Simulizi: Ajira Toka Kuzimu

Simulizi: Ajira Toka Kuzimu

SEHEMU YA 69



ASIA DIGITALI
Neno msikiti, lilimjia akilini mwake katika namna ya kushtukiza. Akafanya tabasamu pana na kujishangaa, imekuwaje hadi akauwaza msikiti ilihali hakuwa mtu wa swala tena.
Tabia zake mbovu za kuwalaghai wanaume na kuwaibia mali zao, leo hii anawaza msikiti.
“Au nd’o shetani kuzeeka anakuwa malaika…” Asia alijiuliza huku wazo la msikiti likiwa palepale. Na hapo ndipo alipokumbuka juu ya kijana wa kuitwa Hassan Tembo!!
Ni muda mrefu sana alikuwa ameelezwa sifa zake na uwezo wake kipesa.
Asia hakutaka kitu kingine cha ziada kwa mwanaume zaidi ya pesa. Hakujali juu ya utu wake, lakini zaidi ni kwamba Asia alikuwa akijiuza katika namna ya kidigitali. Hayajui mapenzi wala hajui nini maana ya kupendana…. Anachoamini ni kuwa anatoa penzi nawe umpatie pesa. Tena sio pesa kidogo!!
Anachuma mamilioni.
(MIKASA ZAIDI YA ASIA NI KATIKA SIMULIZI YA ASIA DIGITALI kama hujaisoma wasiliana nami inbox)
Alikuwa anamiliki gari yake, na nyumba nzima ya kupanga….. pesa yote aliitoa kwa wanaume katika njia za ki-digitali.
Asia akiwa na rafiki yake Husna wakaongoza njia kuelekea msikitini Kariakoo…
. . Jua lilikuwa kali, kilammoja alifanya jitihada za kupambana na joto la jijini Dar es salaam.
Hekaheka za hapa na pale Kariakoo ziliufanya mji kuonekana mdogo sana.
Kanzu nyeupe na mabaibui meusi yalitapakaa huku na kule ishara ya sala ya ijumaa.
. . Asia naye alikuwemo katika hekaheka za siku hiyo.
. . Muda wa sala ulipowadia kila mtu alikuwa mahala pake akiswali.
. . Asia naye alikuwa mmoja kati ya waliojumuika kuswali katika msikiti ambao hajawahi kuswali hapo kabla.
. . Asia aliswali huku mahesabu yake yakienda sawa kabisa juu ya mipango yake madhubuti kichwani.
. . Muda wa swala ulipomalizika Asia alitoka nje ya msikiti.
. . Akaangaza macho huku na kule.
. . Aliyategea mawindo yake yaweze kunasa.
. . Hatua kwa hatua Asia alijitembeza, kwa kasi huku akipigia mahesabu makali ya tukio ambalo litatokea.
. . Asia alikuwa akimtazama mwanaume mfupi mweusi ambaye huenda alikuwa amependeza kuliko wote ndani ya kanzu yake yenye thamani ya juu.
Asia alimtazama jinsi alivyokuwa amejikita katika kutumia simu yake. Asia akatumia upenyo ule.
. . Akajipitisha mbele yake, bwana yule pasipokumwona Asia akajikuta amemkanyaga. Asia akajilegeza akatua chini.
. . Aliyemgonga alikuwa ni Hassan Tembo, Munyama mukubwa kamba fedha ambaye alikuwa amevurugwa haswa na tukio lililotokea kwa Mamamia.
Hassan alikuwa anajulikana sana maeneo yale ya msikitini, asingeweza kumkimbia Asia ama kumpuuzia, aliheshimika kutokana na moyo wake wa kujitolea huku akiwa kijana mdogo.
. . Tukio la Asia akalitumia kama nafasi nyingine ya kuthibitisha kuwa ana pesa japo kwa wakati huo alitumia gari la kuazima na hakuwa na kadi yake ya benki japo alikuwa na kiasi fulani cha pesa alichokuwa amehifadhi ndani ya nyumba yake.
Akaamuru apelekwe katika gari lake binti yule.
Wafuasi wakambeba Asia hadi ndani ya gari la Tembo.
. . Akisindikizwa na wanaume wawili Hassan alimchukua Asia hadi katika hospitali ya watu binafsi maeneo ya mnazi mmoja.
Hapa sasa hakuwahitaji wale watu tena, akabaki peke yake.
Uzuri ni kwamba alikuwa na bima ya afya hivyo alifanya utaratibu na pesa kiduchu ikaongea Asia akatibiwa bure kwa kutumia kadi yake.
. . Hassan baada ya kuelezwa kuwa binti yule hakuwa amepata majeraha makubwa sana aliamua kuondoka naye aweze kumrejesha nyumbani.
Wakiwa ndani ya gari Hassan Tembo akakumbuka kuwa alikuwa matatani, na kilichochokonoa kichwa chake ni kisa cha Mamamia, akajiuliza ni lipi lilisababisha yale mambo kutokea. Akakumbuka na kujisahihisha kuwa haukuwa utaratibu wake kulala na msichana mmoja mara mbili.
Mh! Yawezekana ndo tatizo kweli ama?? Alijiuliza bila kupata jibu.
Akilini mwake sasa aliingiwa na ujasiri wa ajabu sana, hakutishika na kilichotokea chumbani akiwa na Mamamia, ile akili yake ya zamani ikarejea tena kwa kasi akaona Asia alikuwa mtu sahihi kabisa wa kumfanyia majaribio.
 
