Simulizi: Ajira Toka Kuzimu

Simulizi: Ajira Toka Kuzimu

SEHEMU YA 53



Kichwani akiwaza kumiliki laki tano upesi upesi!!!
Mlango ukafungwa!! Tembo akajipekua na kutoa kitita!!
“Hebu zihesabu hizi ni ngapi..”
Brenda akapokea….. akajikita katika kuhesabu. Hili lilikuwa kosa la jinai….
Zile pesa badala ya kunukia kibenkibenki zikawa zinatoa harufu ya marashi ya Mamamia.
Matamanio ya kuwa na Mamamia yakaanza kumpanda Brenda. Akajaribu kujizuia lakini hakuweza… mwishowe akakoma kuzihesabu zile pesa.
Tembo akafanya tabasamu lake kama kawaida kisha akatumia fursa ile kutimiza kile alichokipanga katika kichwa chake!!
“Brenda….” Akamuita kwa sauti yenye kitetemeshi cha amri fulani hivi. Brenda akamkazia macho tu.
“Una maamuzi ya aina mbili hadi sasa…. Wewe kwanza na kisha dada yako…”
Brenda akashtuka kusikia vile.
“Maamuzi gani tena jamani…..”
“Kuna mtu aliwapiga picha tena sio picha moja ni picha nyingi tu…”
“Picha? Picha gani?”
“Brenda… hujui kuhusu picha tena…. Si picha wewe na dada yako….”
“Ndio mimi na dada thatha picha dhipi….”
“Mkiwa mnafanya mapenzi…” Tembo akajibu!!
Hamu zote zikamwisha Brenda ghafla…. Akatamani kujizika lakini hakuweza. Akatumbua macho..
Tembo akatoa kile kicheko chake lakini safari hii hakikumvutia Brenda…
“Nani amekwambia Hathani eeh nani? Na alitupiga picha nani?” alihoji Brenda huku hofu ikionekana wazi machoni pake.
“Mi mwenyewe sijui hata nimeziona kuna mtu anazo nikaziiba….”
“Zipo wapi kaka..”
“Unataka kuona mlivyokuwa uchi mmekumbatiana..” maneno yalimtoka Tembo asijue ni wapi ameyapata…. Hakujua yu katika ulimwengu gani.
Brenda alichoka!!
 
SEHEMU YA 54


“Lakini hilo bado sio tatizo…. Tunaweza kulimaliza iwapo tutashirikiana….”
“Kiaje thatha na wakati kuna picha tumepigwa..eeh aibu hii jamani weeee!!”
“Picha ninazo mimi….. mmoja kati yenu anatakiwa kuzifuata mahali…”
“Kama unazo hapa naziomba Hathani ama hata kama ni kwako twende..”
“Ni picha za kikubwa sana anatakiwa kuzifuata mkubwa … kwani wewe na Mamamia nani mkubwa?”
Brenda akashusha pumzi ndefu kabla ya kujibu kwa sauti iliyokata tamaa “MAMAMIA”
“Basi ni yeye anayetakiwa kuzifuata….” Tembo alijibu huku akitabasamu.
“Mh! Mamamia alikukaba aisee.. ila na wewe ni balaa yaani mwee! Ulimpagawisha hadi akapoteza fahamu. Doh! Hata mpiga picha naye alikuwa jasiri looh!” Tembo alijisemesha maneno yaliyomkera sana Brenda akajihisi kuabishwa sana na ilikuwa ni sawa na kuvuliwa nguo hadharani.
“Hathani nitakupa chochote utakachotaka tafadhali kama kweli unadho hizo picha nipatie nami nikupatie chochote….” Brenda akajaribu karata yake ya mwisho.
“Ni kweli BreBre nitakupatia iwapo tu utanipatia Mamamia….. hata hivyo kwa leo bado na wewe itabidi tu nikuondoe hofu..”
“Uniondoe hofu? Kiaje labda….”
“Sitahitaji pesa zozote kutoka kwenu kwa sababu hamuwezi kunipa nikitaka. Namuhitaji Mamamia azifuate picha zenu… ahaa kuhusu hofu ngoja nije nikunong’oneze …” Tembo akamsogelea Brenda… Brenda akamzuia kwa mikono yake.
“Hutaki kujua ama unataka kujua…” Tembo akahoji kibabe… Brenda akawa mdogo akamruhusu Tembo amnong’oneze.
Hili lilikuwa kosa la jinai!!!
“Sitawaaibisha iwapo mtatii nitakachoomba!!” alinong’ona Tembo katika sikio la Brenda.
He! Sasa hiki nd’o cha kuninong’onedha!!! Alijiuliza Brenda huku akipigwa na butwaa!!
Wakati huohuo kidole chake kimoja kikijaribu kulikuna sikio lake, lakini huu mkono wa kidole haukutosha labda… Brenda akazidi kujikuna…..
Huo muwasho haukuwa wa kawaida, ulikuwa ule muwasho ambao hukunwa na ulimi wa Mamamia wawapo wawili….. sasa muwasho sikioni umekuja akiwa peke yake?? No! hakuwa peke yake… mbele yake alikuwa ni Tembo.
“Mimi nataka kwenda Hathani, sijisikii vizuri…” Brenda akamuaga Tembo huku akijaribu kusimama…. Lakini hakuweza miguu haikuwa na nguvu na alitambua haswa kuwa alikuwa anamuhitaji Mamamia eneo lile.
Tembo hakulaza damu!!
Brenda alikuwa anahofia kuaibika njia nzima atakayokuwa anatembea kwenda nyumbani…. Alipojitambua kuwa ana hofu… ni hapo akakumbuka kuwa Tembo aliahidi kumtoa Hofu….
Naam!! Ilikuwa kama alivyodhani… Tembo akamdama na kutumbukiza ulimi katika sikio lile lililokuwa linawasha!!
Ebwana eeh!! Brenda akatokwa na yowe kubwa… upesi Tembo akaiendea luninga akawasha na kuweka sauti ya juu kabisa.
Yaliyoendelea yakabaki kuwa siri yao!!
Lakini Tembo alimtoa hofu Brenda kwa asilimia zote!!
Lakini huu ukawa mwanzo wa mkasa!!
 
