Simba yatolewa kwa penati 4 - 3 | Orlando Stadium

Simba yatolewa kwa penati 4 - 3 | Orlando Stadium

Hahaha, kusema kweli leo zikiwa chache ni tatu bila. Kwa zile dakika kumi za mwisho walizocheza pale Lupaso nikiangalia na backline yetu na viungo wetu alafu lile pira walipige dakika tisini hakuna pa kutokea.
Tutarudi saa tatu usiku.
 
Si Tunacheka Tu Wanavyo Danganyana [emoji23]
orlando-pirates-21-22-kit-2.jpg
 
Kila la kheri Simba Fc [emoji91]
Nguvu moja
 
Kabumbu la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup (CAFCC), hatua ya robo fainali kuendelea kutimua vumbi leo April 24, 2022 ambapo wenyeji Orlando Pirates anapambana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika mchezo wa mkondo wa pili, kwenye dimba la Orlando Stadium Nchini Afrika Kusini.

Ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali, ambapo Orlando wakihitaji ushindi tu huku wakizuia Simba wasipate bao. Na Simba SC anaingia kwenye mchezo huu akihitaji sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele kwani tayari ana mtaji wa bao moja alilopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa April 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Pablo Franco Martin amesema kuwa wanakwenda uwanjani kujaribu kushinda mchezo huo ili kuweza kutinga hatua ya Nusu Fainali huku Kiungo Left Footer Magician, Rally Bwalya akisema wanajua umuhimu wa mchezo huo.

"Umepita muda mrefu tangu timu kutoka Tanzania kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Afrika. Tunajua umuhimu wa mchezo huu. Hautakuwa rahisi kwakuwa Orlando Pirates wapo nyumbani. Lakini Sisi tuna faida ya ushindi wa nyumbani ila hatutatumia kigezo hiki kwenye mchezo huu hivyo tunahitaji matokeo ya ushindi ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote". amesema Rally Bwalya.

Simba SC ikishinda Tanzania imeshinda. Kila la heri wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa Simba SC.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku [TZ] saa 12: 00 Jioni [SA] Usikose Ukaambiwa..Jopo zima la Wanasimba Na Wengine na Wadau wa Soka wote tuwepo hapa ubaoni JF.

Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana

....... Ghazwat.......

View attachment 2198524
Mungu ibariki SIMBA
Screenshot_20220424-083432.jpg
 
Leo ndio tunatoka rasmi kwenye michuano ya CAF kwa msimu huu...all the best Simba mmepambana kwa kiasi chenu!!
Watakutukana, watakukejeli! Lakini ulicho kiandika hapa, ndiyo ukweli wenyewe. Yaani ukweli mchungu.

Na wakirudi Bongo, wanakutana na kipigo kingine tena cha ✌️ bila, tarehe 30!
 
Back
Top Bottom