Simu gani ina kamera bora kwa bei nafuu?

Simu gani ina kamera bora kwa bei nafuu?

Hii sio kweli kabisa.... Ni simu ya hovyo kwenye nini?

Ninatumia Samsung kwa muda mrefu ila kwa pixel huu ni mwaka wa 2 navutiwa kununua matoleo ya juu zaidi.

Mnawadanganya sana watu humu mitandaoni.
Ili nifaidike na Nini wakati mi mwenyewe natumia Gpixel4xl
 
Ili nifaidike na Nini wakati mi mwenyewe natumia Gpixel4xl
kwa akili yako fupi matatizo yaliyo kwenye hiyo simu yako Gpixel4xl ndio yatakuwa kwenye simu zooote za pixel...hivi unajua simu za Google pixel zina matoleo mangapi mbona zina matoleo mengi tofauti sasa ww na ki pixel chako kimoja hata haijulikani unaitunza vp au unatumiaje pia hatujui hio simu yako ya pixel mbovu ni used,refurbished au brand new..sasa yanini unahukumu simu zote za pixel kisa kisimu chako kimoja kinasumbua kwako basi ndio matoleo yote tofauti ya pixel hayafai..huna maana boya tu
 
Google pixel inajitahidi kwenye pic ila kusema haina mpinzani ni uongo. I phones na Samsung zinafanya vyema inategemea na budget Yako.
Mf. Iphone 6 niliwahi kushoot clips za wedding usiku ukumbini M hall Arusha (ukumbi una lights nzuri) videos ni amazing sana. Hivyo kwa kuanza unaweza tumia I phone 7, Google pixel, Sony pia zinajitahidi sana. Kwa video iphone lineup kuanzia 8 nakuendelea ziko safi sana.
 
Nunua google pixel kwa camera tuu
Ila kaka unataka camera na performance nenda na samsung pamoja na iPhone

Kuhusu bei
Simu nzuri kwa pixel ni kuanzia 6a
Bei zake ni 450K hadi 480K kwa pixel nzuri
Ila hata hizi pixel 3, na 3a nazo ni nzuri bei yake zinaanzia 250K

Kwa muongozo zaidi unaweza ni check
 
Ndo utueleze, ni simu ya hovyo kwenye nini ukitofautisha na zingine?
Google pixel tatizo lake kubwa hazikai na chaji pili zinazima ovyo yaani pixel kufa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nyingi ni used na zina short term software update huwezi kuzitumia kwa muda mrefu. Zinakufa sana kioo na bei ya kio chake ni sawa na bei ya simu.
 
Nunua google pixel kwa camera tuu
Ila kaka unataka camera na performance nenda na samsung pamoja na iPhone

Kuhusu bei
Simu nzuri kwa pixel ni kuanzia 6a
Bei zake ni 450K hadi 480K kwa pixel nzuri
Ila hata hizi pixel 3, na 3a nazo ni nzuri bei yake zinaanzia 250K

Kwa muongozo zaidi unaweza ni check
6pro bei yake inaendaje mkuu
Na 7 pro
 
Back
Top Bottom