SEHEMU YA 70


. . Dini ya shetani.
Hassan alitakiwa kumwongezea wafuasi shetani. Na wafuasi waliokuwa wakihitajika ni wasichana.
. . Hassan alitakiwa kuwa anawaingiza wasichana katika utumwa ambao utawaweka dhambini. Na dhambi ile wataigawa kwa wanaume wao!
Tayari alikuwa amewavuruga wasichana zaidi ya sita. Wasichana hawa sita kadri walivyokuwa nao wanaunda cheni kubwa zaidi ndivyo Tembo alivyozidi kutajirika.
Hii iliitwa biashara ya mtandao ambayo Tembo alijiunga bila kujua ili aweze kujikwamua kutoka katika umasikini. Na kweli ikawa!!
. . Mitindo yake ya kizaramo, ujanja katika mapenzi ulimuwezesha kuwakamata wasichana wengi sana.
. . Sasa aliona hata Asia alikuwa msichana sahihi sana kwake.
. . “Binti..unaishi wapi kwani?” Tembo alivunja ukimya.
. . “Mbagala rangi tatu..” Asia alidanganya.
. . “Ok..naomba tupite mahali nimesahau kifaa changu halafu nikupeleke nyumbani.” Tembo akaingiza ujanja.
. . Asia hakupinga, kwani hata yeye alikuwa anataka Tembo ajilengeshe aweze kumtapeli kidigitali.
. . Tembo aliendesha gari hadi akaifikia hoteli maarufu na ghali kiasi mitaa ya Kinondoni.
Akamuacha Asia garini, upesi upesi Tembo akachukua chumba kwa senti alizokuwa amebakiwa nazo.
. . Akamwendea Asia garini.
. . Akamsihi wapate chakula kabisa. Asia hakupinga akakubali.
Moyoni kila mmoja alikuwa akifurahia kuwa na mwenzake zaidi na
zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa akiwaza la kwake lakini lililofanana na la mwenzake. Asia alikuwa akiwaza namna ambavyo atamuingiza mkenge Hassan Tembo na kisha kujipatia pesa za bwelele, Hassan Tembo naye alikuwa akiwaza na kuwazua namna ambavyo atamtumia Asia kupata pesa nyingi zaidi huku akiamini lile gundu la Mamamia litakomea hapo.
. . Kila mmoja alikuwa kidigitali zaidi. Pagumu hapo…
. . Tembo hakuwa na wasiwasi kuhusu kufanikiwa kwake kwani alikuwa anaamini kuwa yupo ambaye alikuwa akifanya kazi badala yake.
. . Asia alilazimika kutumia akili zaidi.
. . Baada ya kupata chakula Tembo nd’o alizuga kukumbuka kitu ambacho alikuwa amekisahau katika chumba kimojawapo katika hoteli hiyo.
. . “Vipi nikusindikize?” Asia aliingiza ujanja wake. Tembo akafurahia ombi lile.
Asia digitali na Hassan Tembo wakaongozana hadi chumbani.
Kama ilivyokawaida ya Asia akazuga hapa na pale mara ajikalishe vibaya.
Tembo akatabasamu kisha akafanya kitendo cha ghafla ambacho Asia hakukiona lakini taratibu hali ikabadilika.
. . Matiti ya Asia yakaanza kumwasha taratibu, akayakuna kidogo. Mara yakaendelea kumwasha tena.
. . Hali hii ikamshangaza kidogo, muwasho huu ulikuwa wa aina yake. Haukuwa katika namna ya kukera lakini ulikuwa wa kusisimua.
. . Asia anasisimka? Maajabu.
Matiti yakaendelea kuwasha kwa fujo.
. . Asia sasa alikuwa anamuhitaji mkunaji.
. . Nani zaidi ya Tembo?
. . Tembo alielewa ni nini kinaendelea. Alimsikitikia sana Asia kwani alikuwa anaenda kuingizwa katika mtiririko wa aina yake ambao una maana moja tu. Kumtumikia shetani.
Ni kweli Asia alikuwa amemtumikia shetani kwa kipindi kirefu, lakini hii ya sasa ilikuwa ni utumikiaji wa kilazima.
. . Tembo alikuwa anamuingiza katika ajira mbaya.
Asia akiwa pale kitandani jicho limemlegea hakuelewa ni nini kinaendelea lakini hakika alikuwa anahitaji huduma kutoka kwa Tembo.
Hassan Tembo akajawa na huruma akamvagaa Asia pale kitandani.
 
