Simuelewi Mzazi mwenzangu, tumeachana lakini bado anasumbua


Wewe nae umemkazia sana mwanatu!
 
Ni mshenzi halafu looser. Kaa makini naye.
 
Mwanaume akikuoa ukiwa na ujauzito wa mtu mwingine, Jitahidi siku ya Valentine day umtengenezee bango la shukrani. Maana kati ya wanaume 100 unaweza ukampata mmoja tu anaeweza kumudu kuishi na mke wa hivi.

Nakushauri upunguze mawasiliano na huyo mzazi mwenzako maana huyo ndio atakaekuja kukuharibia ndoa yako. Vinginevyo mruhusu mwanao akaishi na Baba yake ili uwe huru.
 
Ongea na mume wako kuhusu usumbufu unaopata kutoka kwa huyo mbuzi wako,
Ikiwezekana muombe mumeo ndio awe kiunganishi kati ya huyo mbuzi wako na mtoto wako, yaani baba watoto akitaka kuongea au kujua lolote kuhusu mwanae ampigie mumeo sio wewe.
 
Mtumie picha unampa mabusu mumeo, ajinyonge [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nakuhakikishia mbuzi akijiongeza kidogo tu akawa anatuma na ya kutolea haitachukua muda mama mbuzi atatoa mzigo.
Kupasha kiporo hapo ni suala la muda tu, maelezo ya mama mbuzi yanaonesha hana chuki kabisa na mbuzi ila ana hasira akikumbuka jinsi mbuzi alivyomfanyia.
Siku hasira zake zikiisha ndio siku kiporo kitaanza kupashwa.
 
Nadhan nitakua kichaa kama nafurahia matendo yake alafu nije tena kulalamika huku

Unafurahia hayo matendo yake bila shaka yoyote ile. Ungekuwa hufurahii, basi usingewasiliana naye kwa siri na kuulizana habari za mtoto na za huyo Mr. wako.

Kata mara moja mawasiliano na huyo mbuzi wako kabla mambo hayaja haribika.
 
inahusu nini sasa hapa
 
Kama unaipenda Ndoa yako achana nae Mara Moja laa sivyo ataishia kukukaza au Mumeo atakuacha kwa Kudhani labda Unatembea na Mzazi mwenzio, na Hii ndo Sababu baadhi yetu hatupendi kuoa wanawake ambao washazaa maana Hamjielewagi, Jitu limekuacha katika mazingira mabuvu leo hii anakupigia sim asee! Mlango ambao umeufungua Matokeo yake sio Mazuri, Trust me labda Mumeo awe hana sauti kwako ila Kama kichwa kinafanya kazi sawasawa basi Subiri Kuharibiwa ndoa yako

Najua Unajisemea Hatufanyi kitu, Ila msimamo wako wa Mwanzo Ulikuwa mzuri sana "Mtoto akimaliza shule utamchukua" very logical ila Sasa Umelegeza moyo Unajiona Ume win [emoji1787][emoji1787][emoji1787] My friend hujui akili zetu vizuri sasa shauri yako, Huyo mwenzako anataka akuharibie ndo maana Maongezi yenu sio ya Mtoto tena, Anaumia kukuona una maisha, Anaumia huyo, anateseka sana huyo achana nae japo najua ni ngumu kuelewa maana Viumbe nyie wengi wengi hamuelewagi kitu

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Mlime block mbuzi huyo!!!!

Umfungulie mtoto akifika 18

Kwanza haudumii mtoto guts za kukupigia simu anatoa wapi
 
Umeishamzalia mime wako?
 
Huyo jamaa ni fala....na usimuendekeze hata kidogo atakuvunjia ndoa. Mfanye ajute maisha yake yote kwa kumpiga block kila kona...au jifunze matusi ya nguoni akikugusa aambulie matusi mapya mapya afe kwa stress
πŸ˜¬πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Msimamo ni muhimu Sana katika Hilo unalolipitia.

Huyo mbuzi Hana tofauti na mchawi.
 
Haya mama Mbuzi tumekusikia, fikisheni salamu kwa mr. Mbuzi ache kusumbua kisa mbuzi yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…