SEHEMU YA 55


Brenda akiwa njiani kurudi nyumbani akawa anapima ladha ya tembo na ile ya Mamamia….. ladha ya Tembo ilikuwa baabkubwa zaidi. Lakini huyu Tembo anahitaji Mamamia nd’o afuate zile picha….
Wivu!! Wivu ukamwandama Brenda ambaye alihitaji kuipata tena ile ladha ya kipekee… ladha ya Mnyama mkubwa!!!
Tembo!!
Akafikiria namna gani anaweza kumuhujumu Mamamia ili huyo wa kuitwa Hassan Tembo aweze kuwa mpenzi wake moja kwa moja.
“Kwandha akiwa mpendhi wangu na hidho picha atadhichachana!!” Brenda alijisemea huku akitabasamu na kujipa matumaini yote kuwa ataibuka mshindi katika hili.
****
MAMAMIA alijiona mjinga baada ya kutokwa machozi kwa muda mrefu.
Hakika, kilio hakikuwa tiba juu ya haya ambayo alikuwa ameelezwa na mdogo wake juu ya picha za uchi zinazoshikiliwa na Hassan.
Alipomkumbuka Hassan Tembo na kiumbo chake kidogo akajisikia aibu kujishusha kwake na kufuata maelekezo juu ya picha hizo. Lakini angefanya nini iwapo picha zingesambaa na heshima yake kuporomoka.
MAMAMIA akaamua rasmi kulipigania suala hili kabla halijafika pabaya. Akachukua namba ya simu ya Tembo na kumpigia kwa ajili ya mazungumzo.
Akategemea kuwa Tembo atamwomba penzi!!
Haikuwa hivyo, badala yake akapewa miadi ya kukutana sehemu ya wazi kabisa kwa ajili ya kuchukua zile picha kama kweli zipo!!
Mamamia akiwa anajijaza imani kali kuwa Tembo akiwa mwanaume kama wanaume wengine atauingia mkenge na kutamanika kingono. Akaamua kumvalia mavazi ambayo moja kati ya wanaume mia moja anaweza kukwepa kutamanika. Brenda akajisikia vibaya sana kumwona dada yake akiwa amevaa vile.. aliamini kwa kila namna Tembo ataingia mkenge!!
Roho ilimuuma!!!
SIKU IKAFIKA!!!!
MAENEO ya Mbezi ya Kimara kwa Msuguli. Mamamia akiwa ameegesha gari yake mahali na Tembo naye akiwa ameegesha GX 100 yake. Wote walikuwa wakitazamana baada ya Tembo kumweleza Mamamia juu ya nini kinatakiwa ili azipate zile picha….
Mamamia hakuamini kabisa kama kweli yawezekana sharti likawa dogo kiasi kile!
Yaani kumsindikiza tu hadi nyumbani kwake na hata ndani siingii!!
Jambo jepesi sana. Mamamia akakubali, Tembo akatabasamu kisha akaingia garini na kuanza kuongoza njia kuelekea bagala. Mamamia akifuata kwa nyuma.
**BRENDA anahitaji Tembo awe mpenzi wake jumla…
**MAMAMIA anaelekea mahali asipopajua…..
ITAENDELEA!!!
 
CHAGUA SIMULIZI IPI TUANZE NAYO.

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - NYEMO CHILONGANI ~ Simulizi ya Kusisimua
......(Kura 0/10)

DEAD LOVE ( PENZI LILILOKUFA ) - AZIZ HASHIM ~ Simulizi ya Maisha.
.....(Kura 0/10)

MIKONONI MWA NUNDA - BEN R. MTOBWA ~ Simulizi ya Kijasusi
......(Kura 3/10)

OOH!! KUMBE TAMU - YONA FUNDI ~ Simulizi ya Mapenzi.
.....(Kura 0/10)

Simulizi yenye kura 10. itatumwa, kura hazijafika 10 msimu wa pili utaishia hapa
 
SEHEMU YA 56


*****
WALIIFIKIA nyumba ambayo Tembo alikuwa anaishi, Mamamia akamtazama Tembo na kujisikia vibaya sana. Tembo alikuwa mfupi kuliko yeye…… katika maisha yake aliwahi kuapa kuwa kamwe hatakuja kuingia katika mahusiano aidha na mwanaume ambaye amemzidi umri ama ambaye yeye amemzidi urefu.
Sasa yupo na Tembo na anahisi amemzidi vitu vyote hivyo, umri na urefu!!
Aibu gani hii!! Kiapo kikayeyuka. Sasa tembo alikuwa na sauti, akisema twende ni kwenda akisema hakuna ni hakuna!! Na sasa wameifikia nyumba ya Tembo. Amri ikatolewa.
Ingia ndani!!
Mamamia Mango hakuwa na ujanja. Akaingia ndani lakini kichwani akikumbuka mipango yake vyema iwapo Tembo atahitaji kufanya naye mapenziu. Na bila shaka ni hilo lilikuwa linafuata maana mwanaume kumwingiza msichanan chumbani kwake bila sababu kuu usikuusiku ni kukaribisha majaribu.
Mamamia akaficha ghadhabu yake yote juu ya Tembo, akajifanya kutabasamu kila dakika huku akijifanya kuifurahia hali ya mle ndani.
Awali alidhani huenda Tembo ni kakijana tu kazugaji hakana hili wala lile ila zile picha tu nd’o zinampa kiburi.
“Hata hapa sio kwake wala nini!!” Mamamia akajisemea katika nafsi yake akiamini kuwa Tembo hana uwezo wa kuishi nyumba kubwa kama ile peke yake. Lakini hakuwa Tembo aliyempa jibu, macho yake yakakutana na picha ya Tembo ukutani. Picha kubwa kabisa iliyopachikwa imara ukutani.
“Mh! Ananizuga huyu ameachiwa tu geto na wenyewe!!” bado Mamamia hakutaka kuamini moja kwa moja kuwa Tembo ana mafanikio makubwa vile kumzidi yeye.
Alipogeuza macho kutoka katika ile picha akaanza kuzithaminisha samani za mle ndani, runinga bapa kubwa ilisheheni ukutani, sofa za bei ghali, zulia zito haswa, akazidi kuangaza zaidi na zaidi na mwishowe akakiri kuwa kama kweli Tembo anaimiliki nyumba ile basi heshima kwake.
Mamamia akaanza kusahau kama alisema kuwa ka-Tembo ni kaqfupi na kadogodogo hakamfai. Wazo jipya likaibuka kichwani mwake. Akafikiria kumrubuni Tembo ili auingie mkenge kama kweli anazo zile picha basi ampatie ama azitie moto kwa heshima ya penzi.
 