SEHEMU YA 71


. . Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa Asia alikuwa akifurahia penzi. Hisia zilikuwa juu mno na alionyesha ushirikiano wa hali ya juu.
Wazo la kutumia upenyo ule kumwibia Tembo lilipotea, Asia alikuwa katika dunia nyingine.
. . Laiti kama Asia angekuwa anamtambua Tembo vizuri, asingethubutu kujiingiza katika jaribio la kumdhulumu.
. . Tembo alikuwa mwanaume kama wanaume wengine kwa sababu anavaa suruali kama wengine lakini Tembo hakuwa mwanaume wa kawaida.
Alikuwa anasambaza ajira ya kutoka kuzimu. Ajira ya kumtumikia shetani.
. . Baada ya tendo Asia alikuwa amechangamka sana. Alikuwa amepata faraja ya mwili wake.
Asia akaijiwa na wazo la kuzungumza zaidi na Tembo ikiwezekana wawe wapenzi.
Akapanga kusema haya kwa Tembo baadaye wakiachana.
. . Tembo kama alivyoahidi alimwendesha Asia hadi Mbagala akamwacha kituo kikuu. Wakapeana namba na kuagana. Asia akiwa anashangaa Tembo ni mwanaume wa aina gani hadi ameweza kumpagawisha namna ile.
BALAA KWA ASIA ALIYETOLEWA KAFARA
. . Siku iliyofuata kizungumkuti kikaanza.
. . Asia akiwa peke yake chumbani, alianza kupatwa na hisia za maajabu.
Zile hisia za kuwashwa matiti na kupata hamu ya kufanya ngono.
. . Asia alizipuuzia lakini mara zikaendelea kumnyanyasa.Asia alihitaji kukunwa, lakini mkunaji angetoka wapi?
. . Mkusanya uchafu alisikika akiugonga mlamgo wa Asia.Kinyume na siku zote Asia alimkaribisha ndani. Mkusanya uchafu akaingia, Asia akafika hadi sebuleni akiwa na kanga moja.
. . Mkusanya uchafu akashangaa lakini hakuweza kufumba macho.
. . Asia alikuwa katika mateso makubwa.
. . Mkusanya uchafu naye mwanaume anajua mwanamke akiwa katika uhitaji anakuwaje.
. . Mkusanya uchafu akaona hii ilikuwa nafasi ya kipekee ya kutuliza hamu zake. Akamvamia Asia akaitupa kanga mbali naye.
. . Kilichofuata Asia hawezi kukisimulia zilikuwa ni raha za kipekee.
Baada ya tendo Asia akakimbia chumbani kwa aibu kubwa. Mkusanya uchafu akaondoka zake huku akistaajabu nini kimetokea.
**BALAA…..Asia ametolewa vip kafara…..
USIKOSE KESHO….
 
