Simon Rwamugila(Omutwale): Nyerere alipewa u-Head Prefect akatuchanganya akili Tabora Boys

Simon Rwamugila(Omutwale): Nyerere alipewa u-Head Prefect akatuchanganya akili Tabora Boys

Mzee mohamed said au sio!?
Wise...
Mimi nilichofanya nimeandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa
Tanganyika ambayo wengi mlikuwa hamuijui.

Hili la kwanza.

Pili nikaeleza matatizo yaliyojitokeza baada ya uhuru na iliwahusu sana
Waislam.

Kwa bahati mbaya wako ambao hawakupendezewa na historia ile na ikawa
natuhumiwa kwa udini kwa sababu nimeeleza mchango wa Waislam katika
kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaweza kuangalia hapa kwani jicho halisahau kile jicho la camera liliona:
UHURU DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA



Selemani Mamba
Shujaa wa Maji Maji


ABDULRAUF%2BSONGEA%2BMBANO.jpg


Sultan Abdulrauf Songea Mbano wa Songea
Shujaa wa Maji Maji

KLEIST%2BSYKES%2BAND%2BSONS.jpg


Kushoto aliyesimama ni Ally Kleist Sykes, na kulia kwake ni
Abdulwahid Kleist Sykes, mbele kushoto ni Kleist Sykes
Mbuwane na Abbas Kleist Sykes. Katika hawa aliye hai ni Abbas.
Ukoo huu umeacha kumbukumbu nyingi kwa maandishi katika harakati za
kuunda African Association 1929 na kuunda TANU 1954. Picha hii imepigwa
mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam kutoka Lower Kabete Kenya
alipokuwa akipata mafunzo ya kijeshi katika King's African Rifles kabla
hajakwenda Burma kujiunga na Burma Infantry. Angalia utaona Abdul amevaa
sare ya Jeshi la Mfalme wa Uingereza. Ilikuwa akiwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia
(1938 - 1945) ndipo alipoamua kuwa 6th Battalion iliyokuwa na askari kutoka
Tanganyika waunde TANU wakirudi Tanganyika kudai uhuru.

AFRICAN%2BASSOCIATION%2BOFFICE%2B1933.jpg


Ufunguzi wa Jengo la African Asociation 1933 jengo lililojengwa na uongozi wa
Kleist Sykes kati ya 1929 - 1933 na hapa ndipo ilipoundwa TANU 1954 wanae
wawili Abdul na Ally wakiwa waasisi wa chama hicho.

WAASISI%2BWA%2BTANU%2B1954.JPG


Waasisi wa TANU 1954

BARAZA%2BLA%2BWAZEE%2BWA%2BTANU.jpg


Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir 1955

HAMZA%2BMWAPACHU.jpg


Hamza Kibwana Mwapachu 1913 - 1062

ABDUL%2BSYKES%2BNA%2BJULIUS%2BNYERERE.JPG


Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
katika dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957



Kushoto: Bi. Tatu bint Mzee, wa tatu Julius Kambaraga Nyerere
wa tano Bi. Titi Mohamed wanamsindikiza Mwalimu Nyerere
Uwanja wa Ndege safari ya UNO 1955

SHEIKH%2BSULEIMAN%2BTAKADIR.JPG


Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere
Nyuma kulia: John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere.
 
Kuna mkurupukaji alitaka kuifunga JF sijui madini kama haya yangepatikanaje
 
Kumbe hii tabia ya kuchakachua matokeo ilianza hata kabla hatujapata UHURU!!!!!!!!!
 
Tangu enzi za Idris Abdul Wakil.

Idris Abdul Wakil alipambanishwa na kivuli enzi zile kura za "Ndiyo/Siyo". Akashindwa (watu waliomkataa walikuwa wengi kuliko waliomkubali).Matokeoyakatoka, mpakawatu wa Daily News wakayaona.

Nyerere alivyopata habari, wakafanya sarakasi zaowakabadili ndiyo zikawa siyo na siyo zikawa ndiyo.

Watu waliokuwa Daily News kipindi hicho wanajua hizi habari.

Baadaye aliendeleza mchezo huohuo,Salmin Amour alikuwa anamletea kiburi sana Nyerere. Siku Salmin alivyoshindwa uchaguzi,alimpigia Nyerere magoti abadilishe matokeo, Nyerere akanyanyua simu akapiga simumoja tu matokeo yakabadilishwa.

