Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

Waziri anayehusika na utumishi Simbachawene asema asilimia 40 ya wafanyakazi wa serikali ni mizigo

swali kwa nini hawaachishwi kazi? Wapishe wengine?

Serikali kwa nini inaendelea kuwakumbatia?

-------

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama.

Aidha, Mhe. Simbachawene amesema kumeibuka tabia ya baadhi ya Watendaji wakuu hao pindi Mtumishi mwenye sifa za ziada anapohamia kwenye Taasisi anayoiongoza hupata hofu na kutompangia najukumu kwa hisia kuwa ametumwa kumchunguza a au kuchukua nafasi yake

Ameeleza kuwa tabia hiyo kwenye utumishi wa umma haikubaliki na wale wenye tabia hiyo wajirekebishe haraka kwani Taasisi hizo wanazoziongoza ni za umma na sio mali yao binafsi

Katika hatua nyingine, Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu kwa wananchi, Mhe. Simbachawene amezitaka Taasisi za Umma kutoa huduma za kidijitali kutokana na fursa hiyo

Vilevile, Mhe. Simbachawene amezitaka Taasisi za Umma ambazo hazijaanza kutumia mfumo wa kidijitari wa e-Mrejesho ziingie mara moja la sivyo zitachukuliwa hatua kali na Ofisi anayoiongoza.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, ( e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba aliwashukuru washiriki wa kikao hicho cha jumla 1526 ya ushiriki wao ambapo jumla ya mada 18 ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na kujiwekea mikakati ya kukabiliana na changamoto za usalama wa mtandao Serikalini.

Amesema kikao hicho kimejadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Serikali Mtandao pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuchangamkia fursa ya kujifunza teknolojia mpya zinazoibukia ili kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani kote.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe.Festo Kiswaga ameishukuru e-GA kwa kuendelea kuuamini Mkoa wa Arusha ikiwa ni mara ya tano sasa vikao hivyo vimekuwa vikifanyika Mkoani humo hali iliyopelekea Mkoa huo kuwa wanufaika wakubwa wa kiuchumi pamoja na kuwa wadau namba moja wa matumizi ya Serikali Mtandao.

Naye Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka amesema Ofisi yake itasimamia na kufanyia kazi maazimio yote yaliyowasilishwa leo na kuhakikisha utekelezaji wake unawasilishwa katika kikao kijacho

Pia, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya e-GA, Dkt. Jasmine Bunga amesema kikao kazi hicho kimekuwa muhimu kwa washiriki ambapo mbali ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili pia wamejiwekea mikakati ya kuendelea kujenga Serikali ya kidigitali.

Amesema lengo ya kujiwekea mikakati hiyo ni kuhakikisha Serikali inapiga hatua kubwa kwenye matumizi ya mifumo ya TEHAMA itakayoleta tija na ufanisi wa hali ya juu katika utoaji wa huduma bora za haraka na za uhakika kwa wananchi.
Tunakataa! Ni zaidi ya hapo! At least 75%
 
Wengine wapo mtaani mwaka wa Tano wanaendelea na mishe zao na wakipokea mishahara yao kila mwezi ,hukuvwengine wameajiriwa sekta binafsi wamesimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za hela ambayo haifiki hata robo ya mshahara wake so wanakula mishahara miwili miwili huku wanaingiza na serikalini wanaendelea kuingiza pia wakiwa nje ya kazi
 
Mfanyakazi amemaliza kazi,halafu hataki kuondoka kwa vile saa ya kuondoka haifaki.
 
40 percent is just too much of a burden to shoulder. How did they hire the employees who have no value addition.

Results ya employment ya watoto wa mjomba, shangazi etc Kama wanajuwa ni mzigo, basi wawatoe!!

Kiongozi huwezi kutoa kauli kama hiyo hadharani halafu na solution huna. Ni bora ukae KIMYA

Naona waziri ndio mzigo kama tatizo umeliona unaanza kulalamika bila kutoa maamuzi. You are the biggest problem
Kwa uzoefu wangu kwa serikalini lazima kuwe na mzigo tena asilimia ni zaidi ya hiyo .Sababu ni ndogo ndogo tu wala sio kubwa sana.

Wafanyakazi wengi wa serikali ni watu waliojihakikishia mshahara then wanatafuta njia ya kwenda mbele zaidi ,ishu kama kwenda kusoma ni bora wafute ; kazini kwetu napiga vitengo vitatu kwa pamoja ,hao wawili wameenda kusoma tena mwaka huu na wengine wanaenda .Kiufupi ufikishaji wa huduma kama ilivyokusudiwa ni zero kila mtu anatafuta vyeo.

