Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

sikiliza wewee, chanjo ya mafua ipo na inatolewa kila mwaka kwenye nchi za wenzetu wenye miili rojo rojo. Chanjo ya Covid nayo ipo, inafanya kazi kuufundisha mwili namna ya kupambana na corona, aina hii ya chanjo inaitwa RNA vaccine ambayo hutumia njia inaitwa mRNA ( messenger RNA) kuzalisha kinga. Anachokifanya Magufuli japokua kinatucost roho za watu lakini ni sahihi, sisi hatuna uchumi wa kuwalipa watu wasipofanya kazi, marekani huko wana lockdown lakini wananchi wanapewa milioni moja kila mmoja ( dola 600 kila mmoja wa familia), huko uingereza kina rashford wameifanya serikali iwape watoto vyakula vya bure, sosi haya hatuyawezi, korona ni janga ila kwetu janga kubwa ni uchumi wetu wa dola bilioni 50. Kama tutauziwa kinga ya korona kwa bei wanayouziwa afrika kusini ya ~ dola 6 kwa dozi, tutatumia ~dola milioni 390 (~ shilingi bilioni 840) kwa dozi za watanzania wote. Bila msaada hizo hela hatuzipati. TRA wameambiwa wakusanye walau trilioni 2 kila mwezi kuanzia januari, tukifanya lockdown ndo kwaheri uchumi wetu
 
kitu pekee nachojiuliza mpaka sasa, kwa nini tanzania ambao hatuchukui tahadhari yoyote hatujadhurika sana kama wanaochukua tahadhari?
 
kitu pekee nachojiuliza mpaka sasa, kwa nini tanzania ambao hatuchukui tahadhari yoyote hatujadhurika sana kama wanaochukua tahadhari?
Tahadhari inapovhukuliwa inazaa Matatizo mengi.
Mfano lockdown inazaa kushuka kwa kinga, umasikini, msongo wa mawazo n.k

Barakoa huleta magonjwa ktk mfumo wa upumuaji n.k, n.k
 
Blah blah blah

Rais anachukua uamuzi ila nchi nzima ipo kinyume nae...

Ajifikirie mno....

Ana matatizo ya thinking
Siyo nchi nzima wako kinyume na uamuzi wa jpm. Mm pia ni mtanzania. Hao walio kinyume waache mihemko watoe suluhisho la korona kama wanalifahamu
 
Hii upuuzi mkubwa kuamini tamko la Rais
Kwani wewe wajibu wako wa kiagya
Hacha utoto asee
 
Brother

Jifikirieni sana yaani....

The whole country haiamini anachokisema JPM....

Ugonjwa hauna mjadala,solution ni kunawa,barakoa na distancing,thats it!

Unaongea nini wewe maiti ya JPM?
Mbona wazungu basi wanazidi kufa kwa maelefu pamoja na kuchukua hatua zote hizo?

Hakuna njia hata moja iliyofanikiwa kupunguza corona! Hakuna.
 
Ugonjwa hauna mjadala,solution ni kunawa,barakoa na distancing,thats it!
Mbona kama suluhisho lako limeondoa mambo mengine kama lockdown, kufunga makanisa, kufunga mashule, kuzuia sherehe, na kuzuia mazishi? Haya maigizo yakifanyika korona itaisha? Na maigizo haya mwisho wake lini? JPM is right!
 
Hakuna anayetaka Jpm afungie wat u,ila Tz siyo kisiwa......serikali kuwahamasisha wananchi wake mbinu za kujikinga siyo dhambi.......kama huna mtu wa karibu au ndugu aliyeugua huu ugonjwa huwezi kuelewa mkuu,ni ngumu sana
 
La msingi hapa ni kuwaambia wananchi ukweli ili wajue na kuchukua tahadhari. Malaria ipo na inaua kila siku lakini uwepo wake unajulikana na watu wote na njia za kujikinga zinajulikana. Wenye uwezo wa kuzingatia wanazingatia na kupata matokeo yake. Wasiozingatia nao matokeo wanayaona.
 
Hadi sasa siajajua wanaotaka Rais atangaze janga la corona, je lengo lao ni kitu gani? Sijaona hata mmoja anayetoa njia itakayowezesha kumaliza huu ugonjwa kwa asilimia 100.
Hakuna popote duniani ambapo umedhibitiwa 100%. Kinachofanyika ni kujaribu kupunguza kasi ya maambukizi. Mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa hilo ipo na zile zilizodharau na kuacha maambukizi yaongezeje kwa kasi ipo.
 
Wewe hufi? Hapo ulipo umejifungia kwa shemeji yako hujui huo ugali unaokula unapatikana vipi ndio maana akili yako yote inawaza kwamba rais akisema tujifungie ndani corona inaisha.
Nitakufa ila sitakufa kama mjinga! Kwahio akili zote umezipeleka kwenye tumbo, sio? Mitanzania sijui lini mtakua na akili. Ona sisi, kila siku tunapewa updates


 
Rais gani? Amefanya nn? Amefanikiwa kwa kiasi gani?
Swala la kufanikiwa au kutokufanikiwa ni lingine, suala la kwamba rais gani amefanya Nini kama hili nalo ni la kukueleza basi Tz mna tatizo
 
Mkuu unachokisema ni kweli kabsa by the way.

Ila kwa nchi kama zetu hizi ikifanya ivyo.

Watu watakfa kwa strees tu ya maisha akiugua tuu kdog hatajua tayar ni korona. So ni stress juu ya stress .
 
Nitakufa ila sitakufa kama mjinga! Kwahio akili zote umezipeleka kwenye tumbo, sio? Mitanzania sijui lini mtakua na akili. Ona sisi, kila siku tunapewa updates
Unapewa updates ndio corona inapungua?

Mbona mnakuwa wapumbavu?

Nikafikiri una kitu kinaonesha mmefanya corona kupungua, kumbe updates kuonesha jinsi waathirika wanavyoongezeka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…