SEHEMU YA 57


“Kwanza alikuwa ananitaka huyu tangu zamani…” Mamamia akajisemea huku akijiweka tayari kuingia kazini.
“Halafu mbona kama Napata hisia naye jamani…” alizidi kujiuliza…..
“Mamamia…karibu!!” hatimaye Tembo aliyekuwa ameingia chumbani alirejea na kumkaribisha Mamamia tena.
Ni wakati huo ambao Tembo hajajiandaa kufanya alichotaka kwa Mamamia likatokea jambo.
Mamamia akijua kabisa kuwa lile zulia ni zito sana akapiga hatua mbili mbele akijifanya kukosa umakini akajikwaa na kuanguka chini.
Yowe likamtoka!!
Tembo akagutuka na kutimua mbio. Akamfikia pale alipokuwa, akainama ili aweze kumsaidia.
Huyu sasa alikuwa Tembo halisi ambaye hayupo katika ajira!! Akamshika Mamamia.
Binti mkata viuno akatabasamu katika nafsi na kujipongeza juu ya mtego wake kunasa.
Akauvaa ujasiri na kisha akapitisha mikono yake yenye kucha ndefu kiasi, akamshika Tembo kidogo ya kiuno chake kisha akambinya kitaalamu, Tembo akaungana naye zuliani. Ili asiseme neno Mamamia hakutaka kumziba Tembo kwa kutumia mikono, majambazi ndo huziba watu kwa mikono.
Dawa ya moto ni moto na hata dawa ya mdomo ni mdomo!!
Mamamia akauwahi mdomo wa Tembo kwa kutumbukiza ulimi wake kule. Tembo aliyekuwa anahitaji kuzungumza akashangaa anabadili zoezi na kuanza kumung’unya ulimi ule aliotupiwa na Mamamia.
Mamamia hakuhitaji kupoteza walau pointi moja katika zoezi hili, mkono mmoja ukasafiri hadi katika masikio ya Tembo, kidole kidogo cha mwisho kikazama sikioni.
Sasa Mamamia alimwachia Tembo mdomo aweze kusema.
Kwedli alisema lakini alisema maneno yasiyoeleweka. Wakati anasema hayo Mamamia aliendelea na shughuli nyingine.
Baada ya dakika nne…..
Tembo alikuwa kama alivyozaliwa. Mnaya mkubwa kamba fedha kwa mara ya kwanza katika ajira yake anakutana na mwanamke wa maajabu!!
Mamamia!!!
 
SEHEMU YA 58


Wanaume ndo huwabeba wanawake na kuwapeleka chumbani!! Lakini Mamamia akaionyesha tofauti ambayo wengi hawaijui.
Akamnyanyua Tembo na kumweka mgongoni….. kama vile mtoto mdogo Tembo akiwa uchi wa mnyama akasalimu amri….
Mamamia akababia na kukipata chumba cha Tembo!!! Hakuwa na papara hata kidogo, shetani kapata mjanja wake!!
Badala ya kumrusha kitandani kisha na yeye kujirusha hapo jambo ambalo Tembo alilitegemea, Mamamia akamrusha Tembo kisha yeye akatoka nje mbiombio na baada ya sekunde kadhaa akarejea akiwa na chupa ya asali aliyoitoa sebuleni kwa Tembo.
Tembo hajui hili wala lile akapigwa bao jingine la kisigino!!
Mamamia akamwagia asali kiasi mgongoni kisha akaanza kuilamba akiitapoakaza huku na kule. Nani wa kujali kuwa yale mashuka yanachafuka??
Hakuna hata mmoja!!!
Baada ya hapo Tembo akasafirishwa kwenda katika dunia nyingine. Ile ladha aliyokuwa anaiota siku nyingi sana sasa alikuwa anaipata hapa.
Kiuno kisichokuwa na mfupa!!!
Baada ya nusu saa Mamamia akiwa anampelekesha Tembo hatimaye alianza kumhoji maswali. Tembo akaanza kujibu kwa fujo hata ambayo hajaulizwa…..
Hakujua kama anajibu ama hajibu!!
Mamamia hakujali akaendelea na yake!!
Baada ya saa moja na nusu!!! Tembo alikuwa hoi kivyake na Mamamia hoi kivyake.
Walikuwa wamesinzia!!!
Majira ya saa nane usiku Tembo anakurupuka usingizini anamwamsha Mamamia na kumweleza jambo moja zito.
“Nakupenda Mamamia!!!” ajabu na kweli!!!!
Mamamia akatabasamu kisha akambusu Tembo midomoni, halafu wakajifunika shuka tena ikawa zu ya kitanda kuhangaika kwa mara nyingine.
Awamu ya pili tena Mamamia akawa mshindi. Kuhusu picha Tembo akamweleza Mia kuwa hazikuwepo na asitarajie madhara yoyote yale.
Kwa shughuli aliyofanya usiku uliopita Mamamia alitarajia ushindi tu….
Na kweli ulikuwa ushindi, lakini ushindi ulioleta balaa.
****
 
SEHEMU YA 59


BRENDA alikuwa akiumiza kichwa chake na kujiuliza anaanza vipi kuingia katika milki ya Tembo, akajiuliza dada yake naye akifanya mapenzi na kijana yule itakuwaje kama akinogewa?
Usiku ulizidi kwenda hadi kunakuchwa bado Mamamia alikuwa hajarudi. Wivu ukamshambulia sana Brenda lakini hakuwa na namna akajiapiza kuwa iwapo Tembo atawapatia hizo picha basi huo nd’o utakuwa wakati muafaka wa kumrubuni Tembo hadi awe mpenzi wake wa kudumu.
Hakujua kama Mamamia naye alikuwa na mawazo kama yake. Majira ya saa tano asubuhi Mamamia alirejea nyumbani akiwa na furaha tele!!
Akamweleza Brenda kuwa picha zilikuwa kwenye kompyuta na zote wamezifuta!!
Brenda akafurahia huku akijiahidi kumsaka Tembo kwa hali na mali.
****
TEMBO hakujua kama anaishi kwa kanuni, kanuni ambazo hazikuandikwa mahali zaidi ya ndoto ile ya siku ya kwanza kuingia katika ulimwengu huu wa mauzauza. Tembo alikuwa anajiuliza sana ni kwanini akishafanya zinaa na msichana mmoja hataki wala hajisikii tena kufanya naye kwa mara nyingine.
Hakujua kama hiyo nd’o ajira!!
Lakini kwa Mamamia ilikuwa tofauti, usiku ule ulikuwa wa maajabu sana…. Akautamani ujitokeze tena.
Clara, Lucy Kezi, Maria, Rehema, Brenda na wengineo wengi hakuwahi kuwaza kuzini nao tena….. lakini ladha ya Mamamia akaitamani tena.
Baada ya juma moja akaamua kumtafuta….
Wakapanga kukutana nyumba za kulala wageni!!
Mamamia akakubaliana na Tembo, wakati huo wakiitana ‘mpenzi’.
“Yaani ikiwezekana mi namuoa huyuhuyu kwani nini….” Tembo alijisemea siku hiyo. Na akatarajia kusema na Mamamia juu ya jambo hilo la ndoa.
“Mh….ile asali ile…. Mh! Ule ulimi looh na vile viuno walah simwachii hivihivi yule mi naweka ndani, kwanza ninaishi nyumba kubwa nina pesa…. Yaani naona ndoa ileeee watu Temboooo Temboooo!!!” Hassan Tembo alikuwa anazungumza peke yake katika gari….
Alichukulia wepesi jambo lile lakini hakujua ugumu wake!!!
Na labda ule ukawa usiku ambao hakutaka kuusahau kamwe!!!
NINI KILIJIRI……
ITAENDELEA….
 
