Sababu kubwa ni moja tu, hii timu mpaka sasa ndio inaonekana ni kibonde katika hili kundi na haishangazi sana kwani Niger (Timu ya Taifa na hata vilabu vya nchi hiyo) hawana record nzuri katika soka kama tulivyo Tanzania...
Umeongea kwa jicho la kiufundi sana, asiyekuelewa ni punguani pekee, nilishasema timu tishio niliyokwisha kuiona kwenye hili kundi ni Asec mimosas na berkane, licha ya asec kifungwa na simba hapa nyumbani lakini kiufundi walikuwa vizuri sana kuanzia kwenye kujenga mashambulizi yao, umiliki wa mpira, physical yao walikuwa perfect sana,
kufungwa kwao ni mambo ya nje ya uwanja zaidi tunajua mambo yanayofanyika pale kwa mkapa ili simba washinde wala akuna siri juu ya ilo kipimo tutakiona wakienda ivory coast kurudiana maana awatofanya wanachokifanyaga nyumbani, Na hawa gendamarie akuna ubishi ndo kibonde wa kundi ukiwaangalia vizuri kiufundi wana mapungufu mengi Sana kuanzia kwenye safu yao ya ulinzi,
kiungo mpaka ushambuliaji, hivyo ili ujiakikishie kutoboa unatakiwa umfunge uyu kibonde nyumbani kwake alafu umsubilie kwako uzoe point nyingine, hii michuano ni kwenda na hesabu, nimemsikia kocha wa simba anafurahia kupata droo ugenini lakini anasahau amepata droo kwa timu ya aina gani? Suala sio kupata droo tu. i
shu ni umepata droo na timu yenye kiwango gani maana wengine wataenda pale na wataipiga na wewe auna uwezo wakwenda kumfunga Asec au berkane nyumbani kwao kwa simba hii tusidanganyane hapa, akuna timu itakubali kufungwa nyumbani kwao zaidi ya hawa vibonde gendamarie,
saa nyingine ukweli mchungu lakini ndo uhalisia timu itayochukua point 3 nyumbani kwa gendamarie itakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kusonga mbele kimahesabu!