SIMIYU: Waliouza kaburi la Bi Hapi Lupigila kwa TZS 30M wakubali TZS 500K

SIMIYU: Waliouza kaburi la Bi Hapi Lupigila kwa TZS 30M wakubali TZS 500K

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466

HATIMAYE KABURI KATIKATI YA BARABARA BARIADI LAONDOLEWA.. FAMILIA YARIDHIA YAKUBALI YAISHE​

Zoezi la kuhamisha kaburi likiendelea
===
WIKI Moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila kuagiza kuondolowa kwa Kaburi lililokuwa katikati ya Barabara ya Nkindwabiye-Halawa, Familia ya Saguda Madako imetekeleza agizo la kuondoa kaburi hilo huku wakikubali kulipwa fidia ya shilingi laki tano na Serikali.

Ikumbukwe kuwa familia hiyo iligoma kuondoa kaburi la Habi Lupigila, kwa madai kuwa hadi walipwe kiasi cha shilingi milioni 30 na kwamba kaburi hilo lilikuwepo eneo hilo tangu mwaka 1975.

Wakizungumza na malunde 1 blog jana mara baada ya kuondoa kaburi hilo baadhi ya ndugu wa marehemu (wana Ukoo) wamesema kaburi hili lilikuwa limejengwa eneo hilo ambalo hapakuwepo na barabara bali ilikuwa sehemu ya barabara.

‘’Tulikuwa tumejenga hapa, tukahama kwenda Matongo, wakati tunajenga hapakuwa na barabara bali lilikuwepo zizi…baadae lilipita barabara, changamoto ni hii ya kuhamisha kwenda kuanza mazishi upya’’’ anasema Susan Mayenga na kuongeza.

‘’Serikali tunaomba ibadilishe sheria kwa ajili ya kulipa fidia, hili tatizo siyo kwetu tu linaweza kutokea kwa wengine, serikali ibadilishe utaratibu wa fidia….kuna gharama za mazishi, usafiri kwa sababu ni msiba mwingine’’ anasema.

Saguda Madako Mayenga anasema mama yake mzazi alifariki tangu mwaka 1975 na kuzikwa katika kijiji cha Nkindwabiye, ambapo kwa sasa limepita barabara linalotoka Byuna-Nkindwabiye hadi Halawa.

Anasema fidia ya shilingi laki tano ambayo wamepatiwa na serikali haitoshi kwa sababu wanahamisha kaburi na kwenda kufanya mazishi upya huku akiiomba kurekebisha sheria ya fidia ili iweze kukidhi mahitaji.

Anaeleza kuwa familia hiyo ilikuwa haijagoma kuhamisha kaburi hilo, bali barabara ilikuwa imelifuata kaburi kwa sababu miaka ya nyuma hapakuwepo na barabara katika eneo hilo.

‘’Tuliiomba serikali ituwezeshe kutoa kaburi, lakini hatukuweza kuelewana, sasa tumekubali tuhamishe, japokuwa laki tano haitoshi kwa sababu tutanunua jeneza, usafiri pamoja na chakula’’ anasema Madako akiongea na malunde 1 blog.

Ng’wamba Susani, mtoto wa Marehemu (Habi Lupigila) anasema serikali imemkumbushia kifo cha mama yake mzazi wakati huo fedha waliyolipwa kwa ajili ya fidia haitoshelezi.

Naye John Ndulu Lupigila ambaye ni msimamizi wa wana Ukoo anasema tukio hilo ni sehemu ya maumivu kwa wana ukoo sababu marehemu alifariki tangu mwaka 1975.

Anasema wana ukoo wamechangishana fedha ili kuweza kufidia gharama za kuhamisha kaburi kutokana na fedha walizolipwa na serikali kutokidhi mahitaji ya zoezi hilo.