SEHEMU YA 60

TEMBO hakujua kama anaishi kwa kanuni, kanuni ambazo hazikuandikwa mahali zaidi ya ndoto ile ya siku ya kwanza kuingia katika ulimwengu huu wa mauzauza. Tembo alikuwa anajiuliza sana ni kwanini akishafanya zinaa na msichana mmoja hataki wala hajisikii tena kufanya naye kwa mara nyingine.
Hakujua kama hiyo nd’o ajira!!
Lakini kwa Mamamia ilikuwa tofauti, usiku ule ulikuwa wa maajabu sana…. Akautamani ujitokeze tena.
Clara, Lucy Kezi, Maria, Rehema, Brenda na wengineo wengi hakuwahi kuwaza kuzini nao tena….. lakini ladha ya Mamamia akaitamani tena.
Baada ya juma moja akaamua kumtafuta….
Wakapanga kukutana nyumba za kulala wageni!!
Mamamia akakubaliana na Tembo, wakati huo wakiitana ‘mpenzi’.
“Yaani ikiwezekana mi namuoa huyuhuyu kwani nini….” Tembo alijisemea siku hiyo. Na akatarajia kusema na Mamamia juu ya jambo hilo la ndoa.
Laiti kama angejua!!!
***
Hali ya hewa ilikuwa tulivu kmaiwavyosiku zote isiponyesha mvua jijini Dar es salaam. Hasahasa siku za mapumziko.
Gari dogo aina ya vits lilikuwa likatiza mitaa ya Mwenge huku gari jingine aina ya Gx 100 likivinjari mitaa ya Temeke kwa Azizi ally.
Magari yote mawili yalikuwa yanaelekea Kijitonyama. Hoteli yenye hadhi ya juu kiasi Fulani jijini Dar es salaam nd’o yalikuwa makutano ya gari hizi mbili.
Lakini chumba kilichokwenda kwa jina la Paris katika hoteli hiyo ndo alikuwa makutaniko ya miili miwili.
Mamamia Mango na Munyama Mukubwa Tembo.
Wawili hawa walizungumza kwenye simu kabla kila mmoja akaelezea namna alivyomkumbuka mwenzake na hatimaye wakaamua kukutana ili wafurahishane tena.
Majira ya saa kumi na mbili jioni, walikuwa nje ya hoteli ile wakipata mlo wa jioni, Tembo ambaye alikuwa amejaza pweza za kutosha tumboni alishushia na mchemsho wa samaki wakati Mamamia alijipigilia mchemsho safi wa kuku.
Kisha wakatelemshia chakula chao na mvinyo wa zabibu ya Dodoma!!
Naam ila mmoja akafurahi yeye na nafsi yake kutokana na chakula kile ambacho hautakosea ukiita mlo kamili.
Saa mbili usiku walikuwa chumbani!!
Tembo ambaye kama kawaida huwa hana papara alimtuliza Mamamia kabla hajaanza manjonjo yake.
“Mamamia….. nahitaji penzi letu lisiishie hewani kama wengine waliopita….” Kwa sauti nzito ya kiume Tembo alikoroma.
“Unamaana gani kwani?” alihoji yule binti ambaye kuanzia juu hadi chini jinsi alivyovalia halikuwepo la kumkosoa. Aliyapanga mavazi vyema na mwili nao ukayapokea.
“Namaanisha kuwa…. Nataka tuoane Mamamia… nayasema haya kutoka katika nafsi yangu.nitakuwa na amani sana hili likiwa kweli….” Alijieleza Tembo huku akiwa ameinama. Mamamia alijikuta anafungua kinywa chake asijue lolote la kujibu. Akataka kusema neno lakini akakwama.
Tembo akabaki kusikiliza mtazamo wa Mamamia…..
 
SEHEMU YA 61


“Mbona mapema sana Hasan.. mapema sana yaani dah!!”
“Unaishi kwako Mamamia nami naishi kwangu ni kiasi cha kubadili makazi tu we uhamie nyumbani kwangu…. Nani wa kukuzuia.. Brenda mkubwa yule sio mtoto mdogo… Mia.. please!!” alisihi Tembo. Sauti ikapenya na kumvuruga Mamamia. Akakosa msimamo thabiti, akaangukia kifuani mwa Tembo…..
Hapakuwa na haja ya kumalizia jibu nd’o lilikuwa lile kuwa na yeye Mia alikuwa tayari.
Wakataka kupongezana… pongezi kwa kufanya ngono!!
Hii ni kuanzisha vyema mahusiano yao……
Kama kawaida yake Mamamia kaanza makeke yake, hii ilikuwa zaidi ya siku ya kwanza.
Safari hii alijipanga zaidi!!!
Kipande cha ndimu, udi na madikodiko mengine.
Tembo akaingoja huduma ile ya maajabu, baada ya kuoga pamoja akalazwa chali binti akaanza uchawi wake wa kitandani. Mara amguse Tembo huku mara amguse kule. Miili ikigusana joto la aina yake linaleta msisimko.
HOFU!!
MAANDALIZI haya yalikuwa yanafurahisha awali, Mamamia alikuwa akimng’ata Tembo kichokozi na wakati mwingine zile kucha zikamtomasa huku na kule mwili wa Tembo ukapata burudani ya aina yake, burudani iliyomfanya kutangaza ndoa mapema.
Maandalizi haya yakabadilika ladha, Mamamia akaanza kung’ata kwa nguvu, Tembo aka anaumia lakini anajikaza akihisi ni bahati mbaya, mara akawa anafinywa kwa nguvu tena makucha yakawa yanampa suluba.
Hapa napo akajikaza lakini akijiuliza kulikoni hali inakuwa vile.
Mara Mamamia akaacha kufinya Tembo akapata unafuu, lakini likatokea jingine la kustaajabisha. Kile kipande cha ndimu ambacho Tembo alingoja kuijua kazi yake kikaminywa kwa fujo.
Tembo hakujua ni kitu gani kinaendelea mpaka pale alipofumbua macho na kuruhusu yale maji ya ndimu kumwingia machoni.
Hapa haukuwepo uvumilivu tena, Tembo akapiga mayowe makubwa sana. Akajirusha upande upande asijue ni wapi atakapotua.
Akajibamiza ukutani!!
Akayapikicha macho yake huku akimzuia Mamamia ambaye alikuwa akihaha huku na kule ili aweze kuminya maji zaidi machoni mwa Tembo.
Hatimaye jicho moja likafanikiwa kuona mbele!!! Mamamia alikuwa amevaa chupi yake aina ya bikini shingoni huku mkononi akiwa na kipande cha ndimu. Sura yake ilikuwa imetaharuki sana!!
“Mamamia… umekuwa…” kabla tembo hajamalizia kauli hii alishangaa kumwona Mamamia akiruka kando na kisha akaanza kuipekua suruali ya Tembo.
Humo akatoka na simu ya Hasan aina ya Samsung Gallaxy S4……. Wacha wee!! Tembo akajaribu kumzuia Mamamia asifanye lolote na ile simu. Lakini alikuwa amechelewa Mamamia akairusha simu ile kupitia dirishani.
 
