Simba yatolewa kwa penati 4 - 3 | Orlando Stadium

Simba yatolewa kwa penati 4 - 3 | Orlando Stadium

Ghazwat huwa nikiona hilo jina naona kama jitu moja la Egypt huko Al Ahly

Almounem, Zaki au gomaa atakua😁

images (1).jpeg

Gomaa
images.jpeg


Zaki

Ghazwat kati ya hao ni yupi wewe?😁
 
Nilimwambia pilipili isoila ,yakuwashia nn??


Aache Wanasimba tutangaze zetu.


Sisi mbona hatuna shobo na mtu!!.
MAKOLOKOLO mnafurahisha sana, kwa taarifa yako hapo mpo kimya kama maji ya mtungini, lakini kimbembe ni ikiwa mtashinda hiyo mechi dhidi ya Orlando Pirates, utaona jinsi gani MAKOLOKOLO FC huwashwa washwa na YANGA FC hata kama hachezi naye ana kwa ana [emoji23]
 
Kabumbu la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup (CAFCC), hatua ya robo fainali kuendelea kutimua vumbi leo April 24, 2022 ambapo wenyeji Orlando Pirates anapambana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika mchezo wa mkondo wa pili, kwenye dimba la Orlando Stadium Nchini Afrika Kusini.

Ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali, ambapo Orlando wakihitaji ushindi tu huku wakizuia Simba wasipate bao. Na Simba SC anaingia kwenye mchezo huu akihitaji sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele kwani tayari ana mtaji wa bao moja alilopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa April 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Pablo Franco Martin amesema kuwa wanakwenda uwanjani kujaribu kushinda mchezo huo ili kuweza kutinga hatua ya Nusu Fainali huku Kiungo Left Footer Magician, Rally Bwalya akisema wanajua umuhimu wa mchezo huo.

"Umepita muda mrefu tangu timu kutoka Tanzania kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Afrika. Tunajua umuhimu wa mchezo huu. Hautakuwa rahisi kwakuwa Orlando Pirates wapo nyumbani. Lakini Sisi tuna faida ya ushindi wa nyumbani ila hatutatumia kigezo hiki kwenye mchezo huu hivyo tunahitaji matokeo ya ushindi ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote". amesema Rally Bwalya.

Simba SC ikishinda Tanzania imeshinda. Kila la heri wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa Simba SC.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku [TZ] saa 12: 00 Jioni [SA] Usikose Ukaambiwa..Jopo zima la Wanasimba Na Wengine na Wadau wa Soka wote tuwepo hapa ubaoni JF.

Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana

....... Ghazwat.......


View attachment 2198524
Kila la heri mnyama
 
Simba atafungwa nyingi tu na Kisha kutolewa nje ya mashindano.
 
Naona leo mmewahi kujianzishia uzi

Guvu moya

All the best Orlando pirates 😂😂😂😂😂😂😂

Friends of namungo msikasirike sana
 
Back
Top Bottom