Ndugu zangu kuna taarifa nimezipata kuwa inadaiwa kuna Mgodi umetitia kutokana na mvua zinazoendelea Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu na Watu kadhaa kufukiwa.
Mgodi upo Kijiji kinaitwa Ikinabushu, details za jina na kilichotokea zaidi bado sijazipata.
Mliopo karibu na Bariadi tupeni taarifa zaidi.
======
WATU ZAIDI YA 10 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA
SIMIYU: Tukio la kutitia kwa kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Ikinabushu uliopo Wilayani Bariadi linadaiwa kusababisha watu zaidi ya 10 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Wilaya na Mkoa wote wapo eneo la tukio.
Hali hiyo imetokea wakati mvua zikiendelea kunyesha kwa wingi Mkoani #Simiyu. Taarifa zaidi zitafuata.
=====
UPDATES
Zoezi la kufukua miili ya wachimbaji waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa IKINABUSHU uliopo kijiji cha Ikinabushu Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imefikia 22 hadi kufikia usiku wa Jumamosi January 13.
Mkuu wa Wilaya Bariadi Simon Simalenga amethibitisha idadi hiyo Usiku huu wakati akizungumza na #CloudsDigital
Machimboni ni kama jeshi la ziada, aisee maisha Kule sio kabisa Kuna watu wamejichoka sana, ila nachopenda Kule Kila mtu anamuheshimu mwenzake na kumuona mpambanaji, ujinga ujinga wa kuleteana ubabe ni mara chache sana kuona
Wewe hujawahi pambana wewe mwanaume usiseme hivyo ukifukishwa duniani kupambana tu, yumkini huajwahi lala polisi wewe ama kwenda kwa sangoma chonganishi kama sivyo basi uwe unasali sana dua ibada
Wewe hujawahi pambana wewe mwanaume usiseme hivyo ukifukishwa duniani kupambana tu, yumkini huajwahi lala polisi wewe ama kwenda kwa sangoma chonganishi kama sivyo basi uwe unasali sana dua ibada
acha Polisi mi nimeshakaa jela tofauti tofauti mikoa tofauti na kuhusu kwa Sangoma nilishaogea makaburini sana tu ila mgodini chini ya ardhi siendi na kwenya maji siendi sio kwamba nitaishi milele ila kufa huku najiona hapana 🙌
Pole yao wafiwa na nchi kwa ujumla
Ila kwa biashara hizi na kazi kama ya kuingia chini wakati wa mvua hivi bora serikali ingekuwa inasitisha uchimbaji wa hivyo
Serikali ina wajibu kuwalinda Raia kama hivi
Kweli ndio ajira zao lakini ni hatari sana kwa wakati huu
Kuna sehemu inaitwa Mererani, wanachimba Tanzanite. Kuna jamaa aliniambia wachimba wenye lifespan yao inapunga kwa sababu ya lile vumbi. Vumbi la ile sehemu ni baya sana, liko kama majivu, ukichanganya na moshi wa baruti wanazotumia kulipua miamba, ni hatari. Magonjwa ya mapafu kujaa maji ni mengi.