SEHEMU YA 62


Kutoka ghorofa ya tano waliyokuwepo hadi kufika chini. Simu ikasafiri kwenda kukutana na ardhi.
“R.I.P my Phone…..” Tembo akajisemea kwa sauti ya chini.
“Mamamia matani mengine ujue sii mazuri…” sasa akajaribu kumkoromea Mamamia. Akategemea yule binti ataingiwa hofu lakini alijidanganya.
Hapohapo Mia akajirusha na makucha yake yakamparua kifuani Tembo aliyewahi kumkwepa.
Sasa hofu ikamwingia Tembo, jeuri yake ikaishia pale pale ambapo Mia alichukua suruali yake pamoja na shati. Akamshtua Tembo kama anamfuata vile… Tembo akakimbia uchi mle chumbani huku ule mkia wake uliokuwa wima wakati Mamamia akimlamba huku na kule ukiwa umelala chali.
Mia akaingia bafuni, Tembo alipopata ujasiri wa kumfuata alikuta nguo zake zikiwa katika tundu la choo!! Mamamia alikuwa anacheka sasa!!
“We Mamamia wewe….ujue sina nguo za kubadili” Tembo akaita, badala ya kujibiwa akapondwa na sabuni iliyokuwa mikononi mwa Mamamia. Akapiga mayowe huku akitoka nje!!! Mamamia hakumfuata… aliendelea kufanya mambo asiyojua kwanini anayafanya.

Tembo akahofia hali ile na kugundua kuna jambo ambalo haliendi sawa!!
Akachukua taulo akajifunga kiunoni!! Pekupeku akatoka nje huku akijiapiza kuwa akifika nje atatafuta namna ya kutoweka moja kwa moja.
Hatua mbili baada ya kuuacha mlango akakumbuka kuwa ndani ya mifuko ya suruali yake ndiyo kuna kadi ya benki na pesa zake nyingine, ataondoka vipi bila kuwa na pesa???? Hilo lilikuwa swali gumu sana ambalo jibu lake lilikuwa moja tu!! Kurudi ndani ya kile chumba cha Mamamia wa maajabu!!.
Upesi akarejea chumbani akipishana na mteja mwingine wa kike aliyebaki katika mshangao kwa hali aliyokuwa nayo Tembo.
Akanyata hadi mlango wa bafu, uoga ukaanza kumtawala baada ya kukuta bafuni hakuna mtu na zile nguo zake hazipo katika tundu la choo.
“Mamamia…. We mamamia….” Akaita kwa sauti ya chini.. lakini hakujibiwa. Akaangaza pande zote za chumba asione kitu chochote!!
Akaingia tena bafuni mzimamzima!! Mwili mzima ukiwa unatetemeka
Mara akasikia mchakato nyuma ya mlango wa bafu!! Ile anageuka ghafla akanaswa shingo yake akafurukuta lakini haikusaidia kitu, harufu ya mkojo ikamfanya ajaribu kutazama.
Ilikuwa suruali yake iliyokuwa imemkaba. Haikumkaba kimasihara. Ilikuwa inamnyonga kweli. Akajaribu kupiga makelele na kujirusha huku na kule bado hakuweza kuchomoka katika ile suruali.
Hatimaye akaachiwa ghafla akatua chini!!
Akakohoa sana kabla ya kugeuka na kutanabai kuwa Mamamia aikuwa amevaa lile shati alilolitoa katika mikojo na alikuwa anatabasamu.
“Ametoa wapi hizi nguvu huyu dada……” alijiuliza Tembo huku taulo ikiwa imemtoka kiunoni. Yeye na mkia wake wote walilalia marumaru ya bafu lile.
“Nisamehe…nisamehe Mamamia…” kwa uoga Tembo akajikuta akiomba msamaha bila kujua ni kwa kosa gani alilolifanya. Mamamia hakujibu kitu badala yake alimsogelea Tembo, kisha akamruka na kwenda zake chumbani.
Tembo akaipekua upesi na kwa tahadhari kubwa ile suruali. Akitegemea kuambulia walau kadi na pesa zake lakini haikuwa vile akaishia kukutana na maji maji tu ya chooni.
Zimeenda wapi sasa!!! Akajiuliza… mara akamsikia Mamamia anacheka peke yake. Tembo akaitupa mbali ile suruali kwa uoga. Akangonja labda Mamamia atatokea kule ndani lakini kimya kikatanda hakuna aliyetokea.
 
SEHEMU YA 63


Tembo akanyata na kuifikia tena suruali yake, akaweka kinyaa kando. Akaingiza mikono kila pande lakini hakuna kitu!!!
“Au huyu mwendawazimu amechukua… eeh Mungu nisaidie mimi…” Tembo akakumbuka kumwomba Mungu…. Na hapohapo akaendelea kuhaha akitafuta kadi ya benki na pesa zake.
Jitihada hazikuzaa matunda hakupata hata kitu kimoja!!
Akaokota taulo ambalo lilikuwa limelowana, akajifunga tena kiunoni. Akanyata hadi chumbani, akamkuta Mamamia akiwa amelala hoi kitandani. Tembo hakutaka kupoteza nafasi zaidi, alikuwa anamuhofia Mamamia na kile kiuno bila mfupa alichokuwa akikiwaza hakikuwa na maana tena…. Huku akiwa anatembelea vidole vya mbele kwa kunyata. Aliufikia mlango akaufungua na kutoka mkuku taulo kiunoni.