Mlundikano wa wafanyakazi sehemu moja kutokana na sababu za kimazingira ,watu hupenda kujilundika mkoa fulani kuliko mwingine .Matokeo yake sehemu za mijini watu ni wengi mpaka hawafanya kazi wengine meanwhile huko kijijini hakuna watu .

Ruhusa za hovyo hususani hizi za kuumwa ,kuuguza mzazi ,mke au mtoto ni hatari sana mbaya zaidi kama mzazi itabidi mtu aende mkoani huko maana hafanyi kazi mkoa waliopo wazazi wake. Haya mambo ni kawaida sana waliokuwa na familia ni changamoto ,mtu miezi yuko Muhimbili kuuguza mtoto wake sio rahisi kuepuka mambo hayo.​
 
Mnaandaliwa kisaikolojia something fishy called redundance is coming,,,,,,,,,,,,,
 
Je ni asilimia ngapi ya wanasiasa ni mzigo?
Kabla ya kutaka kutoa kibanzi machoni pa mwenzake, tafari mwenendo wako
 
Kwa uzoefu wangu kwa serikalini lazima kuwe na mzigo tena asilimia ni zaidi ya hiyo .Sababu ni ndogo ndogo tu wala sio kubwa sana.

Wafanyakazi wengi wa serikali ni watu waliojihakikishia mshahara then wanatafuta njia ya kwenda mbele zaidi ,ishu kama kwenda kusoma ni bora wafute ; kazini kwetu napiga vitengo vitatu kwa pamoja ,hao wawili wameenda kusoma tena mwaka huu na wengine wanaenda .Kiufupi ufikishaji wa huduma kama ilivyokusudiwa ni zero kila mtu anatafuta vyeo.

Mlundikano wa wafanyakazi sehemu moja kutokana na sababu za kimazingira ,watu hupenda kujilundika mkoa fulani kuliko mwingine .Matokeo yake sehemu za mijini watu ni wengi mpaka hawafanya kazi wengine meanwhile huko kijijini hakuna watu .

Ruhusa za hovyo hususani hizi za kuumwa ,kuuguza mzazi ,mke au mtoto ni hatari sana mbaya zaidi kama mzazi itabidi mtu aende mkoani huko maana hafanyi kazi mkoa waliopo wazazi wake. Haya mambo ni kawaida sana waliokuwa na familia ni changamoto ,mtu miezi yuko Muhimbili kuuguza mtoto wake sio rahisi kuepuka mambo hayo.​
📌wewe kama huna kichwa cha shule baki na certificate yako.Acha wenzako watafute GREEN PASTURE in their ways.

📌Hutaki watu waumwe tengenezeni maroboti yafanye kazi 24/7/365days.

📌Kuna siku 14 za mwaka kwa kila mtumishi kwaajili ya mambo ya kijamii na dharura.

📌Ili watu wasirundikane hiyo mikoa yenye kuchangamka au mijini sambazeni maendeleo in equal distribution katika mikoa yote.Mngeweza hata kuwapa vipaumbele wafanyakazi wa migombani huko kwa vitu kama mikopo nafuu,nyumba na allowance za hapa na pale.Hampo inovative na bado mnalilia efficiency kwa wafanyakazi wenu.

📌Nchi hii kila mtu analalama hata wenye uwezo wa kufanya mabadiliko wanalalama.Sasa nani amsaidie mwenzake.

📌Wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira ambayo sio rafiki au chini ya kiwango ila badala ya kuaddress challenges faced by this civil servants.Mnaanza kuwananga hivi mtaendelea kutegemea miujiza mpaka lini.
 
📌wewe kama huna kichwa cha shule baki na certificate yako.Acha wenzako watafute GREEN PASTURE in there way.

📌Hutaki watu waumwe tengenezeni maroboti yafanye kazi 24/7/365days.

📌Kuna siku 14 za mwaka kwa kila mtumishi kwaajili ya mambo ya kijamii na dharura.

📌Ili watu wasirundikane hiyo mikoa yenye kuchangamka au mijini sambazeni maendeleo in equal distribution katika mikoa yote.Mngeweza hata kuwapa vipaumbele wafanyakazi wa migombani huko kwa vitu kama mikopo nafuu,nyumba na allowance za hapa na pale.Hampo inovative na bado mnalilia efficiency kwa wafanyakazi wenu.

📌Nchi hii kila mtu analalama hata wenye uwezo wa kufanya mabadiliko wanalalama.Sasa nani amsaidie mwenzake.