Zamani nilivyokuwa naambiwa CCM wamebadili matokeo, nikawa naona kama ni propaganda za wapinzani, baadaye nikaja kukaa na mzee mmoja alikuwa mkubwa wa usalama, karibu sana na Nyerere, akasemamwenyewe walifanya michezohiyo sana, na wahenga wa Daily News wakanifumbua machokwamba michezoimechezwa Zanzibar tangu kabla ya vyama vingi kuanza, maana kule kulikuwa na mpasukowa Unguja/Pemba tangu kabla ya vyama vingi kuanza.
Ooo
 
Kumbe Nyerere michezo ya kubadili matokeo ya uchaguzi hajaanza Zanzibar.

"Msimamo wa Nyerere. Msimamo wa Nyerere. Ni kipaji cha mwenyezi Mungu baaba, kapewa tangia tumboni, kabla hajazaliwa"
Alikua mtaalam wa biology na English lakini hesabu za kutoa makumi hajawahi kosea akamwigiza benjamini mkapa kura za mshindi wakwanza kutolewa 240000-112000 mshindi wa pili lazima utangazwe ccm imekopi ....imekua luleko[emoji23][emoji23]
 
huyu omutwale namjua alikuwa na watoto wake kama sita hivi wote wanacheza mpira balaa, alafu wana fujo ukimgusa mmoja wanakuchangia kama nyuki, ila kusema ukweli ukanda ule wa kiziba ulisheheni watu muhimu sana kwa Taifa ili, mfano Berenado mulokozi, Mzee kagasheki baba khamis kaghasheki, mzee Abdunuru suleimani, na wengine
Mzee Kagasheki hatoki Kiziba.
 
Kama kawaida yangu huwa nataka kujua yaliyoendelea Miaka ya Nyuma hasa kutoka kwa watu waliopigania nchi hii na kudai uhuru

Simon Rwamugila Kwa koo za Kihaya ana jina la Omutware yaan mtu au mshauri wa karibu wa Mukama(King)
Ukifika bukoba mjini unaelekea kiziba kwa kutumia njia ya Uganda ,ukifika katoma unachipuka kama unaelekeea Mugana kabla ya Mugana kuna njia ya Kwenda Ishozi, Kiziba unafika Kwa Omutwale Mushaijaki,

Mzee Simon Rwamugila Mushaijaki ni miongoni mwa wazee waliopigania haki nchini Tanzania na kabla ya kuja Tanzania alaikaa na kuiwakilisha Tanzania Nchini Ujerumani, mpaka miaka ya 70 akarejea nchini Tanzania,

Kuna shirika linaitwa TIDESO ni miongoni mwa waanzilishi wa mwanzo wa shirika ilo ambapo alitumia kiinua mgongo chake kuhakikisha wahaya wanaochipukia wanaenda shule, na walioshindwa kuendelea aliwapeleka Uganda, Mchango wake ni mkubwa mno, Hatimaye mwaka 2008 alitangulia mbele ya haki,

Nimewahi kupata kukaa na mzee huyu na akanisimulia mambo mawili kuhusu Nyerere na Dhana ya kupata uhuru

1. HAKI NA NYERERE ALIVYOPENDA HAKI

Anasema wakiwa shule ya sekondari Tabora maarufu kama Tabora Government School bado mchanganyiko, viongozi wa shule walizoea kubagua wanafunzi wengine na kuwapangia kazi ilikuwa ni kwa kubaguana, kuna waliopewa kazi za kunyanyaswa na kuna waliopendelewa, Juliusi Nyerere hakuopenda suala ili kabisa na aliumia mno kuona haki haitendeki kabisa, walipofika kidato cha tatu Bwana Juliusi Nyerere alichaguliwa kuwa Kakaka Mkuu na alikuja na mabadiriko kadha wa kadha.

