Simon Patrick: Yanga itaenda mahakamani kuweka zuio la kukabidhi timu kwa wazee walioishtaki

Simon Patrick: Yanga itaenda mahakamani kuweka zuio la kukabidhi timu kwa wazee walioishtaki

Hawa Mzee Mpili tu anawatosha, Mzee Mpili ana watu tena anasema ana watu wachafu kwelikweli.
joseph1989 Mzee wenu unamsikia halafu unasema hamuamini imani za kishirikina. Nilikwambia nenda na kimbelembele chako uone kama huyo Mzee hajapewa kazi ya kukushughulikia
 
Nani mwenye uwezo wa kumsajili Aziz Ki hapo?

Wachawi utawajuwa tu kwa tabia za hawapendi wanapoona mafanikio, wanataka bakuli ili wapate nafasi ya kuiba pesa na kukaa magetini siku hizi hamna ni N card tu.

Unanichukulia poa sana eti? Ngoja nichukue timu.
65f8b47b-098e-4b97-bbdd-4eb8bcf77cbf.jpeg
 
Tatizo lenu kubwa ni kwamba hamna mwanasheria, ndiyo maana kila siku mnashindwa kesi.

Haiwezekani taasisi kubwa kuwa na kesi inaendelea Kisutu hadi inaisha mnakuja kulalamika eti hamkushirikishwa.

Hauwezi kusema utaenda kufungua kesi nyingine ya jinai dhidi ya waliokushitaki wewe kwa kisingizio cha walifoji saini, kwanza hao wazee walihitaji saini za wajumbe wa bodi za nini? Inaonyesha Yanga ilituma watu waiwakilishe mahakamani, hao ndiyo walifoji saini za wajumbe, leo wanawakana kuwa hawakuwa watu sahihi. Kosa linakuwaje la anayeshitaki?

Yanga hamna mwanasheria.
Yanga haikutuma mwakikishi ndio maana hukumu inasomeka kama ya upande mmoja. Yaani yanga wawakuhusishwa ila kuna mtu alijifanya kuiwakilisha Yanga lakini hakutumwa na taasisi.
 
Yanga haikutuma mwakikishi ndio maana hukumu inasomeka kama ya upande mmoja. Yaani yanga wawakuhusishwa ila kuna mtu alijifanya kuiwakilisha Yanga lakini hakutumwa na taasisi.
Mnajichanganya. Unasema kuna mtu alijifanya kuiwakilisha Yanga, hapohapo unasema hukumu inasomeka ya upande mmoja. Na wewe unaamini Yanga iwe na kesi Kisutu, mtu atoke zake huko aje kuiwakilisha, hadi kesi inaisha ndiyo Yanga washtuke? Mnafikiria kweli nyie?
 
joseph1989 Mzee wenu unamsikia halafu unasema hamuamini imani za kishirikina. Nilikwambia nenda na kimbelembele chako uone kama huyo Mzee hajapewa kazi ya kukushughulikia
Vip bado upo ulaya ya JF au usharudi......... karudie Komenti yako ya mwisho uliyo andika kwenye mjadala wa Yanga kwenda South. Mimi siamini kwa hivyo vitu vina msaada kwenye mpira sijajua ww wa ulaya ya JF.

Halafu mimi siamini ktk siasa za wazee wala Makomando wa hizi timu.Hata mzee mwenyewe mpuuzi mpuuzi, akiuliza atakwambia timu inahitaji busara,utazani labda busara inalipata posho au mishahara.

Wakae pembeni wawache wenye uweledi.

Halafu hili sekeseke la Yanga lisikufanye ukasahau migogoro na timu yako Kolo FC, maana naona mnajiliwaza kwa hawa wahuni wanaotafuta kula kupitia Yanga. Ila Yanga ipo stable.
 
L

Tangu lini GSM akaongea na media au Instagram?

Mwamedi ndio anajurikana kwa kutangaza kapata hasara na timu haiachi.
Juzi hapo injinia katangaza mapato ya mwaka mzima kuwa wamepata hasara.
Sasa huu ndo Muda wa kuwaachia timu hyo wazee.kama wao wamepata hasara kwanini Wana ng'ang'ania timu?waondoke.yanga ni kubwa kuliko GSM na genge lake.wazew wameamka
 
Vip bado upo ulaya ya JF au usharudi......... karudie Komenti yako ya mwisho uliyo andika kwenye mjadala wa Yanga kwenda South. Mimi siamini kwa hivyo vitu vina msaada kwenye mpira sijajua ww wa ulaya ya JF.

Halafu mimi siamini ktk siasa za wazee wala Makomando wa hizi timu.Hata mzee mwenyewe mpuuzi mpuuzi, ukiuliza atakwambia timu inahitaji busara,utazani labda busara inalipata posho au mishahara.

Wakae pembeni wawache wenye uweledi.

Halafu hili sekeseke la Yanga lisikufanye ukasahau migogoro na timu yako Kolo FC, maana naona mnajiliwaza kwa hawa wahuni wanaotafuta kula kupitia Yanga. Ila Yanga ipo stable.
Kwa hiyo mlipowakabidhi timu wazee kwenye ile mechi sijui ilikuwa derby ile mlikuwa mna lengo gani? Leo mnawarushia kila aina ya tusi na dharau kisa watu wawili watatu mnaotofautiana nao wamehoji taratibu za kisheria. Nasemaga vyura huwa mna kumbukumbu ndogo sana.
 
