Simu mpya za iphone zagundulika kuwa na changamoto kubwa

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Simu za iPhone 15 & iPhone 15 pro ambazo zimeingizwa sokoni hivi karibuni zimelalamikiwa na baadhi ya watumiaji wake kuwa na msululu wa matatizo

Watumiaji wengi wa simu hizo toka kampuni kinara Duniani kwa utengenezaji wa simujanja wameeleza kuwa simu hizo mpya zina changamoto ya kutoa joto jingi kupita kiasi(zaidi ya sentigredi 46) hasa pale mtu anapocheza gemu kwa muda mrefu,pia simu hizo zimethibitika kuvunjika kirahisi sana tofauti na matoleo mengine ya nyuma.

Mpaka sasa bado haijawekwa wazi ni kipi kimefanya matoleo hayo mapya ya iPhone kuwa na changoto hizo kubwa ingawa kuna taarifa zisizo rasmi kuwa huenda matatizo hayo yatakuwa yamesanabishwa na materials ya titanium yaliyotumika katika utengenezaji wake

Katika kukabiliana na changamoto ya simu kutoa joto kupita kiasi(overheating),kampuni ya Apple wametoa sasisho(software update) ingawa watumiaji wengi wanahofia sasisho hilo litakwenda kupunguza nguvu ya processor
 
Wakati samsung note 7 inatoka na type C ilikumbana na janga zito,mpaka sasa bado haijafahamika hii tech ina athali kiasi gani.

Kuhusu joto pia bado haieleweki kama ni hii tech mpya ya type c.

Kimsingi ndio iphone ya kwanza kukumban na matatizo kutoka kwake kuliko yoyote,tutegemee na milipuko soon.
 
Yeah! Watu sio wajinga sasisho wanalotoa linaenda ku-optimize perfomance ya device ili software isiwe power angry..
 
Ukiachana na hiyo kuna mashindano kati iPhone 15 madr in china na ile made in India, wachina wakidai made in India ni za hivyo hadi wameanzisha how to identify a made in India iPhone😁
 
Mkuu nimenunua iphone mpya charger hamna mpaka sasa natafuta charger OG sipati.
 
Charger OG andaa 45k fika duka linaloeleweka.utapata fast charger nzuri tu.
Acha drama basi? Umenunua series gani?
Chaja mbona zimejaa madukani? Au shida maokoto? Maana bila 45k hupati chaja
Hakuna charger ya viwango stahiki. Labda taja ni duka gani, kuwa ya 45k hakuifanyi iwe ya uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…