Goromondo Isamula mkazi wa Nkindwabiye anasema marehemu alikuwa ameolewa na Madako Amva, alifariki muda mrefu na kaburi hilo lilikuwa kwenye zizi ambapo familia ilijengelea baada ya barabara kupita.

Anaongeza kuwa kaburi hilo lilikuwa njiani, lilikuwa hatari kwa sababu magari yangeweza kugongana na wao kama wananchi wamefurahi kaburi hilo kuondolewa njia sababu barabara imeonekana.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nkindwabiye Safari Ng’habi Himbo akizungumza na malunde 1 blog ameishukuru serikali pamoja na wananchi kwa mwitiko wa kushiriki zoezi la kuhamisha kaburi lililokuwa kikwazo katikati ya barabara hiyo.

‘’Niwashukuru ndugu kwa kukubwali wito wa serikali kwa kuondoa kaburi hili lililokuwa adha kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na magari, ilikuwa ni shida magari yalikuwa yanasababisha ajali katika eneo hili’’ anasema Safari.
Anaeleza kuwa aliishawishi serikali pamoja na ndugu ili waweze kukubaliana na hatimaye kulitoa kaburi, ‘’nashukuru Serikali upande wa TARURA, wananchi sambamba na ndugu tumekubaliana kutoa mwili kuoka hapa Nkindwabiye kwenda kata ya Matongo’’. anasema.

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu

the dead body since 1975, this is another sign of primitive society, since 1975 what is in there? spending the production time and manpower with all those people around there instead of one or two people take the left over and send anywhere.
 
Boss huwajui wabongo? Wewe hata ukianguka na baiskeli yako lazima wajae kukuzingira.
 
Wamekuta jeneza jipya tuu au
Jeneza jipya limenunuliwa, familia imesema isaidiwe na raia maana laki tano haitoshi kununua jeneza na chakula.

Hakuna tena maeneo ya kuzikia japo na kwenye hayo maeneo nayo miili inahamishwa ie vingunguti.

Nowhere kwenye maisha ya milele, si duniani wala kaburini,

Poleni wana familia.
 
the dead body since 1975, this is another sign of primitive society, since 1975 what is in there? spending the production time and manpower with all those people around there instead of one or two people take the left over and send anywhere.
Utakuwa mjibga pamoja na lugha yako ya kukodi hii. Fuvu la binadamu liligunduliwa liko makumbusho hadi leo watu waliangalia kwa pesa. Huyo hata ukoo wake haujulikani sembuse huyu.
Juzi ufaransa imerudisha jino la LUMUMBA wa Congo kama sehemu ya suluhu walikuwa na jino miaka yote.
Hilo eneo hapakuwa na barabara kaburi likuwepo . Je wangechimbua waiache mifupa nje isihamishwe?
Nyie ndio wasomi tunawategemea sisi la 7B lkn Uprof wenu na u Dr ni takataka kabisa ndio maana tunafeli kwenye mikataba mnapokutana na wenye lugha mliyoazima kujadili[emoji706]

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Fidia gani sasa wakati mtu alishakufa kwamba wakae msimba mwingine wa million30. Mfu ni mfuu tuu
 
Utakuwa mjibga pamoja na lugha yako ya kukodi hii. Fuvu la binadamu liligunduliwa liko makumbusho hadi leo watu waliangalia kwa pesa. Huyo hata ukoo wake haujulikani sembuse huyu.
Juzi ufaransa imerudisha jino la LUMUMBA wa Congo kama sehemu ya suluhu walikuwa na jino miaka yote.
Hilo eneo hapakuwa na barabara kaburi likuwepo . Je wangechimbua waiache mifupa nje isihamishwe?
Nyie ndio wasomi tunawategemea sisi la 7B lkn Uprof wenu na u Dr ni takataka kabisa ndio maana tunafeli kwenye mikataba mnapokutana na wenye lugha mliyoazima kujadili[emoji706]

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
ni ubelgiji sio ufaransa mkuu...
 
Back
Top Bottom