Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

lakini nilitarajia kuona serikali ikitenga ward maalum hospitali kwa ajili ya wagonjwa hao, mfano wakati wa kipindupindu.
Kwa hili nakubaliana nawe mkuu. Lkn tatizo jiwe serikali yake imefilisika. Mwezi huu kachelewa hata kuwalipa mishahara watumishi wa umma. Hana hela.
 
Tusisumbuane akili hapa bila sababu za msingi hakuna mtanzania asiyejua kuwa Kuna Corona na hakuna mtanzania asiyejua njia za kujikinga na Corona.

Hivyo watu kujikinga na kuchukua tahadhari si mpaka Rais atamke Kama wewe umeshindwa kujichunga mwenyewe na familia yako basi hilo ni tatizo lako binafsi na niujinga wako.

Kinachopigiwa kelele na wapinzani kuwa Rais atangaze Kuna Corona ili wapate point ya kuzodoa kwamba ULIJIDAI HAIPO SASA KIKO WAPI (wakati huo wamesahau walivyokuwa wanajazana kwenye mikutano ya kampeni bila hata hizo barakoa)

Hilo ndio lengo kuu na tunalijua hivyo lisemeni tu wazi wala msisingizie kuwa Rais hajatamka ndio mana watu hawachukui tahadhari.

Usipojikinga hilo ni tatizo lako na familia yako.
 
Reactions: nao
Safari hii JPM atatoa tamko hakuna kutangaza marehemu ,kesho msubirini akizindua majani sijui miti chatu country
 
Msimamo wake kama upi sasa? Inavyoonesha nyie ni wajinga sana yani!

Unataka mpaka rais aje aseme fanya hivi na vile? Hukuwepo wakati corona inaanza? Pamoja na kelele zenu alisema huu ugonjwa hakuna njia iliyofanikiwa na hivyo tuishi nao tu. Na akasema wazi kwamba hatafungia watu ndani kama mnavyotaka. Cha ajabu sana mnalalama huku mnaenda kurundika huko kariakoo alafu unaingia humu jf kupiga mayowe.

Acheni hizo jamani kama unaogopa sana kaa ndani kwako na familia yako hadi utakaposikia corona imeisha kabisa duniani ndio unatoka
 
Kwa hili nakubaliana nawe mkuu. Lkn tatizo jiwe serikali yake imefilisika. Mwezi huu kachelewa hata kuwalipa mishahara watumishi wa umma. Hana hela.

Labda hili la kutokuwepo kwa hela ndipo tatizo lilipo.
 
Kinachopigiwa kelele na wapinzani kuwa Rais atangaze Kuna Corona ili wapate point ya kuzodoa kwamba ULIJIDAI HAIPO SASA KIKO WAPI (wakati huo wamesahau walivyokuwa wanajazana kwenye mikutano ya kampeni bila hata hizo barakoa)
Siyo kila anayepiga kelele ni mpinzani mkuu. Maaskofu umewasikia, na Kuna watu chungu nzima. Lkn wote hawana hoja zenye mashiko.

Binafsi naona jiwe ana misimamo yake fulani tu. Lkn siyo kwamba anawaogopa wapinzani eti watamzodoa.
 
umeandika vizuri mkuu sema kila mtu achukue tahadhari
 


 
Kuna watu walinunua barakoa kwa wingi sasa baada ya watu kutozivaa wanaona wataingia hasara ndio maana wanataka itangazwe kuwa ipo corona ili wauze hayo ma barakoa kwa bei gari,
Kabla ya corona ziliuzwa shilingi 100 ila baada ya corona wanauza mpaka elfu mbili au tatu
Baada ya kupuuza corona watu wanaona hasara ya hayo ma barakoa na ndio wengi wanatusumbua humu.
 
Wenye akili tumekuelewa! Madebe matupu yaache yaendeleale kupiga kelele!

Kuna mtu leo kaniambia hali sio nzuri. Nikamuuliza umefiwa? Akasema hapana amesoma tuitaa! Nyambafu..
 
Hakuna msimamo sahihi wewe wa kusema uongo na kusababisha Watanzania kutojikinga hivyo kuongeza kasi ya maambukizi na vifo. Mbona Nchi za jirani Marais wamesema ukweli kuhusu ugonjwa huo na kila siku wanatoa taarifa ya maambukizi mapya na vifo vipya kwanini yeye aendelee kung’ang’ania kuudanganya umma wa Watanzania huku yeye mwenyewe akiwa kajificha kijijini? 😳
Nakubalia nawe kuwa watanzania tunaongozwa na saa mbovu (dikteta). Lln hata saa mbovu kuna wakati inaonyesha muda sahihi. Kwa msimamo wake juu ya korona ni sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…