SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

Levinus Kidanabi,
Amehukumiwa kwenda jela miaka saba, Pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni kumi na tano za kitanzania. Huko Bariadi.
Kwa kosa la kumkosoa rais Samia, kupitia "Facebook."

Mambo kama haya kipindi cha "JPM" ndio tulizowea kuwasikia wapinzani na wanaharati nchini wakipiga kelele kupitia Media za Kimataifa.

Pia wakiandika nyaraka kwa Wanadiplomasia wa Balozi mbalimbali zilizoko nchini ili kuomba nchi zao zichukuwe hatua kwa serikali.

Lakini mpaka sasa,tangu huyu mwana CCM ametiwa hatiani, kisa tu, katoa maoni kinzani kwa kiongozi wa CCM na Rais wa nchi.

Sio... Zitto, Mnyika, Abdul Nondo, Lema, Lissu, Maria,
LHRC na wengineo wooote wanajitanabahisha kupigania na kuendesha harakati za vitendo vinavyokiuka haki za uhuru wa kidemokrasia nchini.

Wako kimya as if hawahasikia kitu... Au ndimi na vinywa vimejaa asali?
... ila yajayo yanatafakarisha zaidi, na huenda yakatufukarisha zaidi badala ya kutufurahisha zaidi....

Alamsikhi!
IMG-20221021-WA0006.jpg
 
Na wewe Ulikuwa jela nini ? wewe hujaona humu maandishi ya jambo hilo ?
 
Wana CCM wana IQ kubwa hawawezi,kamwe hawawezi kumtusi Rais mama yetu mpendwa.Hilo litakuwa jambazi la kile chama kisichojitambua na hilo shati lililovaa ni la wizi kutoka ofisi za chama tawala.
Yaani mwanaccm afungwe na ccm halafu unataka wapinzani wapambane?
 
Levinus Kidanabi,
Amehukumiwa kwenda jela miaka saba,Pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni kumi na tano za kitanzania.huko Bariadi.
Kwa kosa la kumkosoa rais Samia,kupitia "Facebook."

Mambo kama haya kipindi cha "JPM" ndio tulizowea kuwasikia wapinzani na wanaharati nvhini wakipiga kelele kupitia Media za Kimataifa.

Pia wakiandika nyaraka kwa Wanadiplomasia wa Balozi mbalimbali zilizoko nchini.ili kuomba nchi zao zichukuwe hatua kwa serikali.

Lakini mpaka sasa,tangu huyu mwana CCM ametiwa hatiani,kisa tu,katoa maoni kinzani kwa kiongozi wa CCM na Rais wa nchi.

Sio... Zitto,Mnyika,Abdul Nondo,Lema,Lissu,Maria,
LHRC na wengineo wooote wanajitanabahisha kupigania na kuendesha harakati za vitendo vinavyokiuka haki za uhuru wa kidemokrasia nchini.

Wako kimya as if hawahasikia kitu.....Au ndimi na vinywa vimejaa asali?
...ila yajayo yanatafakarisha zaidi, na huenda yakatufukarisha zaidi badala ya kutufurahisha zaidi....

Alamsikhi!View attachment 2395023
Hao wanaharakati mliwatukana sana.

Muokoeni sabaya kwanza
 
Tambua tu Ya Kwamba Wote Wapinzani na hao Wenyewe Wana Lamba Asali...!

Sasa We hujui Kuwa Asali ni Tamu...
Asali pia Ina Chemikali inayofanya Macho 'kutoona kwa Muda' yaani transient visual loss na 'kutosikia kwa Muda' yaani transient hearing loss...!

Acha kbs asikwambie Mtu Asali ni Tamu....! Hiyo ndo sbb ya huu Ukimya.
 
Hujaelewa uzito wa hoja yangu ulipolalia mkuu!

Mimi ninawauliza kama ilikuwa chuki binafsi,sababu yule aliwatenga na ulaji,na huyu anawagawia kidogo kidogo asali toka kwenye Buyu kubwa?
Hayo utajua mwenyewe
 
Wana CCM bana, yaani pamoja na kuwabagaza, kuwasema vibaya, kuzuia haki zao za kisiasa, kuwatesa, kuwabambikia kesi za uchochezi na za uongo, kuwasweka mahabusu na kuwafunga, kuhujumu mali zao, kuwatia vilema vya maisha, wengine kuwauwa kabisa, kuzalisha wakimbizi wa kisiasa, na pia hata kuwadhulumu katika chaguzi za 2019 na 2020, leo hii bado mnataka waje wawasemee na kuwapigania haki zenu za kikatiba!?

