Hivi humu ndani naomba nieleweshwe
NADHARIA ya kua
5G inatumia bundle kubwa kuzidi
4G, maanake naona hiki kitu watu wengi wanakiamini, mimi akili yangu imegoma kuamini.
How????????
Yaani una file la
10Mb, ukili download kwa
4G litatumia data chache mfano hio hio
10Mb,
Na ukili download kwa
5G litatumia data zaidi mfano
15Mb?, Logic iko wapi hapaa?
Nijuavyo
4G & 5G it's just Internet Speed,
i.e how fast your going to download/stream e.t.c file/content at a given time...
Labda iwe hivi...
Kwanza achana kabisa na file la ku download, hapo sijui utumie technolojia gani kunielewesha..
Twende kwenye streaming hapa unaweza ukanishawishi.
KIVIPI??
Ukiwa unaangalia lets say Movie Neflix au YouTube mfano katika resolution ya
1920×1080(FULL HD) kwa kutumia speed ambayo inacheza, yaani kuna mda inakua
4G mda mwingine
3G/H+, hizo sites zina sifa za ku detect data speed yako na ku adjust resolution ya Movie yako, mfano kutoka kwenye
1920×1080(FHD) kwenda kwenye
1280×720(HD), ili angalau kukusaidia movie isisimame kabisa, ndio maana mda mwingine unaona inakuja na ukungu ukungu na ku stack, labda data zikishuka sana ndio itasimama kabisa.
Kwahio basi, matumizi ya data yanapanda na kushuka kulingana na Connection yako, (Naamini as long umeweza ku login Jf unajua, Resolution = Data kubwa, and vice versa).
Lakini ukiwa katika Connection iliyoko JUU na ipo STABLE (mfano hio
5G sasa) Video yako yote utaiangalia katika resolution ya
FHD, na hapo ndipo matumizi ya data yataonekana makubwa..
Kwa hilo ndio nitakubali Hoja yenu, otherwise mnipe nisichokijua.
Chief-Mkwawa .