SEHEMU YA 72


. . Hali hii ya utumwa iliendelea tena siku nyingine.
Siku hii mwili wa Asia ukawa mali ya ‘Mr. kucha’…….
. . Hii nayo ikapita. Asia hakuwa kibiashara tena bali alikuwa analiwa bure tena alikuwa akipata faraja ya hali ya juu.
. . Asia yule wa digitali akajikuta amaewingizwa mkenge. Sasa akawa mfuasi wa mapenzi.
Hakujua kama mapenzi hayo alipachikwa na Hassan Tembo ili amsaidie kuongeza idadi ya waumini katika kontena lake la kishetani.
Kila muumini mpya mmoja, pesa ya Tembo ilikuwa inaongezeka.
Asia hadi kufikia wakati huo alikuwa amevuta wateja wapya sita na alikuwa anaendelea kuvuta wengine.
. . Fedheha na aibu zikamtawala na kumpelekesha Asia, akajikuta katika maamuzi mabaya sana.
Maamuzi ya kukataa kurejea alipotoka.
. . Asia alikuwa mfuasi wa mapenzi hapo zamani, alikuwa akipenda amependa kweli lakini baadaye akayageuza mapenzi hayo kuwa biashara. Akapata pesa nzuri. Lakini tangu akutane na Hassan Tembo basi mambo yakabadilika, hazikuwa zikipita siku tatu, Asia alikuwa anahitaji mwanaume wa kukidhi haja zake.
. . Alikuwa anawashwa sana matiti yake, ni mwanaume pekee alihitajika kwa ajili ya kumkuna.
Kila alivyokunwa akajikuta akitoa na utupu wake.
Hii kwake ilikuwa dharau isiyostahimilika.
. . Asia akaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Hawa nao wakamtaka kimapenzi.
Akawapa huduma bila mafanikio.
. . Baadhi ya waganga wakampa maelekezo kuwa kila anapowashwa awe anawatembelea wampe tiba. Huu akaona ni upuuzi.
. . Waganga wa jadi hawakumsaidia chochote.
. . Hospitali napo walisema lugha zao ngumu ambazo Asia hakuzielewa, wakampatia vidonge lakini bado hali ikawa tete. Hamu kwa Asia ikadumu. Na alipoipata haikupoa hadi pale alipopata wa kumpooza. Leo akipoozwa na huyu kesho anapoozwa na yule.
. . Wanaume wakahadithiana na sasa wakawa wanamlia ‘taiming’ akiwashwa wamkune.
Hali hii ikamdhoofisha Asia. Na kumweka katika hali ya kukata tamaa.
Hakuwa mchakarikaji tena. Hakuwa kidigitali tena.
Asia hakungoja ukurasa ujifunge wenyewe akaamua kuufunga kwa nguvu.
. . Ilikuwa siku kama siku nyingine, wanaume kadhaa walikuwa wakiranda randa jirani na nyumba ya Asia wakingoja akumbwe na muwasho.
Walingoja sana kwa siku hiyo lakini hapakujiri chochote. Hali ambayo iliwakera sana, kwani waliufanya mwili ule kama mali yao halali.
. . Wengine waliendelea kuvuta subira hadi usiku lakini cha kustaajabisha Asia hakusikika walau kujishughulisha katika chumba chake.
Ajabu na kweli.
 