Mojamoja kwa moja hadi mpokezi kwa fujo zote akamkuta yule dada ambaye aliwapokea. Ile kukutanisha naye macho akakumbuka kuwa kuna pesa kadhaa waliziacha pale mapokezi.
“:Nipatie ile elfu nane dada…. Tafadhali naomba..”
Dada wa mapokezi alijikuta akimpatia pesa Tembo bila kuuliza chochote, lakini zaidi alikuwa anamshangaa nini kimemsibu hadi anatoka na taulo pekee kutokea ghorofa ya tano hadi mapokezi.
Muhudumu akadhani Tembo atarejea chumbani kwake, lakini haikuwa hivyo. Akaufungua mlango wa kutoka nje akatimua mbio vilevile na taulo lake kiunoni.
Bahati ikawa upande wake akakutana na dereva wa bajaji, Upesi akajirusha ndani ya bajaji. Mwendesha Bajaji akapiga yowe la hofu lakini Tembo akamtoa hofu kwa kumkabidhi pesa yote aliyokuwanayo mkononi..
“Nipeleke Kinondoni kaka… Kinondoni kwa Manyanya pale…..” huku akiwa ametaharuki alimwelekeza dereva.
“Kaka nini tena kwani…. Fumanizi ama……” dereva alihoji.
“Umenifumania wewe ama… hebu acha dharau kijana acha kabisa dharau nasema….” Tembo alikaripia. Dereva akawa mpole.
Akaondoa bajaji upesi!!
****
SALUM Mohamed nd’o aliyeibeba aibu ya Hassan Tembo ya siku hiyo. Tembo hakusema lolote lililotokea aliomba kupumzika kwanza hadi ifike asubuhi ndo anaweza kusema lolote. Salum akamuhifadhi kwa siri kubwa kama Tembo alivyohitaji.
KWELI asubuhi ikafika lakini ule muda wa kuelezana palikuwa na habari nyingine nzito zaidi. Habari iliyomvuruga Salum zaidi kabla hajamshirikisha Tembo. Salum alikuwa haeleweki eleweki, alikuwa amevurugwa haswa na Tembo hakujua kulikoni, na hata alipotulia na kumweleza Tembo vizuri, ikawa zamu ya Tembo kupagawa maradufu!!!
**Nini tena kimejiri asubuhi hiyo!!
**Nini hatma ya MAMAMIA ….
Bofya LIKE kama tupo sambamba… weka maoni yako pia!!
ITAENDELEA!!!!
 
SEHEMU YA 64


SALUM Mohamed nd’o aliyeibeba aibu ya Hassan Tembo ya siku hiyo. Tembo hakusema lolote lililotokea aliomba kupumzika kwanza hadi ifike asubuhi ndo anaweza kusema lolote. Salum akamuhifadhi kwa siri kubwa kama Tembo alivyohitaji.
KWELI asubuhi ikafika lakini ule muda wa kuelezana palikuwa na habari nyingine nzito zaidi. Habari iliyomvuruga Salum zaidi kabla hajamshirikisha Tembo. Lakini baada ya kumshirikisha Tembo akachanganyikiwa zaidi.
“Salum.. nipatie nguo zako kaka nijikongoje Mbagala geto aisee….” Tembo alimsihi Salum ambaye akili yake bado ilikuwa haijakaa sawa.
Tembo akajiongeza akaingia chumbani na kuchukua nguo za Salum.
Kituko kingine. Nguo zikamzidi mwili!!!
Akazivaa hivyohivyo!! Akakutana na shilingi elfu kumi mezani akaitwaa!!!
Akaondoka bila kuaga akimwacha Salum akiwa amevurugwa na taarifa aliyoipokea asubuhi hiyo kuwa Mamamia amerukwa akili na ametoka nyumba ya kulala wageni akiwa uchi wa mnyama. Mwanaume aliyekuwanaye hajulikani ni nani?
Salum alikuwa amemtaka kimapenzi Mamamia kwa muda mrefu sana bila mafanikio lakini aliposikia ameachana na aliyekuwa mpenzi wake akaamua kuanza upya mashambulizi.
Sasa anaambiwa Mamamia amekuwa kichaa!!!
***
Taarifa za Mamamia kupata wazimu hazikuyafikia masikio ya Brenda kwa upesi.
Hii ni baada ya kuwa na usiku mgumu kupita yote aliyowahi kuwanayo. Alihangaika kuutafuta usingizi kwa masaa kadhaa bila mafanikio. Alijaribu kulala kwenye sofa akajaribu kulala katika zulia bado hali ilikuwa ileile.
Hakujisumbua kujiuliza mara mbilimbili nini kilikuwa chanzo cha yote haya. Alijua hakika kuwa ni wivu ulikuwa unamsumbua, wivu dhidi ya dada yake mpenzi.
Naam!! Aliamini kuwa ukimya wake unasababishwa na penzi zito analolipata kwa munyama mukubwa kamba fedha Hassan Tembo.
 
