mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,759
- 1,061
Hakuna kitu kafanya huyu zaidi ya kuwatisha makandarasiKiherehere kilizidi bora akapumzike.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kitu kafanya huyu zaidi ya kuwatisha makandarasiKiherehere kilizidi bora akapumzike.
Kuwatisha makandarasi ni jambo baya?Hakuna kitu kafanya huyu zaidi ya kuwatisha makandarasi
Kafulila hata mimi kaniuma aiseeee
Kwani kafariki?Kafulila hata mimi kaniuma aiseeee
amenMungu wa Mbinguni akuongoze Kafulila, Utakuwa mkuu wakati wote mbele za watu, Umefanyika baraka kwa watu wengi,
Kiherehere kilizidi bora akapumzike.
Hivi vyeo vya kisiasa ni vyeo vya ovyo ovyo sana, kwa mtu mwenye akili sawasawa awezi kukubali teuzi za kisiasa ni bora kubaki na kazi yako ya kitaaluma, Vyeo vya kutegemea aliyekuteua ameamkaje siku iyo wakati huo wapambe wengine wanakuvizia ukosee wakulipue na wao wafikiriwe kwenye teuzi ni kazi zisizokuwa na uhakika wa kesho yakoKafulila amshukuru Rais Samia, awaaga wananchi wa Simiyu
![]()
- Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.
Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.
Alhamisi Julai 28, 2022, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa ambapo amewateua wapya tisa, amewabadilisha vituo baadhi yao na wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi.
Katika mabadiliko hayo, wakuu wa mikoa tisa wameachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine, miongoni mwa walioachwa ni pamoja na Kafulila.
Wengine ni Ally Hapi (Mara), Robert Gabriel (Mwanza), Steven Kagaigai (Kilimanjaro), Charles Mbuge (Kagera), Wilbert Ibuge (Ruvuma), Marco Gaguti (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Rukwa), Binilith Mahenge (Singida).
Akizungumza na Mwananchi, Kafulila amemshukuru Rais Samia na kuwaaga wananchi wa Simiyu huku akiwataka wampe ushirikiano mkuu wa mkoa mpya, Dk Yahya Nawanda na kuendeleza walipokuwa wamefikia.
“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla.
“Pili, ni kuwatakia heri wana Simiyu wote na kuwaomba waendeleze yote tuliyofanikisha pamoja na mengine zaidi ambayo hatukuweza kufanya ambayo watafanya na RC mpya. Binafsi nitaendelea kuitumikia nchi yetu kwa nguvu ile ile kama raia mwema.
“Natoa wito kwa wana Simiyu Kushirikiana RC mpya na zaidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kazi kubwa anayoifanya ya kujenga Mkoa wetu wa Simiyu hasa kwa mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya Mkoa,” amesema Kafulila.
Amewataka wananchi wa Simiyu kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kufanikisha maono ya kujenga Taifa mpya na kujenga mkoa wa Simiyu hasa katika mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya mkoa.
Rais Samia ateua wakuu wa mikoa wapya, tisa watemwa
“Waendelee kumuunga mkono Rais wetu kufanikisha maono makubwa ya kujenga Taifa moja kubwa kiuchumi na hivyo kisiasa ma kujenga jamii kubwa ambayo kila mmoja anayo fursa ya kushiriki ujenzi bila kujali tofauti hizo,” amesema Kafulila
“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla
Watachagiwaje wakati hamuwataki?Ni muda sasa umefika Wakuu wa mikoa wawe chaguo la Wananchi na siyo Rais..... Katiba mpya sasa.
Ameen,Mungu wa Mbinguni akuongoze Kafulila, Utakuwa mkuu wakati wote mbele za watu, Umefanyika baraka kwa watu wengi,
Inawezekana maana Rais kasema kuna wengine atawatumia maeneo tofauti..naskia ataletwa wizarani.
Umesikia vibaya.naskia ataletwa wizarani.
CHADEMA mnasikia raha sana,Ameshindwa kufanya mabadiliko alijua kuongoza ni sawa na kupiga kelele mke kamwacha na pesa aliyohongwa itakwisha atabaki kuwa asieaminika hata kidogo na hawezi kuchaguliwa Tena kwenye nafasi za kuchaguliwa
Upinzani gani hao wanaofurahi.mfanye maujinga yenu uko alafu msingizie wengine.mtaangaika sana hadi jua lizame.Chadema mnafanya sherehe,
Note, Rais wangu Samia unapomwondoa mtu na wanaofurahia ni Upinzani, Si afya kwa Chama chetu
Kiukweli Chadema mmefurahi sana huyu Kafulila kutenguliwaUpinzani gani hao wanaofurahi.mfanye maujinga yenu uko alafu msingizie wengine.mtaangaika sana hadi jua lizame.
Hayo madudu yameisha?Rais ana taharifa nyingi za siri kuhusu wateuliwa wake, mkuambiwa madudu ya kafulila mtazimia