Mzee Wa Kazi Chafu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2022
- 2,245
- 4,966
Kwame Peprah Lazima Akwamishe Watu Leo [emoji4]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila laheri mnyama....Kabumbu la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup (CAFCC), hatua ya robo fainali kuendelea kutimua vumbi leo April 24, 2022 ambapo wenyeji Orlando Pirates anapambana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika mchezo wa mkondo wa pili, kwenye dimba la Orlando Stadium Nchini Afrika Kusini.
Ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali, ambapo Orlando wakihitaji ushindi tu huku wakizuia Simba wasipate bao. Na Simba SC anaingia kwenye mchezo huu akihitaji sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele kwani tayari ana mtaji wa bao moja alilopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa April 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kocha Pablo Franco Martin amesema kuwa wanakwenda uwanjani kujaribu kushinda mchezo huo ili kuweza kutinga hatua ya Nusu Fainali huku Kiungo Left Footer Magician, Rally Bwalya akisema wanajua umuhimu wa mchezo huo.
"Umepita muda mrefu tangu timu kutoka Tanzania kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Afrika. Tunajua umuhimu wa mchezo huu. Hautakuwa rahisi kwakuwa Orlando Pirates wapo nyumbani. Lakini Sisi tuna faida ya ushindi wa nyumbani ila hatutatumia kigezo hiki kwenye mchezo huu hivyo tunahitaji matokeo ya ushindi ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote". amesema Rally Bwalya.
Simba SC ikishinda Tanzania imeshinda. Kila la heri wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa Simba SC.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku [TZ] saa 12: 00 Jioni [SA] Usikose Ukaambiwa..Jopo zima la Wanasimba Na Wengine na Wadau wa Soka wote tuwepo hapa ubaoni JF.
Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana
....... Ghazwat.......
View attachment 2198524
Yote heri. Mnyama apite tuNimeliona goli moja SIMBA 1-0
kuna mafundi 2 mmoja wa Mlingotini mwingine Isevya Tabora wote wameona Simba ana goli moja.Nimeliona goli moja SIMBA 1-0
UkomeNaona leo mmewahi kujianzishia uzi
Guvu moya
All the best Orlando pirates 😂😂😂😂😂😂😂
Friends of namungo msikasirike sana
Naunga mkonoMuhimu asianze mugalu tu
Teh teh teh 😂😂 hizi kamati za ufundi hizi....kuna mafundi 2 mmoja wa Mlingotini mwingine Isevya Tabora wote wameona Simba ana goli moja.
mechi ipo South lakini huku bongo watu atulali[emoji28][emoji23]Teh teh teh [emoji23][emoji23] hizi kamati za ufundi hizi....
Kuna shabiki mmoja wa mfuga ng"ombe kasema Manyele amchukue na yeye akamfanyie mambo nimewaza huko utopoloni kuna nini nimekosa jibu..Tuliw ww unafata nini hapa?Kila lakheri Orlando Pirate piga hao Makolo