Simon Rwamugila(Omutwale): Nyerere alipewa u-Head Prefect akatuchanganya akili Tabora Boys

Mzee mohamed said au sio!?
Wise...
Mimi nilichofanya nimeandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa
Tanganyika ambayo wengi mlikuwa hamuijui.

Hili la kwanza.

Pili nikaeleza matatizo yaliyojitokeza baada ya uhuru na iliwahusu sana
Waislam.

Kwa bahati mbaya wako ambao hawakupendezewa na historia ile na ikawa
natuhumiwa kwa udini kwa sababu nimeeleza mchango wa Waislam katika
kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaweza kuangalia hapa kwani jicho halisahau kile jicho la camera liliona:
UHURU DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA



Selemani Mamba
Shujaa wa Maji Maji




Sultan Abdulrauf Songea Mbano wa Songea
Shujaa wa Maji Maji



Kushoto aliyesimama ni Ally Kleist Sykes, na kulia kwake ni
Abdulwahid Kleist Sykes, mbele kushoto ni Kleist Sykes
Mbuwane na Abbas Kleist Sykes. Katika hawa aliye hai ni Abbas.
Ukoo huu umeacha kumbukumbu nyingi kwa maandishi katika harakati za
kuunda African Association 1929 na kuunda TANU 1954. Picha hii imepigwa
mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam kutoka Lower Kabete Kenya
alipokuwa akipata mafunzo ya kijeshi katika King's African Rifles kabla
hajakwenda Burma kujiunga na Burma Infantry. Angalia utaona Abdul amevaa
sare ya Jeshi la Mfalme wa Uingereza. Ilikuwa akiwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia
(1938 - 1945) ndipo alipoamua kuwa 6th Battalion iliyokuwa na askari kutoka
Tanganyika waunde TANU wakirudi Tanganyika kudai uhuru.



Ufunguzi wa Jengo la African Asociation 1933 jengo lililojengwa na uongozi wa
Kleist Sykes kati ya 1929 - 1933 na hapa ndipo ilipoundwa TANU 1954 wanae
wawili Abdul na Ally wakiwa waasisi wa chama hicho.



Waasisi wa TANU 1954



Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir 1955



Hamza Kibwana Mwapachu 1913 - 1062



Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
katika dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957



Kushoto: Bi. Tatu bint Mzee, wa tatu Julius Kambaraga Nyerere
wa tano Bi. Titi Mohamed wanamsindikiza Mwalimu Nyerere
Uwanja wa Ndege safari ya UNO 1955



Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere
Nyuma kulia: John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere.
 
Kuna mkurupukaji alitaka kuifunga JF sijui madini kama haya yangepatikanaje
 
Kumbe hii tabia ya kuchakachua matokeo ilianza hata kabla hatujapata UHURU!!!!!!!!!
 
Ooo
 
Kumbe Nyerere michezo ya kubadili matokeo ya uchaguzi hajaanza Zanzibar.

"Msimamo wa Nyerere. Msimamo wa Nyerere. Ni kipaji cha mwenyezi Mungu baaba, kapewa tangia tumboni, kabla hajazaliwa"
Alikua mtaalam wa biology na English lakini hesabu za kutoa makumi hajawahi kosea akamwigiza benjamini mkapa kura za mshindi wakwanza kutolewa 240000-112000 mshindi wa pili lazima utangazwe ccm imekopi ....imekua luleko[emoji23][emoji23]
 
Mzee Kagasheki hatoki Kiziba.
 
Britanicca inaoneka wewe niwa Ishozi Kyerima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…