Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Mpaka sasa umefiwa na Ndg wangapi?
 
Si kweli, maana kama ni hela ilishakuja na hakukuwa na lockdown. Mimi sio muumini wa lockdown na wala siko hapa kutaka lockdown, lakini nilitarajia kuona serikali ikitenga ward maalum hospitali kwa ajili ya wagonjwa hao, mfano wakati wa kipindupindu.
Weka wodi nyumbani kwako ujitenge
 
Amekupa jibu Sahihi! Jitolee taarifa mwenyewe na nyumba yako inatosha!
 
Anaogopa kuteteresha uchumi wa nchi, maana tamko lake litaathiri sekta nyingi za biashara na huduma.
 
Kwa hiyo wanatangaza na Corona ina pungua?

Mbona mnakuwa wapumbavu?

Huu ugonjwa mpaka sasa hivi hakuna njia iliyofanikiwa,

Sasa kajificha kijiji ukitaka aje ajifiche kwako?
 
Wenye akili tumekuelewa! Madebe matupu yaache yaendeleale kupiga kelele!

Kuna mtu leo kaniambia hali sio nzuri. Nikamuuliza umefiwa? Akasema hapana amesoma tuitaa! Nyambafu..
Ni wajinga sana hawa watu! Ukiona lile li kigogo linapiga kelele kule twiter utafikiri labda kuna njia imeonesha kufanikiwa kuzui huu ugonjwa kumbe bure tu
 
Kwani pamoja na uongo wake uchumi haujatetereka? Mbona ulitetereka hata kabla ya Covid-19 kutokana na sera zake MUFILISI na Covid-19 ndiyo imeharibu kabisa?
Anaogopa kuteteresha uchumi wa nchi, maana tamko lake litaathiri sekta nyingi za biashara na huduma.
 
Siyo kila anayepiga kelele ni mpinzani mkuu. Maaskofu umewasikia, na Kuna watu chungu nzima. Lkn wote hawana hoja zenye mashiko.

Binafsi naona jiwe ana misimamo yake fulani tu. Lkn siyo kwamba anawaogopa wapinzani eti watamzodoa.
Mkuu amini ninacho kuambia hawa wanao lilia Sana kuwa Rais atamke hadharani kuwa Kuna Corona ujue kabisa kuna kitu ama nguvu kubwa nyuma yao, hawa maaskofu na wengineo si mara yao ya kwanza kutamka maneno Kama hayo.

Labda nikuulize, wakati Corona ilipo anza na watu wakawa na hofu kubwa hadi baadhi ya makanisa kufunga makanisa yao mfano Yule Askofu wa Karagwe, kelele nchi nzima kuwa Rais afunge baadhi ya miji mfano dar es salaam je ni nani aliyekuja kuwapa uhakika kuwa Corona hakuna hadi wakarudia maisha ya kawaida hadi hivi leo?? Kuna dawa ililetwa kuizuia hiyo Corona??

Aliye wapa amri ya kufungua yale makanisa wakati waliyafunga kwa amri yao wenyewe ni nani?
Kwanini walifungua? Je Corona iliisha na Kama iliisha iliishaje ishaje?

Kwanini leo kina Askofu Bongaza na wenzake walio amua kufunga makanisa yao kipindi kile wasifunge tena Kama kweli wameona wimbi kubwa la vifo vya Corona Kama walivyo fanya mwanzo, kwanini wasubiri amri ya Rais?

Tuje kwa hawa wana siasa, wakati wanaondoka bungeni kwenda kujiweka karanitini ilikuwa ni amri ya nani??
Na walirudi kwa amri ya nani?? Na waliporudi ugonjwa ulikuwa umeisha na Kama uliisha uliishaje?

Kwenye kampeni walizungumza nini kuhusu Corona na walikuwa wanatumia mbinu zipi kuwalinda watu (wote tuliona jinsi kampeni zilivyo endeshwa)

Sasa leo kwanini watumie nguvu kubwa namna hii kushinikiza Rais atangaze Corona kurudi tena ( kwani ilikwenda wapi ikiwa walipinga kila kitu kilichosemwa na kufanywa na serikali?)

HAPO KUNA KITU KINATAFUTWA KWA MGONGO WA CORONA.

Watu wanaugua, wapi wanako ugua je unaona jinsi wanafunzi wanavyo jazana vyuoni kwenye ma hostel ilipuke Corona kikweli kweli utaweza kuificha mule??

Watu wawe wanapukutika pale k/koo unaweza kuficha pale tusijue hadi tusubiri waraka wa maaskofu ndio tujue Kuna Corona.?

