Simiyu: Baada ya kutenguliwa Ukuu wa Mkoa, Kafulila amshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa

Akina Kafulila tuliwategemea sana kuimarisha siasa za upinzani.
Hawa ndio wanaifanya CCM itawale milele.

Siasa kwao ni ajira na sio nia ya kuimarisha demokrasia.
Chadema hawana uwezo wa ku -retain compitent leaders, Mbowe anawatosha
 
Kiherehere kilizidi bora akapumzike.
Acha ufala kuwajibika unaita kiherehere naamini anakwenda kuwa mtu mkubwa sana ukizingatia nimtumishi mzuri nilitamani aletwe kigoma lakini naamini kunamlango umefunguka ndio waziri mkuu ajae andika hili utabiri wangu huo
 
Hapa nimeshindwa kumuelewa Samia. Unamrudisha Halima Dendego na kumpa ukuu wa mkoa halafu unamuondoa Kafulila. A very wrong move.

Ni kama vile hawezi yeye mwenyewe kama rais kufikiria kwa kina, najua kuwa Kafulila bado ni kijana na kichwani yupo vizuri atapewa cheo kingine labda kulingana na uwezo wake.

Lakini inaonyesha kuwa SSH ni kama vile hayupo karibu na ufanisi wa wasaidizi wake wa moja kwa moja. Ni mbaya sana JK kuwa na ushawishi wa kudumu katika awamu inayoongozwa na SSH.
 
Kwani na Mama nae hana Madudu? Acheni Unafiki na Upumbavu. Ukweli ni kwamba Safu na Vimelea vyote vya Pro Late President Dk. Magufuli ndiyo Vinaondolewa.
Ni kweli, mama anaondoa wale wote wa Magufuli hata kama hawana kosa, kosa ni kuwa "wa Magufuli "!
 
Kwa dendegu usimlaumu samia, mlaumu Mr tabasamu. Hili mbona liko wazi tangu akiwa mkuu wa wilaya Tanga, na kupelekwa kuwa mkuu wa mkoa kusini. Shujaa aliyajua haya akampiga chini.
 
Sio vibaya kufanya mabadiliko ila tatizo lipo kwenye kurejesha majina yale yale.

Hivi nchi hii haina wasomi??

Au majina hayo hayo ndio watanzania waliokwenda shule pekee??

Au ndio wazalendo kuliko wengine??

Kama Taifa tunahitaji mawazo mapya jamani.
 
Aende akafanye kazi zingine! Ye Nan ktk ukuu wa mkoa? Waliondoka akina makonda sembuse yeye. Kwanza yeye alihongwa cheo na Jose kwa lengo la kuua upinzani.
 
Aende akafanye kazi zingine! Ye Nan ktk ukuu wa mkoa? Waliondoka akina makonda sembuse yeye. Kwanza yeye alihongwa cheo na Jose kwa lengo la kuua upinzani. Na ajiangalie Sana atakuja apotee mazima ktk siasa. Up! Down kwake zimekua nyingi Sana! Nccr, chadema, ccm, ubunge, ukatibu tawala, ukuu wa Mkoa!hajiulizi tuu nn tatizo kwake?
 
Aende kigoma Sasa akaliwe funza za miguu
 
Huyu ndugu alikuwa sterling wa ile movie ya escrow alicheza vizuri sana namkubali.
 
Aende akajiajiri nakutumia mashine ya EFD.
Maana wakiwa kwenye nafasi zao wanaona kujiajiri simple sana kama kujamba.
 
Kiherehere kilizidi bora akapumzike.
CHADEMA HAMPENDI SANA WATU WANAOWACHALLANGE KISIASA,MNATAKA MARAC MABUBU ILI MPENYEZE AGENDA ZENU, KAFULILA ALIWACHARAZA SANA KWA HOJA ZAKE NA UTENDAJI KAZI WAKE.
 
Ali Hapi bado na makofi yanamuhusu bwa mdg yule alikua mnafiki sana

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Katiba mpya ingewapa wakuu wa mikoa au magavana "job security" waweze kutekeleza kwa utulivu mipango ya muda mrefu ya wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…