Tangu enzi za Idris Abdul Wakil.
Idris Abdul Wakil alipambanishwa na kivuli enzi zile kura za "Ndiyo/Siyo". Akashindwa (watu waliomkataa walikuwa wengi kuliko waliomkubali).Matokeoyakatoka, mpakawatu wa Daily News wakayaona.
Nyerere alivyopata habari, wakafanya sarakasi zaowakabadili ndiyo zikawa siyo na siyo zikawa ndiyo.
Watu waliokuwa Daily News kipindi hicho wanajua hizi habari.
Baadaye aliendeleza mchezo huohuo,Salmin Amour alikuwa anamletea kiburi sana Nyerere. Siku Salmin alivyoshindwa uchaguzi,alimpigia Nyerere magoti abadilishe matokeo, Nyerere akanyanyua simu akapiga simumoja tu matokeo yakabadilishwa.
Zamani nilivyokuwa naambiwa CCM wamebadili matokeo, nikawa naona kama ni propaganda za wapinzani, baadaye nikaja kukaa na mzee mmoja alikuwa mkubwa wa usalama, karibu sana na Nyerere, akasemamwenyewe walifanya michezohiyo sana, na wahenga wa Daily News wakanifumbua machokwamba michezoimechezwa Zanzibar tangu kabla ya vyama vingi kuanza, maana kule kulikuwa na mpasukowa Unguja/Pemba tangu kabla ya vyama vingi kuanza.