SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

VIjana wawe makini na mgroup ya Watsapp

===
Bariadi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu

Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu 0764996612 isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.

CHANZO: Mwananchi
Huyu kada kabla ya kufungwa ilipaswa kwanza ahojiwe kikamilifu kama yupo nyuma ya Mwigulu na Makamba wenye mpango wa kumezea mate kiti cha rais aliyewateua kwenye nyadhifa za uwaziri. Namshauri mama Samia awafute kazi hawa jamaa na hata kuwafukuza uanachama wa CCM kabla hawajamletea shida.

Mwigulu na Makamba ni wazoefu wa siasa za CCM na wamekuwepo kwenye baraza la mawaziri kwa miaka 10 sasa. Hao sio wajinga wa kusema wamezee kiti cha uRais mwaka 2025. Mwana-CCM yoyote anafahamu kuwa kumezea kiti cha uraisi 2025 kupitia CCM ni kujiua kisiasa kama alivyofanya Membe.

Hao wanajiandaa kwa ajili ya 2030.
 
Back
Top Bottom