SEHEMU YA 73


. . Siku nzima bila kutoka kitandani.
. . Wanaume wenye uchu wakaamua kuingia ndani, kutazama kulikoni.
. . Wakatumia tochi zilizo katika simu zao.
. . Wakapekua huku na kule, hawakuona mtu.
Mwisho wakalifikia jiko.
Ni huku walipoukuta mwili wa Asia ukiwa unaning’inia juu.
Ulimi nje.
Asia hakuwa hai tena. Alikuwa ameamua kujiua
. . Alizaliwa kianalojia akaishi kidigitali na hatimaye anakufa kianalojia akiwa na upande wa kanga shingoni kwake, ulimi nje. Miguu ikining’inia.
. . Wale waliokuwa marafiki zake walikana kumjua. Wale walioshiriki naye kuzitumia pesa alizochuma kidigitali wote wakajiweka mbali na mwili ule.
Serikali ikachukua maamuzi baada ya kutangaza na ndugu kukosekana.
Asia akazikwa na serikali.
Huu ukawa mwisho wa simulizi yake ya maisha. Lakini mwisho huu ukaibua makubwa!!
ASIA alikuwa ametolewa kafara na mganga yule kupitia Tembo ili kumpa nafasi mteja wake yaani Brenda aweze kupambana zaidi kumfikisha Tembo kwenye tiba.
Kifo cha Asia kikaondoka na nguvu nyingi za Tutufye Kanyenye yule mtumikia shetani aliyemuajiri Tembo.
Kilichobaki ili kuleta amani zaidi na kila mmoja kurejea katika hali yake ya kawaida kikawa kimoja tu!!
Hassan Tembo apatikane kisha aongozane na Brenda katika kitanda ambacho kwa mara ya kwanza Hassan aliota ile ndoto na alipoamka akaamka na utajiri huku akifanya mambo ya ajabu bila akili yake kutambua.
Mganga alimweleza Brenda kuwa mzimu ule wa Tutufye unatakiwa kuzikwa moja kwa moja. Kwani baada ya siku saba unaweza kuamka tena huku ukiwa na hasira.
“Umtafute Tembo umweleze ninayokueleza, baada ya siku saba akinyanyuka mimi, wewe, yeye na wote walioajiriwa naye tutakuwa matatani, tutakufa vifo vibaya sana…. Tuntu hajui kusamehe.., narudia tena Tuntu hajui kusamehe….” Mganga alimsisitiza Brenda juu ya hilo, na kisha kumsihi afanye juu chini aweze kumpata Tembo.
WAKATI Tembo anatafutwa kwa udi na uvumba, tayari alikuwa amebadili namba ya simu. Biashara yake ilikuwa imezorota sana hivyo akabaki kuwa mtu wa kujifungia tu nyumbani kwa rafiki yake.
Mamamia naye alikuwa amerejea katika hali yake ya kawaida na asikumbuke kitu gani kilitokea katika maisha yake.
Kifo cha Asia kilikuwa kimeondoka na utawala wa Tuntu… lakini kama alivosema mganga… ilikuwa kwa siku saba tu na baada ya hapo yanafuata maafa. Asia anainuka tena ndani yake akiwa amemvaa Tuntu!!
 
SEHEMU YA 74


Siku tatu zikakatika na hatimaye kubaki nne, mganga hofu ikatawala na Brenda akakiona kifo kikiwa jirani naye.
****
MGANGA alijaribu kurusha matunguli yake lakini hakuna kilichoonekana kuleta uelekeo wa wapi alipo Tembo. Hii ilikuwa ni siku ya nne, mganga akamlaumu Brenda kwa kumwingiza katika tatizo lile, Brenda hakujua nini cha kujibu, tamaa zake za kutaka kuolewa na Tembo zikamtokea puani….
Dar es salaam ni ndogo kwenye ramani tu, lakini kiuhalisia ni jiji kubwa sana, utaanza vipi kumsaka Tembo mtaa kwa mtaa.
Brenda alikonda haswa.. huku nyumbani kwao alitakiwa kumuhudumia Mamamia ambaye licha ya kuwa timamu tena alitakiwa kuwa chini ya uangalizi wa karibu sana. Wakati huohuo Brenda alitakiwa kushirikiana na mganga wa jadi kuweza kutatua lile jambo ili watetetee uhai wao.
Akili ya Brenda ilitanuka haswa!! Hakuwa na mahali pa kupata ushauri, kikubwa alitakiwa kummpata tembo.
SIKU YA TANO.
Brenda akaona ni upuuzi kufa huku ukikiona kifo ukashindwa kukikwepa. Akaamua kumshirikisha Mamamia juu ya jambo lile, Mamaia akataharuki haswa lakini akakiri kupafahamu nyumbani kwa Tembo. Akamuelekeza Brenda vyema namna ya kufika katika nyumba ile.
Mamamia ambaye alikuwa mnyonge aliyekonda, macho yakamtoka pima. Akapagawa haswa na kumuhimiza mdogo wake afanye kila namna aweze kupapata nyumbani hapo na kisha kumsisitiza Tembo afanye kama mganga alivyowaagiza.
Brenda alikodi pikipiki hadi nyumba aliyoelekezwa na dada yake.
Alipoifikia nyumba akapagawa alipoelezwa kuwa Tembo ameshindwa kulipa kodi yake na haonekani alipo…… na mwenye nyumba alikuwa amemchukua mjumbe tayari kwa zoezi la kuhamisha vitu vya Hassan ili ndani ya nyumba ile aingie mtu mwingine.
Brenda alijikaza asiionyeshe hofu yake waziwazi, lakini alipofika chini ya mti mbali na nyumba aliyokuwa anaishi Hassan Tembo, aliketi chini kisha akaanza kulia na kujuta huku akilini akikumbuka kuwa bado takribani masaa ishirini tu!!
Masaa ishirini Tuntufye Kanyenye ainuke tena akiwa na hasira kali….
Harufu ya kifo nje nje!!
**Tembo hajaonekana bado na masaa yanakatika…… nini kitajiri iwapo Tuntu atanyanyuka na kurejea katika utawala!!!
SHARE iwafikie na wengine ambao hawaioni kurasa.
NB: Njia nyingine mbadala ya kuisearch page hii andika ‘George wa had’…. Utaiona bila shida…….
 
