Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijuwi anapanga kufa lini
RIP watz wenzetu.Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.
--
Rais Samia atoa salamu za Rambirambi
''View attachment 2076839
====
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.
Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo
“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza
“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.
Chanzo: Mwananchi
======
UPDATES;
=====
Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni
1. Husna Mlanzi wa ITV
2. Johari Shani wa Uhuru Digital
3. Antony Chuwa wa Habari leo Digital
4. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza
5.Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe
6. Paul Silanga Dereva wao
Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.
Majeruhi ni:
1. Vanny Charles wa Icon. TV
2. Tunu Heman -Mwandishi wa habari wa kujitegemea
Wamelazwa Hospitali ya Bugando Mwanza
=====
RC KAFULILA ATOA SALAMU ZA RAIS SAMIA KUFUATIA AJALI MBAYA YA GARI MKOANI SIMIYU
MKUU wa Mkoa Simiyu, David Kafulila amewapa pole wakazi wa wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kufuatia ajali mbaya ya gari iliyochukua maisha ya watu14.
" Huu ni msiba mkubwa kwenye historia ya wilaya na mkoa wetu. Kupoteza watu14 kwa ajali ni msiba mkubwa kitaifa. Nimewasiliana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amepokea taarifa ya ajali hii kwa masikitiko makubwa na amenituma kufikisha kwenu salamu za pole, na kwamba yupo nasi katika majonzi haya".
" Ni ajali mbaya lakini niwaombe utulivu. Miili 6 kati 14 imetambuliwa na walikuwa sehemu ya msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na hivyo ameondoka nayo tayari kuelekea mwanza kwa taratibu zingine, kwetu hapa zoezi la kutambua miili 8 linaendelea,hivyo niwaombe wananchi tuendelee kuwa watulivu,".amesema.
Ajali hii imetokea siku moja kabla ya siku iliyopangwa kwa ajili ya maombi maalumu mkoa huo itakayangozwa na viongozi wa dini zote mkoani hapa Januari 12 mwaka huu majira ya saa 3.00 asubuhi.
Akizungumzia Ajali hiyo amesema imetokea Leo saa 12.25 asubuhi katika Kijiji cha Kalemela katika Barabara ya Musoma- Mwanza ,Wilaya ya Busega.
Magari mawili STK 8140 TOYOTA LANDCRUISER iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Wilaya ya Ukerewe kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza iliyogongana uso kwa uso na gari Na. T.281 DER aina ya TOYOTA HIACE iliyokuwa ikitoka Lamadi( Simiyu) kwenda Mwanza.
Mpaka saa 6.00 mchana watu 14 wamefariki na kati yao wanawake ni 5 na wanaume 9.
Aidha wanahabari 6 waliokuwa kwenye gari la Serikali na dereva wao ni sehemu ya waliofariki.
Majeruhi wa ajali ni sita, ambapo 2 wapo kituo cha afya NASA na 4 wamepekwa hospitali ya Rufaa Bugando.
Waliofariki waliokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza ni pamoja na-:
Husna Milanzi - ITV,Johari Shani - Uhuru Digital
,Antony Chuwa - Habari leo Digita,Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.
Majeruhi ni pamoja na Tunu Heman -Mwandishi wa habari wa kujitegemea na Vany Charles - Icon TV
Chanzo cha ajali nI mwendokasi wa magari yote mawiliambapo dereva wa LANDCRUISER alianza kuligonga ubavuni gari Na T 816 DCY TATA BUS akiwa amehama na kwenda kulia na baadaye kwenda kuligonga gari aina ya Hiace iliyokuwa nyuma umbali wa kama M.38..
Madereva wote wamefariki kwenye ajali. .Aidha RC Kafulila amesisitiza kwamba taarifa ya mwisho kuhusu uchunguzi wa ajali itapatikana baada ya Kamati ya Usalama Mkoa kupokea taarifa ya uchunguzi wa ajali hiyo.