"Ilikuwa ijumaa tumetoka kumaliza uchaguzi kabla hajafanya suala lolote alipanda juu ya bench ndani ya holi la chakula akatumia kijiko chake akagonga chuma kwa nguvu akasema tangia leo Meza zote za chakula tunapokaa zitapangwa upya na madish ya chakula yote yatagawiwa sawa, maana sisis viongozi tulikuwa tumejitenga tunakula kivyetu na Tunajaza nyama na chukula kizuri alafu wengine hawapati share kama ya viongozi" anaendelea kusimulia

"Ilikuwa vigumu kumuelewa nyerere lakin bwaro zima lilizizima kelele za kushangilia uku viongozi wakijifanya kususa na kununa na kuchukia wakasema tumefanya kosa kubwa sana kumchagua huyu bwana, maana baada ya hapo aliwaambia viongozi kwamba pamoja na kwamba sisi ni viongozi lakini tunapaswa kuongoza kwa kuonesha mfano, ndo maana nataka kila kiongozi awe na kipande chake cha bustani na eneo liliofyekwa vizuri alilofyeka yeye kama mfano kwa wengine. Baadae tuliendana na kasi yake na cha kushangaza utaratibu ulifuatwa bila kuingiliwa na walimu, kwa mwonekano bwana Nyerere alikuwa mdogo ila akija parade kutoa neno tunasikiliza kwa makini maana alikuwa mtu wa ajabu mno na hali ya juu ya ushawishi, hata hayo ya bustani viongozi baadhi walichelewa lakin yeye akaanzisha ya kwaqke kama kaka mkuu na kuwahamasisha, hivyo bwanan huyu alipenda usawa sana." akamalizia point hiyo

2. USAWA WA JINSIA NA RANGI SHULENI

Mutwale anaendelea kusimulia hapa anasema
''Siku moja akapata taarifa kwamba kama kuna ubaguzi hapa shuleni hasa kwa jinsia ya kike na kwa wahindi na waarabu , Kulikuwa kuna utaratibu wa kuwachagua wawakilishi wa madarasa yaan viongozi ambapo aliingilia mchakato kidogo nje ya utaratibu.maaana waafrika waliwanyima uongozi wanawake na waarabu.

Nakumbuka tulienda darasa la form two kuna watu walipendekeza majina ya wagombea ambao watapigiwa kura na Nyerere alisema anataka watu kupiga kura kwa kunyoosha mikono juu si kwakuandika kwenye karatasi ila kwasababu ya undue influence mtanyoosha mikono mkiwa mmeinama chini bila kuona nani kampigia nani. Zoezi likaanza yaliletwa majina matatu mdada mmoja na wavulana wawili, akawaambia tunaanza zoezi na aliyekuwa anahesabu kura alikuwa mzee wanzagi ambaye alitutangulia darasa, akawaambia wanaomtaka fulani. Kwakweli walinyoosha mikono sana kumuunga mkono mvulana mmoja wa kusini walinyoosha kama takribani 40 kati ya 50 na zaidi.

Nyerere akaadika 7 kati ya 50, alafu akauliza wanaomtaka huyu mwingine aliyekuwa chaguo la mwalimu wakanyoosha wawili Nyerere ankumbuka aliandika 29 alafu wanaomtaka wa tatu akaandika alafu zilizobaki kaandika hawakunyoosha maana ilikuwa vigumu kumbishia maana walikuwa wameinamisha vichwa, akawa amefanikiwa kubalance mambo

Tukaenda darasa Jingine ambalo alituma mtu kabla kwamba apendekeze jina la Iqbar muhindi mmoja , baada ya kufika akacheza mchezo ule ule na ukawepo uwakilishi sawa, kwakweli bwana Nyerere alikuwa na Iq kubwa mno,

PIA RWAMUGILA ALINISIMULIA DHANA YA UHURU HURU NA UHURU FUNGWA

Rwamugila Pia akazungumzia tulivyopata uhuru akashangilia lakin mwanasheria mmoja mzungu akamwambia kwamba "Mr. Simon you think Tanganyika gained independence? Rwamugila akamjibu yes, now we are free! Mzungu akacheka akasema "we are just reducing administration costs that’s why every colony will belong to union of previous colonial master, no one granted independence and then we colonize acording to nature time and situation "' mzee Rwamugila akaniambia kumbe haukuwa uhuru kama alivyodhania

Julius_Nyerere_cropped.jpg

Mwalimu Nyerere


10425388_10204182558142214_874747753157115705_n.jpg


Omutwale Mushaijaki Simoni Rwamugila

Ni hayo tu kwa leo

Britanny
Britanicca inaoneka wewe niwa Ishozi Kyerima
 
Back
Top Bottom