30/06/2022.
Msimu wa 2022/2023 uliisha akiwa Hana timu yoyote maana yake ni kwamba hakucheza msimu mzima mpaka unaisha Kwa sababu hakuwa na timu. Na msimu uliofuta wa 2023/2024 ambao ndio huu uko nusu Sasa hivo alipata timu huko nchini Uturuki katika ya TUZLASPOR FC hii ilikuwa tarehe 02/08/2023 akiwa kama mchezaji huru maana msimu wa nyuma yake hakuwa na timu.
Katika timu hii alifanikiwa kucheza Michezo 4 tu pekeee na hakuna goli lolote alilofunga Ndani ya timu yake hiyo ya Uturuki inayoshiriki ligi daraja la Pili lakini pia akiwa na Kadi ya njano Moja.
Ndani ya hii timu yake ya Uturuki, hakuweza kudumu Sana, badala yake alidumu Kwa muda wa mwezi mmoja na siku 13 pekee yaani alikaa siku 43 pekee kuanzia tarehe 02/08/2023 hadi tarehe 15/09/2023 Klabu hii ikavunja MKATABA wake kutokana na kiwango kibovu alichokionesha Ndani ya timu hiyo.
Na kuanzia hapo hakuwa na timu tena Kwa muda wa MIEZI 4 hadi hii Leo, Kwa maana hiyo Klabu ya Yanga imemsajili mchezaji ambaye hakuwa na timu yoyote maana yake ni kwamba wamesajili akiwa huru.
Tujiulize kidogo hapa, hivi timu zetu za Tanzania hazina uwezo wa kusajili mchezaji ambaye Yuko ACTIVE yaani ambaye anacheza na ana mkataba na timu yake?. HUYU NDIYE, (JOSEPH GUEDE GNADOU).#HOLYFINGERS