SEHEMU YA 65


Majira ya saa tatu usiku alijaribu kupiga simu ya Mamamia, ikaita pasi na majibu, akajaribu kupiga simu ya Tembo ili kujihakikishia hii nayo haikuwa inapatikana.
Brenda kashindwa kuyazuia machozi yake!
Alikuwa analilia penzi la Tembo.
Kilio cha Brenda kilikosa maana pale alipokosa mtu wa kumbembeleza akaamua kuyafuta machozi na kuyakodoa macho yake kwenye kioo kikubwa kilichokuwa pale sebuleni, akajitazama vyema jinsi macho yake yalivyokuwa mekundu. Kisha akachukua kiti akakiweka jirani na ukuta akapanda na kubandua picha iliyokuwa ukutani. Halafu akarejea katika kioo.
Akaielekeza picha ile katika kioo na kuanza kujifananisha.
“Hata hanidhidi kwa lolote huyu…” Brenda akajisemea huku akijilinganisha yeye na ile picha ya dada yake ambaye hakuwepo wakati huo,.
“Yaani Tembo na ujanja wake wote ameona huyu nd’o mdhuri kushinda mimi ama…” akazidi kujiuliza. Kisha kwa hasira akaitupa chinbi ile picha.
Brenda akajiona mjinga kuendelea kubishana na picha, akachukua simu yake akatafuta namba aliyoifahamu yeye akabofya na kulipata jina alilokuwa anahitaji.
Akaipiga ile namba!
Alikuwa ni rafiki yake.
Wakazungumza kwa kirefu Brenda akazieleza hisia zake waziwazi juu ya Tembo akasema sana kwa huzuni.
“Kwa hiyo unataka tumfanye kama Lameck….” Rafiki yake Brenda alimuuliza Brenda. Kwa sekunde kadhaa Brenda akafikiria juu ya Lameck na kisha akakubaliana na rafiki yule.
“Asubuhi na mapema tukutane si unajua anavyokuwa na foleni ndefu yule…”
Brenda akakubali na kisha akakata simu!!
Sasa hakuwa anamuwaza Mamamia tena na kumwonea wivu, badala yake alikuwa akiwaza jinsi Tembo atakavyogeuzwa kuwa kama Lameck.
Lameck ni shemeji yake ambaye hana la kusema wala hawezi kukohoa lolote mbele ya rafiki yake huyo aliyempigia simu. Alipomuuliza siri ya mafanikio akamweleza kuwa watu kama hao lazima watengenezwe kwa wataalamu.
Sasa anataka kumtengeneza Tembo na yeye asiwe na la kusema wala kukohoa mbele yake.
“Yaani akishatengenedhwa thatha, nikitaka kwenda Mlimani thity namwambia ananipeleka mara moja, nikitaka kwenda kwake naenda muda ninaotaka, nikitaka aje kunichukua napiga thimu anakuja…. Mamamia atanunajeee!!” Brenda alijipa moyo huku akirusharusha miguu na mikono huku na kule, hatimaye akasinzia kichwani mwake akiamini kuwa wakati wa kumkera Mamamia umewadia!!!
Hakujua kuwa muda huo wawili hao anaowawaza walikuwa kwenye hekaheka za kutisha!!!
***
 
SEHEMU YA 66


Majira ya saa mbili asubuhi tayari Brenda na monica ambaye ni rafiki yake walikuwa katika kijumba cha mzee mwenye kipara, Monica kwa sababu alikuwa mzoefu alizungumza kwa niaba ya Brenda.
“Anaitwa nani huyo mtu wenu…”
“Hathani…” Brenda kithembe akajibu.
“Hathani… Hathani jina la mtu hilo…”
“Hamna sio Hathani ni Hathani…” Brenda akasababisha monica acheke kabla ya kumsaidia, “Anaitwa Hassan babu, huyu ana kithembe….”
“Hassan nani… kuna akina Hasan wengi duniani…”
“Tembo….” Akamalizia Brenda.
Yule mzee mwenye kipara akaanza kupiga makelele yake hapa na pale. Mara apulize hiki mara anuse kile na kisha akapiga chafya, mara acheke. Ilimradi tu varangati.
“Ohhh! Tuntu… Tuntu ndani ya jiji…. Tuntufyeeee!! Tuntu weeee..” mganga akaanza kuzungumza huku akitazama katika maji yaliyokuwa katika sufuria dogo.
“Ajira.. unasaka ajira wewe….mbona umeajiriwa tayari ama haujaridhika na kazi yako…” mganga akamuuliza Brenda.
“Hamna babu mi thitafuti ajira namtaka Tembo…” akajitetea Brenda. Monica naye akahisi mzee wake ameingia chaka kwa kubashiri uongo.
“Hakipo kingine unahitaji zaidi ya ajira binti, unaitafuta ajira ambayo unayo tayari….unamtaka Tembo….. unamtaka Tutufye Kanyenye… Tuntu!!” Mganga akawa kama anazungumza peke yake hivi.
“Ni kweli unamtaka Tembo!!!”
“Ndio babu…”
“Basi nenda ukamlete kamlete nijue namna ya kumsaidia, amemkosea Tuntu tayari na Tuntu hajui maana ya kusamehe…. Kamlete Tembo… maana kinyume na hapo atazua janga kubwa sana kwa waajiriwa wake, mmojawapo ni wewe… tena wewe wa hivi karibuni ndo mtaanziwa…” Mganga alizidi kuropoka.
“Huyu mzee wako vipi Monica eeeh!! Mara natafuta ajira mara nimeajiriwa, mara nimlete Tembo…. Mambo gani sasa haya jamani… naomba tuondoke kwa kweli…” Brenda akiwa amehamaki na kutangaza hasira zake nje nje alikuwa amesimama tayari.
Ghafla yule mganga akamdaka gauni lake akamvutia ndani kisha akambana vyema asiweze kutikisika. Wakati huu aliendelea kuzungumza lugha alizozifahamu yeye mwenyewe.
Baada ya Brenda kutulia, yule mganga alimfunua paja likabaki nje kisha akamnyunyuzia maji kutoka katika kibuyu. Kisha akamvuta kichwa chake akamuinamisha aweze kuona maajabu.
Brenda akisaidiana na Monica wakatazama kilichopo katika paja la Brenda. Ilikuwa ni alama mfano wa fuvu la kichwa. Brenda akapiga mayowe yule mganga akawahi kumziba mdomo.
“Hii nd’o ajira niliyokwambia…. Umeajiriwa na Tuntu kupitia kwa kibaraka wake aliye matatani.. Tembo!! Unatakiwa kumleta Tembo upesi kwangu na hapo ndipo utapata muafaka wa hili jambo, vinginevyo ndani ya siku mbili sio paja tu, mwili wako wote utakuwa uchi ukizurura huko mtaani.” Mganga sasa alikuwa amemuachia Brenda huru.
Brenda hakuwa na namna zaidi ya kufuata maelezo aliyopewa, ni hapa ambapo Monica aliamua kujiweka mbali naye!!
Urafiki wa kinafiki!!
****
 
