Kabumbu la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup CAFCC, hatua ya robo fainali kuendelea kutimia vumbi leo April 24, 2022 ambapo wenyeji Orlando Pirates wanapambana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika mchezo wa mkondo wa pili, kwenye dimba la Orlando Stadium Nchini Afrika Kusini.
Ni mchezo muhimu kwa timu zote kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali, ambapo Simba SC anaingia kwenye mchezo huu akiwa tayari na mtaji wa bao moja alilopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku [TZ] saa 12: 00 Jioni [SA] Usikose Ukaambiwa, Gumzo Ndipo Hapo.
Ikiwezekana Jopo zima la Wanasimba na Wadau wote tuwepo hapa ubaoni JF.
Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana
View attachment 2198524