Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

--
Rais Samia atoa salamu za Rambirambi

''View attachment 2076839

====


Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

Chanzo: Mwananchi

======

UPDATES;

=====

Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni

1. Husna Mlanzi wa ITV

2. Vanny Charles wa Icon. TV

3. Johari Shani wa Uhuru Digital

4. Antony Chuwa wa Habari leo Digital

5. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza

6. Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe

7. Paul Silanga Dereva wao

Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.

View attachment 2077261
Kwa hii mbung’aa nang’ado inaonesha dereva alikuwa anatembea na 150KPH humo sema hiace ilipotokea ndio sielewi au dereva alikuwa anatanua kwenye kilima?
 
Hapo hakuna land cruiser V8. Iliyopata ajali ni land cruiser II - Prado.

Hizo picha ni gari moja ila imepigwa picha angle tofautitofauti.
Wote mnazingua! Hio Cruiser ni LX ya. 1HZ sio V8 wala sio Land Cruiser 2
 
Mimi ninashauri hawa madereva wa serikali wanunuliwe gari za kawaida kama za kwetu watu wa chini. Hizi gari zenye uwezo mkubwa zinawapa viburi na kujiamnini kukimbia mwendokasi wenye matokeo kama haya. Inatakiwa wapewe gari kama kirikuu (suzuki carry) ili tuone kama wataendelea na mwendokasi, wameonywa lakini hawasikii.
Hahahahah hata Kirikuu itapigwa Mosh 3 mzee😅😅😅 tatizo la hawa madereva ni kujiamini kulikopitiliza yeye ana overtake hata kwenye blindspot! Haangalii kuna gari mbele ukute aliion hiace ila akatanua makusudi kabisa ili amalize semi pembeni yake. Mwishowe kashindwa kuimaliza kaivagaa
 
Afanye sherehe msibani, na hicho kibali alichokikalia akitumie yeye kuhama.
Na nasikia amekalia vibali vya watumishi wengine wa hiyo halmashauri.
Yani mtu kakamilisha michakato yote, tamisemi wamempa go ahead hama na kibali wamekituma halmashauri, Mkurugenzi anagoma kusaini na kumpa afunge taarifa ahame.
Inauma.
Sasa kila mtu akikimbia ofisi mnataka abakie pekeyake au
 
Idadi ya watu wanaotembea kwa msafara ipunguzwe, wabaki viongozi wajuu tu,
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alikuwa na ziara Mkoa wa Simiyu?
Unaweza kujiuliza maswali mengi ukakosa majibu....nimeumia mno na kifo cha Husna
Hakuwa na ziara Simiyu walikuwa wanenda ukerewe so walikuwa wanenda kuvukia Bunda, ajali wameipatia wilaya ya busega zamani ilikuwa ni sehemu ya wilaya ya Magu-Mwanza, Walikopatia ajali na makao makuu ya mkoa wa Simiyu ni mbali
 
Magari ya serikali wanajiona kama wao ndiyo wana mamlaka wao wakuu juu ya sheria
Kwenye matumizi ya barabara


Ova
Tatizo ni uzembe yani! Mie naendesha gari ila usalama ni muhimu sana sio kujitanulia kama fala af katika gari ambazo sio salama kwenye barabara ni hizi za kuvunja miwa😅 bora auto ukishindilia brake inaweza simama haraka!

Mtu anakuwa anafungwa mota mie hata kama boss anasumbua ntampotezea tu mpaka ambako naona pako safe nafidia muda😅
 
Tatizo ni uzembe yani! Mie naendesha gari ila usalama ni muhimu sana sio kujitanulia kama fala af katika gari ambazo sio salama kwenye barabara ni hizi za kuvunja miwa😅 bora auto ukishindilia brake inaweza simama haraka!

Mtu anakuwa anafungwa mota mie hata kama boss anasumbua ntampotezea tu mpaka ambako naona pako safe nafidia muda😅
Lakini pia RC kwa mamlaka yake anaruhusiwa kuwa na Police escort ambayo inatangulia kusafisha barabara mbele au mzimu wa ajali ya Sokoine bado ungalipo? kwamba barabara imesafishwa na pikipiki au gari la Polisi lakini anajitokeza mwehu mmoja na ki-hiace chake anaamua kujitoa akili....
 
Unaweza kujiuliza maswali mengi ukakosa majibu....nimeumia mno na kifo cha Husna
Hakuwa na ziara Simiyu walikuwa wanenda ukerewe so walikuwa wanenda kuvukia Bunda, ajali wameipatia wilaya ya busega zamani ilikuwa ni sehemu ya wilaya ya Magu-Mwanza, Walikopatia ajali na makao makuu ya mkoa wa Simiyu ni mbali
Husna yupi mkuu?
 
Umeniwahi kuuliza swali hilo, nakushukuru.

Mkuu wa Mkoa mmoja hawezi kupeperusha bendera yake kwenye mkoa mwingine itifaki inakataza, vivyo hivyo kwa Ma-DC.

Mkoa wa Mwanza umetenganishwa na mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu ambao uko katikati ya Mwanza na Mara, sasa RC wa Mwanza alikuwa anaenda Mara au?


Taarifa imesema RC wa Mwanza msafara huo ulikuwa ni wake, sasa nakunukuu "yuko njiani kuelekea eneo la tukio" tuamini lipi kwamba alikuwa kwenye msafara huo au hakuwemo? Kama msafara haukuwa wa kwake kwanini basi kwenye tukio asiende RC wa Simiyu ambaye tukio limetukia kwenye eneo lake?


Sijawahi kusikia Askari ameshitakiwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani japo tunawaona kila mara wakizivunja hadharani (Mlinda sheria anayetangulia kuvunja sheria), kama hamuamini basi katafuteni kwenye rekodi za Mahakama kama mtapata shauri kama hilo tangu nchi kuwa huru. Zipo scenario ambazo sheria za usalama barabarani zinaweza kuvunjwa e.g. Ambulance, Zimamoto, Misafara ya viongozi wa kitaifa na kimataifa, maandamano yanayopita barabarani yenye kibali halali.

Wanasiasa hawapendi kuona au kusoma kero (hawapendi ziripotiwe) wanapenda kuona au kusoma habari zenye matokeo chanya tu ya kazi zao.

“In politics if you want anything said, ask a man. If you want anything done, ask a woman.”
Usilolijua! Ili ufike ukerewe ukiwa Mwanza ni either uvukie Mwanza mjini, usafiri ni meli almost 5 to 6hrs to ukerewe au upitie Bunda - Kisorya ambako utavuka na fery kwa nusu saa, Mwanza - Bunda Kisorya kwa ule mwendo wao ni 2 to 3hrs
 
Back
Top Bottom