Wakati mambo kama hayo yakiwatokea wapinzani, mlikua mnakenua meno yenu na kutoa lugha za dhihaka, na wala kutokujali kabisa. Haya sasa jini mlilofuga nyinyi wenyewe kwa kulifungia kwenye chupa, sasa linatoka na kuanza kutamani damu zenu.

Sasa kila mtu na apambane kwenye mechi zake, na kwenye ligi yake yeye mwenyewe. Hiyo lia lia yenu haitusaidii kitu chochote kile, zaidi kusikia kelele za mfa maji. Nafikiri kwa sasa mtaanza kufahamu umuhimu wa katiba mpya ambayo itaweka uhuru, haki na uwazi katika mihimili ya dola katika kufanya maamuzi yake.
 
Levinus Kidanabi,
Amehukumiwa kwenda jela miaka saba, Pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni kumi na tano za kitanzania. Huko Bariadi.
Kwa kosa la kumkosoa rais Samia, kupitia "Facebook."

Mambo kama haya kipindi cha "JPM" ndio tulizowea kuwasikia wapinzani na wanaharati nchini wakipiga kelele kupitia Media za Kimataifa.

Pia wakiandika nyaraka kwa Wanadiplomasia wa Balozi mbalimbali zilizoko nchini ili kuomba nchi zao zichukuwe hatua kwa serikali.

Lakini mpaka sasa,tangu huyu mwana CCM ametiwa hatiani, kisa tu, katoa maoni kinzani kwa kiongozi wa CCM na Rais wa nchi.

Sio... Zitto, Mnyika, Abdul Nondo, Lema, Lissu, Maria,
LHRC na wengineo wooote wanajitanabahisha kupigania na kuendesha harakati za vitendo vinavyokiuka haki za uhuru wa kidemokrasia nchini.

Wako kimya as if hawahasikia kitu... Au ndimi na vinywa vimejaa asali?
... ila yajayo yanatafakarisha zaidi, na huenda yakatufukarisha zaidi badala ya kutufurahisha zaidi....

Alamsikhi!View attachment 2395023
Kwanza we ni mnafiki mpk chenji inabaki. Mmekuwa na siasa za hovyo. Kilichomfunga ni sheria. Hata ww ukivunja sheria utafungwa na sheria siyo unafungwa na mtu. Mtii sheria. Wenye akili tumekuelewa unataka kujenga hoja gani ya kipuuzi. Hilo genge lenu litakufa kifo cha mende hamtafanikiwa chochote
 
Sidhani kama Public Figures nao wanahitaji Fake I'ID's...ila kwa Tanzania lolote linawezekana mkuu!
Voicer! Voicer!
Nimekuita mara 2 Kwa sababu Mimi ni miongoni mwa wafuatiliaji wa maandiko ya Kisiasa na kimaono humu JF na nimekuwa nikisoma maandiko yako mengi kuhusu upinzani na michango yako katika hoja zinazopongeza Wapinzani. Nilichokigundua ni kwamba unajua umuhimu wa upinzani ila huwa unajitoa ufahamu labda Kwa maslahi binafsi maana watu wengi maslahi binafsi hutangulia Kila kitu. Kuwa kwako CCM hakupaswi kukugeuza kuwa na roho ya kuunga mkono maumivu Kwa Wenye haki hata kama hawako upande wako. Nimachokiona kwako na wenzio mliokuwa wapiga Debe wa Sera za Magufuli na kuendeleza uhasama na kundi la Samia ndo maana unadhani waliopiga kelele Kwa matendo ya Magufuli Leo hawapigi kelele Kwa kiwango kilekile Kwa Samia. Wewe Hilo linakuumiza Sana lakini hukumbuki na wewe Una nafasi hiyo ya kupiga kelele kupinga dhuluma na uonezi.
Huyu kijana wa Bariadi kweli kaonewa, lakini watu wamepiga kelele tena wengine Kwa verified IDs kama alivyofanya Wakili Jebra Kambole. Kama maoni ya kusema "Hata Samia hili limemshinda" ni kumkashifu basi kumbe Samia ana uwezo wa Kimungu wa kutoshandwa chochote.
Ni wajibu wako wewe kama mwananchi bila kujali itikadi yako kukemea uovu na kuhimiza haki. Lakini wenzetu mmegeuza sitahiki ya haki iwe upande wenu tu, Kwa walio kinyume chenu kimtazamo haki Yao ni Mateso, Badilikeni Sasa au msubiri wakati uwabadilishe.
 
Huyo ni Sukuma Gang, wanamtakana Samia matusi ya nguoni halafu waachwe?

Hawa si ndio walikuwa wakishangilia Tundu Lissu kupigwa risasi
Utamtetea shetani akivuna alichopanda?
 
Back
Top Bottom