🔹 Siamini mahakama ya nchi inayofuata common law system inaweza kuendesha kesi ex parte bila kumpa summons mdaiwa kweli?

🔹 Kweli taasisi inayojulikana kama YANGA na yenye wanasheria hawajui kweli UWEPO wa kesi hiyo au ni dharau na kiburi kwa mahakama?

🔹 Watawezaje ku set aside ex parte judgement na kwa sababu zipi?
 
Kwa hiyo mlipowakabidhi timu wazee kwenye ile mechi sijui ilikuwa derby ile mlikuwa mna lengo gani? Leo mnawarushia kila aina ya tusi na dharau kisa watu wawili watatu mnaotofautiana nao wamehoji taratibu za kisheria. Nasemaga vyura huwa mna kumbukumbu ndogo sana.
Walikabidhiwa na hao mashabiki wanao amini kwenye wazee, mimi siamini kwenye wazee. Kwanza ulimsikiliza huyo mzee leo interview yake Wsafi FM ? Hoja zake umezisikia......?au ndio unajipa Moyo Hersi anaondoka..... Hersi Yupo na ta endelea kuwepo na mdaa huu tunajiuliza bango tuliweke barabara gani msimu ujao.

Hukumu ya mwaka jana ,nakala imepostiwa jana, michezo ya kihuni ya hao wazee ndio maana si wakubali.
 
Walikabidhiwa na hao mashabiki wanao amini kwenye wazee, mimi siamini kwenye wazee. Kwanza ulimsikiliza huyo mzee leo interview yake WhatsApp? Hoja zake umezisikia......?au ndio unajipa Moyo Hersi anaondoka..... Hersi Yupo na ta endelea kuwepo na mdaa huu tunajiuliza bango tuliweke barabara gani.

Hukumu ya mwaka jana ,nakala imepostiwa jana
Usinione napost kuhusu hili wala sina muda wa kufuatilia hayo mauzauza yenu
 
Kwa hiyo mlipowakabidhi timu wazee kwenye ile mechi sijui ilikuwa derby ile mlikuwa mna lengo gani? Leo mnawarushia kila aina ya tusi na dharau kisa watu wawili watatu mnaotofautiana nao wamehoji taratibu za kisheria. Nasemaga vyura huwa mna kumbukumbu ndogo sana.
Lengo lilikuwa kuwapiga mbumbumbu kono la nyani.
 
Usinione napost kuhusu hili wala sina muda wa kufuatilia hayo mauzauza yenu
Hungekuwa huna muda husinge post humu JF, ungedeal na kambi yenu huko Misri na pacha strikers wenu Fred na Jobe.
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Yanga haikutuma mwakikishi ndio maana hukumu inasomeka kama ya upande mmoja. Yaani yanga wawakuhusishwa ila kuna mtu alijifanya kuiwakilisha Yanga lakini hakutumwa na taasisi.
Yanga ni taasisi kubwa inajulikana kila Sehemu hapa nchini inamana kesi ilikuwa inaendelea taasisi haijui kama kuna kesi mahakamani au mnataka watu wote tuonekane mazuzu
 
Yanga inafanya mkutano na waandishi wa Habari muda huu, fuatilia hapa kitakachojiri

Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amekiri uwepo wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Baraza la wadhamini wa Yanga SC ambapo ilisikilizwa upande mmoja na kupelekea kutolewa hukumu ya Julai August 2, 2023.

Aidha, mwezi wa 6 mwaka huu, Yanga SC ilipata taarifa ya ombi la Mahakama kutaka uongozi wote utoke madarakani, ambapo Eng. Hersi aliekekeza idara ya sheria kufuatilia suala hili na kugundua kuwa kesi hii iliendeshwa upande mmoja, pia waligundua kughushiwa kwa saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini. Pia, waligundua uwepo wa kundi la watu nyuma ya wazee hao linalotumika kuvuruga amani ya Yanga hivyo kwa kutumia vyombo vya dola wanashughulikia suala hili.

Kwa hatua ya sasa, Yanga imepekela maombi ya kuomba kuongezewa muda wa mapitio ya hukumu na kesi hiyo sababu hawakushirikishwa tangu awali, kwakuwa watu walioshiriki awali hawakuwa na uhalali kisheria (hawakuwa watu sahihi pia walifoji saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini)

Pia, itapeleka ombi la kuzuia utekelezaji wa hukumu hiyo ili uongozi usiondolewe pamoja na kuzuia wazee wasikabidhiwe timu kwa sasa.

Wakili Simon amesema Yanga itafungua kesi ya Jinai kwa wahusika wote waliopeleka kesi hii mahakamani kwani walighushi saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini wa Yanga.

Pia soma:
1. Hii hapa Hukumu ya kutotambulika kwa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga. Yumo Mwigulu, Mwambe na Tarimba

2. Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Kumbe ilikuwa ni "ex parte judgement"? Acha Makolo yaanze kukenua meno hovyo na kushangilia. Ngoja sasa shauri lirudi tena mahakamani liwekewe "court injunction" kisha mabishano ya kisheria yaendelee.

Mipango kabambe ya Yanga haiwezi kuwa "derailed" kirahisi namna hiyo. Ndiyo maana halisi ya msemo, DAIMA MBELE, MWIKO NYUMA.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Back
Top Bottom