Simle anaylsis: Matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini za USGN ndio yataamua timu mbili za kufuzu kundi "D"

Simle anaylsis: Matokeo ya mechi za nyumbani na ugenini za USGN ndio yataamua timu mbili za kufuzu kundi "D"

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania.

Kwahiyo, timu zitazoifunga hii timu ya USGN nyumbani na ugenini, ndio zina nafasi kubwa ya kusonga mbele na hapa naona Simba teyari wamejiweka katika mazingira magumu baada ya kupata sare leo hii dhidi ya hii timu.

Simba, RS Berkane na Mimosas, wote wana nafasi za kushinda mechi zao zote za nyumbani ila sio ugenini. Mechi ya ugenini ambayo kila timu kati ya hizi timu tatu wanazoweza kushinda, ni ile tu ambayo timu hizi watakutana na USGN (kibonde) huko Niger.

Kwa maana hiyo, matokeo ya nyumbani na ugenini baina ya hizi timu tatu dhidi ya USGN (matokeo ya kushinda), ndio yataamua timu zipi zifuzu.

USGN ikiendelea kuwa kibonde(isipobadilika), Simba watakuwa na nafasi finyu sana ya kusonga mbele baada ya kukubali sare na hawa vibonde kosa ambalo RS Berkane na Mimisosa sidhani kama watalifanya.

Simba kurudisha matumaini, ni lazima ishinde walau mechi moja ya ugenini au itoe sar na na si kushinda za nyumbani kwani kuna kila dalili timu zote zinaweza kushinda mechi za nyumbani isipokuwa hao vibonde (unless nao waacha kugawa point) na ndio maana naseme mechi na huyu kibonde ndio zitaamua wa kufuzu( Simba teyari wamefanya kosa leo).

Mwisho, mshindi wa kwanza na wa pili katika hili kundi anaweza kupatikana kwa kigezo cha idadi ya magoli ya kushinda kwa timu za RS Berkane na Mimosas.

Japo ni mapema sana, lakini huu ndio muelekeo.
 
Kashabikie siasa mzee, huelewi kama Simba akishinda mechi zake za nyumbani zote atafuzu quarter finals?

Unawaita US Gendarmerie vibonde hujui kwamba hawajawahi kufungwa na yeyote?

Mpira ni mashindano siyo matamanio ya kipuuzi.

Hongera Simba Sc kwa mwenendo mzuri wa mashindano.
 
Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania...
Asee home boy hii analysis yako mbona chenga sana. Hivi unajua bingwa wa CAF champions League msimu uliopita alienda pale mambo yakawa mazito akaja kuweka mambo sawa kwenye game ya nyumbani kwake?
 
Uto kwa kujipa kazi ambazo hazina maana hamjambo, hizi pumba hata msimu uliopita tulivyotoa sare na Merreikh kwao mlizileta, mwishowe tukaongoza kundi. Tafuta rekodi za Usgm wakiwa nyumbani uache umandazi
Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania...
 
Dah! Makolokocho fc leo wameponea kwenye tundu la sindano! Walikuwa wanatoka vichwa chini.
 
Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania...
Luc Eymael hakukosea. Hatuna cha kukusaidia. Endelea kumjampia mumeo kwenye shuka . Hata tukikuelewesha namna gani kuhusu ukubwa wa simba katika bara hili la Afrika huwezi kuelewa. Kwaheri!
 
Ukinonde wa Team utaonekana baada ya 90 za kila mchezo, ASEC mlisema ni kibonde lakini kampiga bao za kutosha tu huyo Berkane ambaye mnapigia upatu, si ajabu Berkane akaenda kufa tena kwa hao waniger.

Hivi ile pitch ta waniger na aina ya uchezaji wao unategemea **** mwarabu atatoka kirahisi hapo? Kawaulize Ahly.
 
Gendarmerie wamefungwa mechi gani nyumbani katika siku za hivi karibuni?
Kwa nini una assume watafungwa na ASEC & RSB? Kumbuka waliweza kupata magoli matatu nyumbani kwa RSB.
Eti kisa katoa sare na Simba sc basi inaonekana ni team ya kufungwa na kila team, ile team ni nzuri mno ikiwa nyumbani na ndio maana hata Simba wamepata goal kuhangaika sana.

Si ajabu RSB akaenda akakaa pale.
 
Back
Top Bottom