Simiyu: Baada ya kutenguliwa Ukuu wa Mkoa, Kafulila amshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa

Simiyu: Baada ya kutenguliwa Ukuu wa Mkoa, Kafulila amshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa

Kafulila amshukuru Rais Samia, awaaga wananchi wa Simiyu​

kafulilapic

  • Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Alhamisi Julai 28, 2022, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa ambapo amewateua wapya tisa, amewabadilisha vituo baadhi yao na wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi.

Katika mabadiliko hayo, wakuu wa mikoa tisa wameachwa na nafasi zao kuchukuliwa na wengine, miongoni mwa walioachwa ni pamoja na Kafulila.

Wengine ni Ally Hapi (Mara), Robert Gabriel (Mwanza), Steven Kagaigai (Kilimanjaro), Charles Mbuge (Kagera), Wilbert Ibuge (Ruvuma), Marco Gaguti (Mtwara), Joseph Mkirikiti (Rukwa), Binilith Mahenge (Singida).

Akizungumza na Mwananchi, Kafulila amemshukuru Rais Samia na kuwaaga wananchi wa Simiyu huku akiwataka wampe ushirikiano mkuu wa mkoa mpya, Dk Yahya Nawanda na kuendeleza walipokuwa wamefikia.

“Kwanza nitoe shukran za kipekee kwa Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini kumsaidia katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ni heshima kubwa kwangu ambayo sikuwahi kuipata hapo kabla.

“Pili, ni kuwatakia heri wana Simiyu wote na kuwaomba waendeleze yote tuliyofanikisha pamoja na mengine zaidi ambayo hatukuweza kufanya ambayo watafanya na RC mpya. Binafsi nitaendelea kuitumikia nchi yetu kwa nguvu ile ile kama raia mwema.

“Natoa wito kwa wana Simiyu Kushirikiana RC mpya na zaidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kazi kubwa anayoifanya ya kujenga Mkoa wetu wa Simiyu hasa kwa mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya Mkoa,” amesema Kafulila.

Amewataka wananchi wa Simiyu kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kufanikisha maono ya kujenga Taifa mpya na kujenga mkoa wa Simiyu hasa katika mapinduzi ya zao la pamba na miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa kila kona ya mkoa.

Rais Samia ateua wakuu wa mikoa wapya, tisa watemwa

“Waendelee kumuunga mkono Rais wetu kufanikisha maono makubwa ya kujenga Taifa moja kubwa kiuchumi na hivyo kisiasa ma kujenga jamii kubwa ambayo kila mmoja anayo fursa ya kushiriki ujenzi bila kujali tofauti hizo,” amesema Kafulila
Hivi vyeo vya kisiasa ni vyeo vya ovyo ovyo sana, kwa mtu mwenye akili sawasawa awezi kukubali teuzi za kisiasa ni bora kubaki na kazi yako ya kitaaluma, Vyeo vya kutegemea aliyekuteua ameamkaje siku iyo wakati huo wapambe wengine wanakuvizia ukosee wakulipue na wao wafikiriwe kwenye teuzi ni kazi zisizokuwa na uhakika wa kesho yako
 
Unazani angesema nini zaidi ya kushukuru tu!
 
Hilo ndilo swali nauliza: Hapi kafukuzwa Mara na pia Chegeni kafukuzwa Mara all in the space of one week? Au jambo gani limetokea?
 
Ameshindwa kufanya mabadiliko alijua kuongoza ni sawa na kupiga kelele mke kamwacha na pesa aliyohongwa itakwisha atabaki kuwa asieaminika hata kidogo na hawezi kuchaguliwa Tena kwenye nafasi za kuchaguliwa
 
Ameshindwa kufanya mabadiliko alijua kuongoza ni sawa na kupiga kelele mke kamwacha na pesa aliyohongwa itakwisha atabaki kuwa asieaminika hata kidogo na hawezi kuchaguliwa Tena kwenye nafasi za kuchaguliwa
CHADEMA mnasikia raha sana,
 
Chadema mnafanya sherehe,

Note, Rais wangu Samia unapomwondoa mtu na wanaofurahia ni Upinzani, Si afya kwa Chama chetu
Upinzani gani hao wanaofurahi.mfanye maujinga yenu uko alafu msingizie wengine.mtaangaika sana hadi jua lizame.
 
Back
Top Bottom