SEHEMU YA 67


HABARI ya Mamamia kurukwa akili ilikuwa imemvuruga sana tembo. Kuna maswali alihitaji sana apatikane mtu wa kumjibu lakini bahati mbaya hakuwepo mtu huyo.
Yawezekana Mamamia huwa ana kichaa? Au ana majini? Au ni Malaria ilimpanda kichwani?
Hakupata jibu!! Akaamua kulichukulia jambo lililotokea kama bahati mbaya tu. Akanyanyuka na kwenda kuangalia uwezekano wa kutengeneza namba yake ya simu ambayo Mamamia aliitupilia mbali ikiwa katika simu yake.
Zoezi halikuchukua muda mrefu sana!! Akaipata namba yake, akachukua simu ya ziada iliyokuwa ndani akapachika ile kadi ya simu.
Tembo akarejea hewani!!
Baada ya pale akakumbuka gari yake aliyoiacha kule hotelini.
Naifuata vipi sasa wakati yule bwege sijui aliutupa wapi ufunguo, si nd’o mwanzo wa kushikwa uchawi wakasema nimemtupia msichana wa watu majini mimi Tembo nikaaibika!! Tembo alijisemea huku sasa akiwa muoga waziwazi tofauti na zamani.
“Hapa ngoja nimpigie Kithembe nimuulize” Tembo akaitwaa simu yake….
Shit! Namba ya Kithembe haikuwa katika simu yake, kila jina lilikuwa lilibaki katika simu yake iliyotupwa mbali na Mamamia.
Wakati Tembo akizidi kughafirika mara alianza kukerwa na sauti za watoto waliokuwa wakipiga kelele nyingi sana.
“Hapo washamkamata kikojozi basi leo hapakaliki hapa, yaani uswahilini bwana.. hapa nifanye nihame!!” Tembo alizungumza peke yake.
Zile kelele zikazidi kusogea karibu!! Tembo akaliendea dirisha lake ili aweze kumwona huyo kikojozi aliyeandamwa na wenzake!!
“Yaani vitoto bwana, unakuta na vingine hapo vinakojoa kitandani lakini vimeshupalia kumwimbia mwenzao duh!!” Tembo akacheka mwenyewe kisha akazikumbuka enzi alipokuwa mtoto, hata yeye alipenda kuwaandama watoto wanaokojoa kitandani.
Umati ukazidi kusogea na kelele zikazidi, Tembo katika dirisha lake akazidi kuhangaika ili amwone huyo kikojozi!!
Mh! Mbona kikojozi mwenyewe mkubwa hivi!! Tembo alijiuliza baada ya kumwona yule anayekimbizwa na watoto lukuki.
He! Halafu lipo kama uchi lile au ni nguo ile…. Au chizi jamani mbona hee!!..... maajabu…. Halafu.. halafu lile shati kama, kama shati langu vile au nalifananisha!!
Alipoimnalizia ile kauli yule aliyedhania kuwa ni kikojozi mkubwa sasa alikuwa anatazama mbele….
Tembo akaishiwa nguvu miguuni, akataka kukimbia lakini akajihisi amenasa!!
Jicho lilikuwa limemuona Mamamia Mango.. yule aliyemzulia tafrani nyumba ya kulala wageni huko walipokutana.
Sasa ana kundi la watoto zaidi ya mia moja… wanajongea katika nyumba yake.
Amevaa shati lake lilelile la siku ya tukio!!
Tembo akaanza kulia kama mtoto mdogo!! Mkojo ukaomba ruhusa kupenya Tembo akauzuia, mkojo ukalazimisha kupita……
**Ohooo! Mamamia na kundi la watoto amekuja kukinukisha Mbagala kwa Tembo… mbona balaa…
**Brenda naye hofu tupu ana fuvu pajani!!
ITAENDELEA …
**SIMULIZI HII HUKUJIA KILA BAADA YA SIKU MOJA!!!
 
SEHEMU YA 68

Nguvu zilizidi kumwishia Tembo huku akiiona aibu ikimfuata kwa kasi. Alikuwa na heshima kubwa sana pale mtaani kwao, mama yake mzazi pia alikuwa mtu maarufu hadi mtaa ukafikia kuitwa kwa Mama tembo!!
Sasa anakumbana na aibu ya mwaka!!
Tembo akakumbuka ule usemi wa heri nusu shari kuliko shari kamili.
Akajikongoja hadi mlango wa kutokea nyuma ya nyumba… mlango wa dharula ambao huwa unatumika mara moja moja sana!! Akaufungua na kutokea pande zile, upesi bila kutazama kushoto na kulia alijichanganya katika kundi la watu waliokuwa wakimshangaa Mamamia, akajipenyeza humo ili aweze kutoka kwa usalama.
Ile hali ya kuwa nje ya nyuma ile ambayo kwa namna yoyote ile Mamamia alikuwa amenuia kuingia… walau amani iliishi naye kidogo.
Kama mamamia ataamua kuvamia nyumba na yeye hayupo ndani ilikuwa njema zaidi kuliko yeye kufumaniwa ndani.
Kwanza akithubutu kufanya hivyo lazima watamshika na kumpiga ikiwezekana, hakuna hata mtu mmoja awezaye kumwamini mwendawazimu.
Tembo akajipa moyo kisha akajichanganya katika kundi la watu na kujiweka mbali kabisa na lile tukio.
Bado hakuwa na amani timilifu kwa sababu ya umaarufu wake pale mtaani akahofia huenda anaweza kutokea mtu akamuuliza kulikoni yule dada achague nyumba yake na kuweka kambi pale.
Upesi Hassan akakatiza mitaa kadhaa na kufikia nyumba fulani, akatabasamu baada ya kuona alichokuwa akikihitaji kilikuwepo.
Gari!!
Na mwenyewe ambaye ni rafiki yake naye alikuwepo. Hassan akamweleza juu juu huku akimdanganya kuwa gari yake imeharibika. Yule swahiba wake akakubali kumwazima gari yake.
Tembo akatokomea kuelekea kariakoo, alipoufikia mji akiwa hana kitu cha ziada cha kufanya akaamua kuingia msikiti ambao alikuwa akifahamiana na watu kadha wa kadha. Alifahamiana nao kwa sababu mara kwa mara alikuwa akitoa misaada kila inapotakikanika, hivyo alikuwa akiheshimika pia kama kijana mdogo lakini mwenye mambo makubwa!!
Siku hiyo akaamua kujituliza pale ili tifutifu la nyumbani kwake Mbagala liweze kupoa.
****
Kabla Brenda hajaondoka kwa mganga aliongezewa sharti jingine ambalo lingemwezesha kumrejesha Tembo ama akimkosa basi anaweza kupoteza uhai wake katika namna ya kusikitisha sana.
Mganga yule alizidi kumtisha Brenda na hatimaye akamshauri ayahamishie maswahibu hayo kwa kiumbe mwingine ili apate muda mzuri wa kumsaka Tembo na kumfikisha kwa mganga yule kwa ajili ya tiba.
Mganga akampa Brenda kioo na kisha kumshauri ataje jina lolote ili waweze kuangalia uwezekano wa kuhamisha maswahibu ambayo yangeweza kumkabili kwa sababu ya kuajiriwa na Tembo.
Brenda huku akitetemeka akaijiwa na jina kichwani… akalitaja!!
Mganga akacheka kicheko kifupi kisha akawaruhusu wawili wale kuondoka zao.
Brenda akaanza kuhaha akitafuta namna ya kumpata Tembo huku Monica akijitafutia visababu na kujiweka mbali.
****
 
Back
Top Bottom