Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?

Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?

Huu ni unyanyapaaji wa wanawake nashangaa sana kuona na wanawake wenyewe baadhi yao wanashabikia huyu binti kuondelewa haki yake through ‘character assassination’.

Wanawake watanzania wengi kwa tamaa sijui ndio kupenda kuchuna lipo wazi sio siri ila aina maana hiyo iwe sababu ya kubakwa pia.

Binafsi (true story) nakumbuka binamu yangu kabisa kama miaka 10 iliyopita (kipindi hiko akiwa na umri kama huo wa late 40’s) yeye anaishi London. Alikuwa anatupa story ya holiday kuna vibinti vimemlia sana hela yake vitoto hivyo hivyo vya early 20’s na kutoa mzigo havitaki.

Kuna siku akaviita nyumbani kwake akavinywesha pombe yeye mwenyewe sio mnywaji ugonjwa wake ni nyapu tu.

Baada ya kulewa vile vibinti anawashkaji zake manyanya walimpa sigara special akawasha yeye akawa anazuga tu anavuta moshi anatoa, vile vibinti vyenyewe vinavuta wamemaliza kuvuta sigara nusu saa wapo paralytic hawajitambui; akawafanya anavyojua mwenyewe.

Yeye hakuwa anaona kosa la matendo yake, bahati nzuri aliokuwa anatupa story wastaarabu tukamueleza hiyo ni rape asirudie hiyo michezo; akasema hiyo mbinu yeye alipewa na wenyeji.

Hayo mambo wanawake wanafanyiwa sana Tanzania na wengi wanakaa kimya kwa sababu hizi za kuonekana tamaa zao ndio zimewaponza.

Kuna rafiki yangu mwingine yeye ‘what’s up’ video zake ni ngono tu na connections za mastaa. Kuna siku kanitumia video hivyo hivyo binti wa miaka hiyo hiyo early 20’s amelewesha halafu madogo kama watatu wanapokezana.

Ni upumbavu hasa kwa mtoto wa kike kushabikia huyo binti kwa kumuita sijui ni malaya na nini na nini, hiyo ni rape.

Kwanini ampeleke bar kulewa, afanye mambo yake kwenye gari na binti baada ya kutoka hapo aende polisi ku-report.

It’s a rape na matusi kama haya ya kuwaita wanaofanyia hivyo malaya na maneno mengine ya hovyo yanafanya victim wengine wa matukio ya kubakwa wasijitokeze, ujinga zaidi wanawake kushabikia.

Asilimia kubwa ya wanaume wanaomtetea huyo mkuu wa mkoa the only justification na wao ni wabakaji wa kutumia kilevi In my opinion.
Unaenda hadi nyumbani kwa mtu?

Unakubali pombe,,,unaletewa unakunywa,,,bangi nazo zinakuja unavuta.

Halafu uje useme umebakwa?

Come on guys!
 
Unaenda hadi nyumbani kwa mtu?

Unakubali pombe,,,unaletewa unakunywa,,,bangi nazo zinakuja unavuta.

Halafu uje useme umebakwa?

Come on guys!
Unapomwingilia mwanamke ambae kapoteza fahamu kwa sababu ya ulevi, akienda ku-report polisi huo ni ubakaji.

Mwanamke kuingia ghetto lako aina maana una haki ya kumbaka pia, hata kama alikuja kukupa mzigo kubadili mawazo ni uamuzi wake pia.

Halafu sigara special sio bangi, nenda manyanya uvute embassy yao ya mateja.
 
Mwisho wanaume tuwe makini sana na hawa viumbe, huyu binti kaangusha ndoto za watu wawili kwa kumpa mmoja miaka 30 jela na kumchafua mwingine kwa tuhuma ambazo zitamfuata maisha yake yote. Weekend njema.
Broo tuko makini maana saivi izi kesi mara zakupigwa kisu,mara rungu na kuwekewa sumu,na kuskumwa ndani zimenipa namna mpya ya kuishi na ivi viumbe na ni pale nilipoanza kufuatilia haya matukio nikagundua kwamba wanaume wa Sasa tumejisahau sana , solution ni kubadili mbinu na kanuni za maisha
 
Back
Top Bottom