Simiyu: Mkuu wa Wilaya ya Busega: Nimepigwa mawe wakati wa Maandamano, tumewakamata Watu 108

Simiyu: Mkuu wa Wilaya ya Busega: Nimepigwa mawe wakati wa Maandamano, tumewakamata Watu 108

Maandamano fani za watu,kinyume chenu hupigwa na polisi au wajeshi

Ninyi ,mnapigwa na raia!!!!

Wangekukamati wakuyomboloboshi kabisa
 
Huyu mama wa ajabu sana.

Yaani anajisifia kukamata watu 108?
 
Akizungumzia maandamano yaliyotokea Lamadi, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Faiza Salim amesema athari zilizotokea baadhi ya Viongozi kushambuliwa kwa kupigwa mawe akiwemo yeye (Faiza).

Amesema kwa muda wa miezi minne aliyokuwa katika nafasi hiyo hajapata taarifa ya Watoto kupotea. Amesema “Mabomu ya machozi yamepigwa kwa kuwa walizuia magari yote, wameharibu Miundombinu, maduka... Mamlaka hatuwezi kukubali hilo.”

Kuhusu taarifa za Waandamanaji kupoteza maisha, amesema “Sijapokea taarifa kama kuna mtu amekufa, inawezekana yapo majeraha madogo, baadaye tukimaliza oparesheni tutatoa taarifa kamili, mpaka sasa tumewakamata Wtu 108 na tunawapeleka Mahakamani.”

Pia Soma ~ Simiyu: Wananchi wavamia Kituo cha Polisi wakidai kuna matukio mengi ya Watoto kupotea
Typical colonial mindset..
1) mamlaka hatuwezi kukubali...(mpo kwa niaba ya wananchi mna jukumu la kuwasikiliza)

2) tumewakamata 108...(anasifia idadi kubwa ya wananchi waliokamatwa kama vile ni mafanikio makubwa, kumweka ndani mwananchi sio mafanikio..

3) sijapata taarifa ya kupotea...(unasubiri kuletewa kwa nini usishuke chini waliko wananchi ukapate taarifa mwenyewe)

4) sijaskia vifo..(again yeye ndio mwenye vyombo kwanini asitoe taarifa iliyojitosheleza kuwa hakuna vifo full stop ama vipo period)
 
Kama hakua na taarifa..ina maana huyo mtu ni mvivu hafanyi kazi yake. Anastahili kutumbuliwa tu
 
Back
Top Bottom