SEHEMU YA 75

Tembo alikuwa amejikunyata katika kochi, miguu yake ikiwa imekunjwa kwenye sehemu ya kukalia kichwa chake kikitazama dari.
Tembo alijipapasa katika mabega yake akavipapasa na vishimo juu ya kifua chake akakiri kweli kuwa amekonda sana. Hakuamini hata kidogo kuwa yupo katika msoto mkali ghafla kiasi kile.Lakini licha ya msoto huo kuna jambo la ziada aliligundua katika mwili wake!!
Tembo hakuwa na hamu na wanawake kama ilivyokuwa awali na pia akili yake ilikuwa ikifikiri kwa mapana zaidi. Akajiuliza, ilikuwaje hata akafanya zinaa na wasichana wengi kiasi kile, hakupata jibu la moja kwa moja.
Mlango ulipofunguliwa ndipo akafikia ukomo wa kuwaza kwake, alikuwa ni rafiki yake ambaye alikuwa amemuhifadhi..... Alikuwa anatokwa jasho na shati lake jeupe likiwa shaghalabaghala!
Tembo akaduwaa kumwona yule bwana katika hali ile, haikuwa kawaida yake hata kidogo. Kukosa unadhifu!
"Yupo wapi huyo mwenzako!?" swali lilisikika kutokea nje.... Tembo akataka kusimama na hapo wakaingia wanaume wawili. Sura zao na lafudhi yao ikawatambulisha kuwa ni watu kutoka mkoa wa Mara.
"Wewe nd'o wa kujifanya kidume sivyo..." swali likamuelekea Tembo. Akaanza kubabaika, mara akaongezeka mtu mwingine ndani ya kile chumba. Huyu alikuwa ni mwanamke, mimba yake ikionekana waziwazi. Sura ile haikuwa ngeni sana kwa Tembo lakini hakujua ni wapi aliiona mara ya kwanza.
"Ndiyo huyu mwenzako eeeh!" mzee aliyekuwa na jazba alimuuliza yule binti...
Binti akatikisa kichwa kukubali.
"Kijana nisikilize kwa makini maamuzi ni mawili tu hapa... Utamlea mwanangu na mimba yenu hii... Ama hii RB nikupeleke kituoni sasa hivi..." mzee akazungumza kwa sauti ya chini akijaribu kuidhibiti jazba yake. Lakini mikono yake ilikuwa ikitetemeka kumaanisha kuwa alikuwa ana hasira kali.
Baada ya kusikia kuhusu mimba Tembo akamtazama tena yule binti safari hii akamwangalia mikononi, akakutana na kicheni kilichoandikwa maneno kadhaa, akamkumbuka Beatrice binti wa kwanza kabisa kukutana naye akiwa ameianza ajira asiyoifahamu, akamnunulia chipsi kuku mwishowe wakazini.
 
