Simiyu: Mwili wa mtu wakutwa ukielea kwenye maji, siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM aliposema 'Mkoa wa Simiyu hali si shwari'

Simiyu: Mwili wa mtu wakutwa ukielea kwenye maji, siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM aliposema 'Mkoa wa Simiyu hali si shwari'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
photo_2023-04-02_14-54-10.jpg

Machi 25, 2023 akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Bi. Shemsa Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu alidai kuwa kuna watu wanapotea pasipo kujulikana wanapoelekea ndani ya Mkoa huo.

Pia akabainisha kuwa kuna matukio ya wizi yameongezeka hasa maeneo ya nyumbani wakati wa usiku na kuwa kuna miili ya watu imeokotwa kwenye ‘mifuko ya Rambo’.

Licha ya kusema hivyo na mamlaka kutotoa tamko lolote, leo Jumapili Aprili 2, 2023 mwili wa mtu ambaye bado hajatambulika umekutwa ukielea ndani ya maji katika Msitu wa Masunzu, Mtaa wa Mwaswale, Kata ya Sima, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
photo_2023-04-02_14-54-03.jpg

photo_2023-04-02_14-54-45.jpg

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, mtoto ambaye alikuwa na nguruwe, ndiye aliyegundua tukio hilo na kuanza kupiga kelele.

"Baada ya kelele za mtoto huyo, kuna watu walikuwa kwenye ibada ya jumuiya asubuhi kwenye nyumba moja jirani na tukio, ndipo wakatoka na kwenda kushuhudia.

"Walipofikia kwenye tukio, kila mmoja alishangaa baada ya kukuta mwili ukiwa ndani ya maji, wakapigwa simu kwa Mwenyekiti wa mtaa pamoja na Mtendaji wa Mtaa," anasema Juliana Sonza.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Emmanuel Paul amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi alipiga simu Polisi na kuja kuupoa mwili huo.

"Nimemtambua huyo mtu kwa jina la Boniphace ni mkazi wa huu mtaa, baada ya kuopolewa nimeona kama amenyongwa, lakini tunasubiria Jeshi la Polisi watatupa na majibu baada ya uchunguzi wao," amesema Emmanuel.

Hata hivyo mwili huo umepelekwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

=========

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Blasius Chatanda alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema “Sina taarifa ya tukio hilo, watu wangu hawajanipa hizo taarifa labda nifuatilie.”

Pia Soma:
Mwenyekiti wa CCM Mkoa: Miili ya Watu inaokotwa kwenye Mifuko ya Rambo, Simiyu si salama
 
Enzi za JPM wangesema ni BAVICHA ameuwawa na JPM

USSR
 
Back
Top Bottom