SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

VIjana wawe makini na mgroup ya Watsapp

===
Bariadi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu

Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu 0764996612 isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibaki kutoka mamlaka husika.

"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.

CHANZO: Mwananchi
Kamkashifu kivipi mbona hamuwezi wazi, akipata wakili mzuri anatoka mapema asubuhi
 
Wasukuma hawajawahi heshimu mwanamke..ni dharau kubwa sana mwanamke kuongoza.

Obhonahe nkoko nhima engahelaga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ila mijizi na mifisadi serikalini hutasikia ikihukumiwa.[emoji34]
 
Sasa hapo ni miaka 7 au mi 3? Na ukijumlisha msamaha wa 1/3 ina maanisha atakaa ndani solid 2 yrs.

Hao mwananchi wame edit wakamvalisha kijani ili kuwapumbaza watu waogope kwamba hadi ccm wanashughulikiwa je sisi upande wa pili si itakuwa balaa.
 
Ila akienda HC for Appeal Dogo amachomoka.

Mahakimu wengi Wa lower court Judgment zao haziko solid ni mihemuko.

Nina Uhakika Hyo Judgement Haina Hata Case citation Hata Moja
 
Siku hizi wewe ufanye tu kosa lolote lile dhidi ya mwanamke hata likiwa ni la kawaida tu, kisha upelekwe mahakamani ukutane na hakimu mwanamke..... baba/ kaka utajuta..., nasema utajuuuuta kuifahamu hii nchi au hii dunia!!
 
Naona Sukuma Gang wameanza kunyooshwa.

Huu ni mtifuano wa ndani ya CCM ndani ya magroup yao.

Sisi tuombe lile Group la AfroShirazi lishinde hao wanahuruma kidogo kwetu Wapinzani.
 
VIjana wawe makini na mgroup ya Watsapp

===
Bariadi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu

Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu 0764996612 isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.

CHANZO: Mwananchi
Hukumu imekaa kishabiki zaidi ingwa kashfa no mbaya lakini tungeambiwa alisema Nini ili tujiridhishe
 
:Lisu : Mama amefungua nchi sasa tuko huru.

Zito: Asante hali ya siasa ni nzuri mnoooooo, tuko huru kabisa kukosoa.

Wakati tunaonya kwamba mnawashangilia wachumia tumbo mlikuwa mnapinga na kutupuuza, haya jioneeni sasa.
 
wenye midomo ya kuharisha kaeni chonjo, vinginevyo mtaozea jela, jela pasikie tu bora ulale nje.
 
Screenshot_20221021-170649.png

Screenshot_20221021-170612.png
 
Tayari jamaa kadandia mtumbwi wa vibwengo tuheshimu mamlaka na viongozi kwa ujumla jamani.
 
Back
Top Bottom