View attachment 2076708View attachment 2076725View attachment 2078137
View attachment 2076743
View attachment 2076977
View attachment 2077261
View attachment 2077272
Husna Mlanzi wa ITV
View attachment 2077277
Antony Chuwa wa Habari leo Digital
View attachment 2077278
Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe
View attachment 2077358
Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza
View attachment 2077361
Johari Shani wa Uhuru Digital
View attachment 2078151
Niliacha uandishi wa habari baada JK kutoka madarakani,tulikuwa tukiitwa sehemu,iwe kwa mkuu wa mkoa,taasisi za serikali tunasign elfu 50 hadi laki moja kwa ajili ya kuripoti uongo.Tunapopigiwa simu hata hela ya nauli hatuna tunaambiwa gari litawakuta sehemu fulan.Hii Ni kawaida kupewa hela na kuandaliwa gari kwa ajili ya waandishi wa habari.Vyombo vya habari bado haviko huru,waandishi wanatakiwa wapewe usafir wao ili wasiripoti uongo au maigizo.Kwanza naomba niungane na Watanzania wenzangu kutoa salamu za rambi rambi hakika vifo vya wanahabari hawa na wananchi wengine ingawa sijashuhudia wananchi wa kawaida wakiagwa ni pigo kwa Taifa.
Nikili hakika nimeumia Sanaa maana waliokufa ni age mate wangu.
Sambamba na vifo hivyo ni muhimu tujiulize ukweli hawa wanahabari walikuwa wakifata msafara wa mkuu wa Mkoa nyuma analipokuwa akienda kukagua miladi mlikuwa tayari kwenda kuusema ukweli ambao ungeweza muuzi mkuu wa Mkoa mpaka akawashussha kwenye gari zilizokuwa mwenye msafara wake?
Au mmekufa mkiwa tayari mmezamilia kwenda kuulagai umma wa Watanzania dhidi ya miradi ya ajabu inayoendelea kulutafuna Taifa letu?
Swali Ili naomba lijibiwe na vyombo vyenye mamlaka baada ya kuchunguza miradi hiyo.
Ncha kali
Baada ya kifo chakoSijuwi anapanga kufa lini
Umenikumbusha hii ziara ya obama ilikuwa tanapangiwa kila kitu. Ha haaMaafisa wa Marekani wakati wakitathimini hali na usalama wa rais wa Baraka Obama alipokuja Tanzania, wali konklud kuwa barabara zetu ni mbovu na hatarishi sana kwa usalama wa rais wao, hivyo katika msafar wake aendeshwe kwa mwendo mdogo from ubungo tanesco to airport.
nashangaa usalama wetu wanapo ruhusu kukimbizwa kwa viongozi wetu kwa mwendo wa mashindano ya magari, as if kuna imejensi huko waendapo given ubovu wa barabara.
Nakuunga mkono mkuu..
Wakikujibu nistueKwanza naomba niungane na Watanzania wenzangu kutoa salamu za rambi rambi hakika vifo vya wanahabari hawa na wananchi wengine ingawa sijashuhudia wananchi wa kawaida wakiagwa ni pigo kwa Taifa.
Nikili hakika nimeumia Sanaa maana waliokufa ni age mate wangu.
Sambamba na vifo hivyo ni muhimu tujiulize ukweli hawa wanahabari walikuwa wakifata msafara wa mkuu wa Mkoa nyuma analipokuwa akienda kukagua miladi mlikuwa tayari kwenda kuusema ukweli ambao ungeweza muuzi mkuu wa Mkoa mpaka akawashussha kwenye gari zilizokuwa mwenye msafara wake?
Au mmekufa mkiwa tayari mmezamilia kwenda kuulagai umma wa Watanzania dhidi ya miradi ya ajabu inayoendelea kulutafuna Taifa letu?
Swali Ili naomba lijibiwe na vyombo vyenye mamlaka baada ya kuchunguza miradi hiyo.
Johari Shani wa Uhuru Digital
Misafara ya viongozi imejaa ulimbukeni na ushamba mwingi sana!Misafara ya viongoziji huwa inatembea kwa sifa sana