Narudia tena tahadhari haihitaji kauli ya Rais na Corona si mtaji wa kisiasa hauta wasaidia na wala si mbinu nzuri ya kupenyeza propaganda zisizo na mashiko.
 
Mkuu uneongea vizuri sana!

Uzuri kwenye hili la corona Magu hawezi kutuangusha eti afuate ushauri wa wajinga kina kigogo
 
Mkuu kwa wimbi la kwanza la korona. Dunia nzima iliweweseka, hofu ilikuwa juu kwa kila mtu. Hivyo kila lililosemwa na mzungu liliaminiwa kwamba ndiyo suluhu ya tatizo. Kongole kwa dikteta jiwe aliyejiongeza kwa kufikiria nje ya box.

Kwahiyo hata maaskofu na wanasiasa hawakuweza kuukwepa mtego huo wa hofu na kumwamini mzungu
 
Ndo maana unakujaga na thread mara mwanamke mara mwanaume...

Kwahiyo watu wanakufa na madaktari hata kushindwa kutoa tahadhari Kwa uwazi ndo msimamo sahihi?
Hata watu kuambiana kuna Corona wanaogopa ..ndo msimamo Sahihi?
Ninavyofahamu hakuna siku serikali ilitangaza watu waache kuchukua tahadhari? Hao madaktari walikatazwa kuchukua tahadhari. Kuna mtu kawakataza kutaja neno corona ikiwa linakonga nyoyo zao? Toeni basi ushauri nini kifanyike siyo kutwa kulalama tu kama watoto yatima.
 
Sasa Kama ni hivyo basi waendelee kumuamini huyo Mungu tu au kabadilika hawasikii tena siku hizi, hadi waanze kutoa matamko na mashinikizo ya kipuuzi namna hii??

Maana kama hapakuwa na dawa na wakafungua makanisa na hawa wana siasa nao wachumia tumbo (walio tayari kutumia njia yoyote iliyo mbele yao kupata mtaji wa kisiasa bila kujali athari za mashinikizo yao kwa jamii ) wakaamua kurudia hali ya kawaida yamaisha ina maana si walifanya hivyo kwa Imani tu Sasa kelele za nini?

Haya huyo mzungu wanaye muamini kawapa suluhu gani ya tatizo hadi hivi leo?
 
Umeandika nini sasa wewe zaidi ya kuonyesha chuki za kijinga zisizo na Maana

Jibu hoja, Je? Rais aifunge nchi? Na akiifunga, korona ndio itapotea?

Kwa nini haijapotea huko ulaya walikojaribu kujifungia?
Jaribu kufikiri kabla ya kuandika.
Kutoa tahadhari na kuhakikisha raia wanatekeleza njia mbadala za kupunguza maambukizi ni JUKUMU LA SERIKALI na sio raia wa kawaida.
Hakuna mtu anataka kufungiwa ndani lkn km itasaidia kupunguza maambukizi basi ziwepo njia mbadala kama kupunguza misongamano isio ya lzm. n.k
We kwa mtazamo wako unaona kuna la maana linafanyika hapa?

Acheni ushabiki wa kijinga.
Corona inaua na inamaliza uchumi wa nchi nyingi.
Lzm watu wajiongeze wakisaidiwa na serikali yao sio kubwabwaja tu.
 
Umekosea.
Itakuwa hunijui vema. Endelea kunifuatilia utanifahamu uzuri
ewooooooo mmmmmmh... unalako jwambo... mimi husoma nikiyakuta huwa sifatilii watu humu.. ila nikiamua ni kwa seconds nakuja na kukuonyesha.. sisi sio wasomaji wapitaji wengine humu.. tunajua kukumbuka.. basi tu nilikupima.. ukapimika.. uongooo eeeh
 
Umekosea.
Itakuwa hunijui vema. Endelea kunifuatilia utanifahamu uzuri
sekunde tu.. na umafia wangu.. nimeamua kukucheki


 
Mengine huwa ni prompted ideas tu kulingana na mada na nyakati. Hazina ukweli wowote. Kama ukiweza kufukua makaburi sehemu mbalimbali ndo utajua kwann naitwa Sexless. Wengi, ikiwemo wewe, wanapata taabu sana kunielewa, na hawatanielewa
 
Hiyo hoja yako haina mashiko, kwani JPM ni mara ya kwanza kwenda Chato, hivi umeona shughuli anazofanya kule akiwa amezungukwa na watu mbali mbali wakiwemo mawaziri wake waliotoka sehemu mbambali za nchi na nje ya nchi? Hivi kwa mazingira hayo kweli unaweza sema amekimbia korona Dodoma na kujicha Chato? Katika mazingira hayo unadhani hawezi kuambukizwa korona kuliko wananchi wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…