Nunua mpya Samsung A15 4G 4/128 bei yake 350,000 unapata. Faida zake:
1. Battery kubwa ya 5000 mAh muhimu kwa watu wazima na wa vijijini.
2. Samsung ina software updates nyingi hivyo haiwezi lag na kuwa outdated mapema kama hizo Infinix na Tecno.
3. Samsung ina stable software, camera inayodumu quality na reliability ya parts kama mic, speaker, etc.
4. Kioo kikubwa, three camera lenses kwa ajili ya "washamba" wa kijijini ambao huamini lenzi tatu "macho matatu" ni simu nzuri zaidi. Ukitoa zawadi zingatia mapokeo ya mpokeaji sio mtazamo wako.
5. Vifaa vya A series ni bei nafuu kuliko vya Note, Z na S series. Hasa screen bei inavumilika.
Ninahisi ni simu za wazazi. Usisahau kununua Samsung adapters za type C to C maana A series haziji na chaja, price about @13k. Pia nunua cover around @7k , protector ni @3k.