📌Wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira ambayo sio rafiki au chini ya kiwango ila badala ya kuaddress challenges faced by this civil servants.Mnaanza kuwananga hivi mtaendelea kutegemea miujiza mpaka lini.
Certificate ndio nn? Sina certificate ,sasa kwa akili yako ndogo hao wanaeonda kusoma hata maprofessor wako wana athari gani positive?
 
Kuna mizigo nchi hii kama hawa wanasiasa wetu..? Wabunge wa ndio ndio hata upumbavu wanaitikia ndio.
 
Hivi uliwahi kupata ajali ukajigonga kichwa chako!!??
Uliwahi kupata matatizo ya afya ya akili!!??
Ulizaliwa kichwa chako kikiwa sawa 100%!!??
mihemko na makasiriko ni kitu mbaya sana aise,

hivi inatokana na kukosa mawazo mapya na fikra mbadala sio ndio maana una gubu, right?

sasa si ukae kimya tu gentleman 🐒
 
Nafikiri next time akusanye mawazo mengi zaidi kwa private sector inayohuduwa atajua mengi zaidi...
 
AI imeshaingia anawaandaa kisaikolojia 😂
Mpaka serikali ifanye mabadiliko ya kutumia AI itachukua muda lazima kizazi flani kisiwepo kije kingine fikiria mtu kama Wasira bado yuko na hadithi za kupigania uhuru ni sehemu ya historia ya nchi yetu lakini sio itumike kama fimbo ya kuwachapia ambao hawakuwepo
 
Mtu anaingia saa tatu na nusu kazini,anazuga saa nne anaenda kupiga chai anakaa huko anarudi saa tano na nusu,anazuga saa sita na nusu ana kwenda lunch anarudi saa nane na nusu
Anazuga kazini saa tisa na nusu huyo kaondoka kwake
Ila yote anajuwa mshahara utaingiaaa....

Ova
Kazi zake anafanya nani?
 
Let me make this clear to everyone in this esteemed platform,

awamu ijayo ya uongozi wa serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu mpendwa na kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan & Dr Emanuel Nchimbi,

kuanzia kwenye baraza la mawaziri, taasisi, mashirika na mamlaka mbalimbali za umma hadi watendaji wa ngazi za vijiji na mitaa nchini,

hapatakua na kasumba ya kuhamishwa wizara, shirika, kijiji au mtaa, ukivurunda unapigwa chini na unakwenda nyumbani mazima,

hapatakua na mzaha wala kumuonea mtu aibu wala haya kwa uzembe au makosa yake kazini na kwa kuendekeza mazoe kwenye kazi za utendaji za kuwapelekea wananchi maendeleo.

there will be no excuse at all 🐒
Hili wazo.lilidokezwa na Rais ila najua wameliweka kiporo Ili kupisha uchaguzi.

Pia Kuna ule.utaratibu wa kupimiana Mafuta na kukopeshana magari kama wabunge nao uje kuzingatiwa.
 
Hayati MAGUFURI aliweza kurudisha nidhamu KAZINI MPAKA akaitwa majina ya OVYO Dicteta, roho mbaya...Kuna kipindi mpaka Kuna walio chelewa kazini vitu vyao vilichukuliwa na kupelekwa halmashauli ikabidi wavifuate huko😊

Kwa CCM hii ya mama simuoni huyo mwenye ubavu wa kuwa shurutisha Hawa wazembe wafanye kazi maana hata "MC GREGORY KWENYE THEORY X NA THEORY Y alipata kusema Kuna watu ni wavivu na hawataki kufanya kazi na pia kuna watu ni wachapakazi Sana.

Tuwafundishe watu wetu kua na moyo wa kupenda kazi hata Kama mazingira,malipo hakuna ni ku feel proud kufanya kazi kwa bidii hio ndio iwe spirit yetu..
U feel proud kufanya kazi ya Serikali huku wengine wananeemeka huko Bungeni? Kazi yangu binafsi ndio nitafanya Kwa ku feel proud.

Watu wanakimbilia Utumishi wa Umma Kwa sababu umejengwa katika namna ya kuwaonea watu wasio Watumishi wa Umma so inaatumika kama cover lakini ingekuwa mazingira ya uraiani ni wezeshi hakuna mtu angekaa huko kwenye Utumishi wa Umma.
 
CCM ni mzigo kwa taifa hili kwa miaka zaidi ya 40 wananchi wanaishi kwenye lindi la umasikini licha UTAJIRI wa rasilimali uliopo. Huduma za msingi kwa wananchi zimekuwa ndoto za alinacha, wanafaidika wajanja wachache.
Nani huyo wa kuwatoa.hiyi mizigo na kuwatajirisha? Kwa kutumia kanuni ipi? Watumishi wepi?
 
Back
Top Bottom