Simba yatwaa Ngao ya Jamii kwa Penati 3-1 dhidi ya Yanga, Ally Salim awa shujaa wa mchezo

Simba yatwaa Ngao ya Jamii kwa Penati 3-1 dhidi ya Yanga, Ally Salim awa shujaa wa mchezo

Kaka..

Mie sijaridhika na mpira tuliocheza simba, utopolo kaupiga mwingi zaidi yetu, dk 90 watu presha juu.

Nilisema na ninarudia kusema, simba tunasajili kwa mihemko, toka dirisha lipo wazi, simba tuna shida katika midfield, timu inaongeza mawinga na washambuliaji, wakati tulionao tu wengine hawachezi.

Kocha bado ana shida na phiri, sioni wa kumuweka benchi phiri pale simba, huo ni ukweli uliokuwa uchi.

Hii game nilikuwa naiangalia sina presha nilikuwa nategemea kufumgwa muda wowote.
Ni mapema sana kuwahukumu wachezaji. Bado wanajitafuta
Msimu uliopita tulifungwa na yanga na kombe wakachukua na tukafika robo fainali champion league.
 
UTOPOLO[emoji23][emoji23][emoji23][emoji196][emoji196][emoji196][emoji196][emoji196][emoji196][emoji196]
 
Picha la kutisha
simbasctanzania-20230813-0001.jpg
realclatouschama-20230813-0001.jpg
 
Hapana Sajili hatujafanya mbovu.

Kocha tu ndio hana mbinu ameshindwa kuwa na timing ya kujia hitaji la mchezo linataka aina gani ya formation.

Simba tuna utajiri wa Viungo

Tunao viungo wakutosha

1. Kanoute
2. Mzamiru
3. Ngoma
4. Abdallah Hamis

Moses Phiri sio wakuwekwa bench na Bocco na ndio hapo tunarejea kwenye hoja ambayo inatuunganusha wote kuwa Kocha ana matatizo.

Ila amini kuwa tumesajili vizuri tumekosa mwalimu ambaye anaweza kuwa na mbinu za kuifanya timu iwe tishio pindi inapokuwa na mpira na pindi ikiwa haina mpira.
Katika hao viungo wa4 ni ngoma tu anajua boli, huyo hamisi bado sijamtizama vizuri.

Na je tutashiriki michuano yoote, tukiwa na hao viungo wa4?
Tizama positions nyingine, viongozi wanasajili hovyo.
Wasidizi wa kuwakaribia kapombe na tshabalala hakuna.
 
Yaani Amina Kyando hafai kbs....Kwa Maoni ya Wana Utopolo...

Na Huyu Jonesya Rukya Hafai....Kwa Maoni ya Wana Utopolo ....

Sasa next Match Mleteni Hersi au Mzungu pori...!

Ndani ya 90' ....mnawapa majukumu mazito wachezaji, Urefa na Kucheza pia..! Ndo mana wamekosa penati...
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Brazil 1994, Italy, 2006 na Argentina 2022 walichukua kombe la dunia kwa penalty kama hawajui hao, pengine hawakuwepo kabisa duniani au walikuwa wanakula mtindi wa mama. Najua wengi wameona ya mwaka jana ndiyo maana wanaona kitu cha ajabu!
Watoto wadogo hawawezi kuelewa...(In TID voice.)
 
Sema mkuu baadhi ya tabiri zako kwenye mpira huwa nazikubali sana, japo ile ya Aucho umekosea kidogo uliposema atapaisha japo kukosa amekosa, kuna ile moja ya World Cup mwaka jana

Mwanzoni kabisa mwa michuano baada ya Argentina kufungwa na Saudi Arabia na watu kuanza kuitabiria kuwa haitafika mbali, ukatabiri kuwa ndio itachukua kombe na ukatolea mfano wa Spain, ilivyofungwa na Switzerland kwenye mechi yake ya kwanza kule South Africa kwenye World Cup 2010 hadi kufanikiwa kuchukua WC

Kuna watu nikiona comments zenu kuhusiana na mpira najua hapa huyu kaongea uhalisia kaweka ushabiki pembeni ila kuna wengine akitabiri unaona kabisa huyu kacomment kwa mahaba tu
Nashukuru mkuu🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Katika hao viungo wa4 ni ngoma tu anajua boli, huyo hamisi bado sijamtizama vizuri.

Na je tutashiriki michuano yoote, tukiwa na hao viungo wa4?
Tizama positions nyingine, viongozi wanasajili hovyo.
Wasidizi wa kuwakaribia kapombe na tshabalala hakuna.
Kanoute na Mzamiru unawa exclude?

Viungo wa nne kwa mtazamo wangu naona wanatosha kabisa.

Sajili ya hovyo ni ipi ebu point hata moja kama mfano.

Leo una haki ya kusema vyovyote kwasababu timu haikucheza kimkakati

Lakini Kocha akiisuka vizuri utaniambia.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Sahihi kabisa dada. Brazil ilichukua kombe la dunia 1994 dhidi ya Italy kwa mikwaju ya Penalty, mwaka 2006 Italy ilichukua kombe la dunia dhidi ya Ufaransa kwa mikwaju ya Penalty na 2022 Argentina ilichukua kombe la dunia dhidi ya Ufaransa kwa mikwaju ya Penalty. Wengine historia hiyo hawaijui, ama walikuwa wananyonya au hawajazaliwa kabisa!
Watoto wadogo wataelewa wapi hizo mambo Mkuu[emoji1787]
 
Kanoute na mzamiru ni wavunja kuni, hawana comman kwenye kiungo, hawawezi kutuliza timu, kati yao sijaona kiungo wa kuweka mfukoni viungo wa wapinzani, akawa anatamba yeye tu pale kati,pasi zao nyingi sio za kushambulia, hawana macho ya pasi hatari, kidoogo mzamiru ila kanoute ndio kabisa sio press resistant... Kibaya zaidi hawajui kukaba ni wanacheza rafu za hovyo, wanapaniki haraka.
Kanoute na Mzamiru unawa exclude?

Viungo wa nne kwa mtazamo wangu naona wanatisha kabisa.

Sajili ya hovyo ni ipi ebu point hata moja kama mfano.

Leo una haki ya kusema vyovyote kwasababu timu haikucheza kimkakati

Lakini Kocha akiisuka vizuri utaniambia.
 
Kanoute na mzamiru ni wavunja kuni, hawana comman kwenye kiungo, hawawezi kutuliza timu, kati yao sijaona kiungo wa kuweka mfukoni viungo wa wapinzani, akawa anatamba yeye tu pale kati,pasi zao nyingi sio za kushambulia, hawana macho ya pasi hatari, kidoogo mzamiru ila kanoute ndio kabisa sio press resistant... Kibaya zaidi hawajui kukaba ni wanacheza rafu za hovyo, wanapaniki haraka.
Mechi ya Derby tulioshinda mbili hukuona kazi kubwa aliyofanya Mzamiru na Kanoute?

Tena wakati huo Yanga ilikuwa na mido ngumu chini ya Aucho na Bangala sio kama hivi sasa ilivyo.
 
Onyo; Wakwepeni Utopolo popote mtakapokutana kwa angalau Masaa 72 Yaishe...! Sbb bado Wamejaa hasira, ingawa haileweki hasira hizi ni dhidi ya nani?

Refa..!
Gamondi..!
Wachezaji..?
Diarra...!
Ili Kuepuka ngeu..!
 
Back
Top Bottom