Jibu la swali lako linajibika hapa.
Ni mchezaji yupi iwe Simba au wa Yanga ambaye ni wa ndani anayekipwa mshahara mkubwa kuliko mchezaji wa kimataifa.
Mshahara ni maswala ya negotiations
Wote tunajua sababu za wachezaji wa ndani kulipwa mshahara mdogo husababishwa na mambo mengi.
Sababu ya kwanza ni shauku ya wachezaji wenyewe kutamani kucheza katika hivi vilabu vikubwa wakiamini huku ndio sehemu sahihi ya wao kuweza kukuza majina yao.
Hiyo inafutuatia na wao kuridhika na mshahara wowote ambao watakuwa approached na hizo timu.
Lakini pia hata kulingana na mishahara ambayo walikuwa wanaipata kwenye timu zao ambazo ni ndogo.
Mishahara ile ilikuwa ni midogo so inapotokea Simba na Yanga wanapomfuata mchezaji na kumuongezea kiasi kidogo cha juu kutoka kwenye ule mshahara wake, mchezaji anakuwa motivated na kukubali.
Lakini sababu nyingine ni swala la udalali (middle men) kulingana na wachezaji wa ndani kutamani kucheza kwenye hivi vilabu basi kuna wadau ambao wamekuwa wakitumia hiyo fursa kupiga hela.
Mchezaji anaweza kusajiliwa kwenye makaratasi kukaandikwa mshahara mnono pamoja na signing fee lakini kiasi kingi cha pesa kinaishia kwa middle man.
Na ndio maana huwezi kuona wachezaji hao wakiitwa kwenye vilabu vya nje wanaendelea kulipwa mishahara midogo kama ambayo walikuwa wakilipwa huku.