SEHEMU YA 76


Kumbe alimjaza mimba.
"Tembo eeh ulichoniletea ni aibu mshkaji wangu, mimi nimekabwa ka' mwizi yaani, cha msingi kaka ili heshima iendelee kuwepo ni heri tu hapa kwangu uondoke... Na hilo sio ombi ujue... we una kwako kabisa naomba urejee tu huko." Rafiki yake Tembo aliyekuwa amemuhifadhi alitoa amri hiyo.
Tembo hakuwa na la kufanya, kila jambo baya lilikuwa limegeukia upande wake. Beatrice akaachwa pale na wazazi wake. Tembo akatakiwa kuhudumia tumbo na mama. Wakati huohuo aliyekuwa anamuhifadhi naye akakifunga chumba chake na kuondoka akimwacha Tembo nje akiwa hana la kufanya!!
***
Masaa yalizidi kuyoyoma na ahadi ya mganga yule ikiwa ni moja tu. Kama Tembo hapatikaniki hadi muda alioukadiria kupita basi kifuatacho ni maafa makubwa!!! Wote ambao wapo katika orodha ya kupitiwa na Tembo basi kifuatacho ni hasira ya Tuntu kukaa juu yao.
Vifo vibaya, nd’o mganga alichowaeleza!!
Mamamia akiwa bado dhaifu kiafya akaona ni heri nusu shari kuliko shari kamili, akaamua KUINGIA RASMI KATIKA OPERESHENI MSAKO WA Tembo.
Mguu kwa mguu na mdogo wake wakaandamana huku na kule, wakati huo yakiwa yamesalia masaa kumi na ushee ili Tuntufye aweze kunyayuka tena kutoka katika kaburi ambalo alikuwa amezikwa na serikali ndani ya mwili wa Asia Digitali.
Wakahaha huku na kule jitihada zikagonga mwamba.
Hatimaye wakaamua kurejea tena nyumbani kwa Tembo ambapo hakuwa akiishi tena.
Huku wakitumia usafiri wa pikipiki ya kukodi hawakuweza kuhangaishwa na foleni, wakafika yakiwa yamebakia masaa manne tu kabla ya kutokea hayajatokea.
Kila mara mganga ambaye alikuwa na hofu tele alikuwa anapiga simu kuuliza mafanikio. Uoga wa mganga ukazidi kuwapagawisha akina Mamamia na Brenda. Kifo wakakiona kikiwapungia mkono wa kuwaita. Ile kauli ya Tuntu hajui kusamehe nayo ikazidiu kuvitawala vichwa vyao.
Ilikuwa kama bahati ya mntende kuota jangwani!!
Walipofika nyumbani kwa Tembo wakapewa taarifa kuwa ameenda nyumbani kwa mjumbe ili aweze kupewa mizigo yake iliyotolewa ndani baada ya kuonekana kuwa hawezi tena kulipa kodi yake.
Mamamia na Brenda wakiongozwa na mtoto mdogo wakaelekea nyumbani kwa mjumbe.
Huku likazuka timbwili la aina yake!
 
SEHEMU YA 77


Tembo alikuwa wa kwanza kumuona Mamamia, msichana yuleyule aliyemtaabisha ndani ya kile chumba na kumsababisha aondoke akiwa amevaa taulo pekee.
Tembo akabaki kutetemeka, mjumnbe hakujua nini tatizo. Mamamia na Brenda wakazidi kumsogelea, Tembo akiwa amekodoa macho yake alihamanika haswa!!
Wakati huu hakutaka tena kuaibika kama ilivyokuwa awali, akahesabu mita kadhaa kutoka lilipokuwa geti akaona zinamfaa kabisa kuukwepa mkasa huu wa hatari, Tembo alikywa akimuogopa Mamamia.
Laiti kama angejua jambo aliloitiwa ni kwa ajili ya usalama wake. Wala asingediriki kufanya alilofanya.
Tembo akaamua kutimua mbio ghafla, akimwacha nyuma Beatrice na tumbo lake pamoja na Mamamia na Brenda.
Labda Brenda alikuwa hakiogopi kifo sana kuliko Mamamia nd’o maana akabaki kuduwaa.
Mamamia hakutaka kuipoteza nafasi hii, upesi akalikunja gauni lake, urembo akaweka kando akaanza kutimua mbio kumfuata Tembo. Na kosa kubwa alilofanya Tembo ni kukimbilia sehemu tambalale ambapo anaonekana. Mamamia akaamua kuifanya hii kuwa nafasi yake ya mwisho kumpata Tembo na nafasi yake ya mwisho kuutetea uhai wake ambao upo mikononi mwa Tembo bila yeye kujua.
Tembo hakuamini alipogeuka nyuma na kushuhudia Mamamia akimfuata kwa kasi.
“NBaabika mtaani kwangu leo hii…” Tembo akajisemea huku akiendelea kutimua mbio.,
Alichoendelea kuamini Tembo ni kwamba Mamamia alikuwa amepandwa na mashetani yake bado. Tembo alipokaza mwendo zuali yake ikafunnguka mkanda na kum legea, akajaribu kuipandisja lakini jitihada zile zikagonga mwamba. Suruali ikatelemka na kumnasa miguu, Tembo akaanguka mchangani, na ndani ya sekunde kadhaa Mamamia akawasili…… akamwangukia pale pale mchangani.
Tembo akaanzaq kupiga mayowe!! Mamamia akiwa anahema juu juu akawa anamshangaa kijana huyu, kumbukumbu kuwa aliwahi kuimletea puruykushani walipokuwa nyumba ya kulala wageni hazikuwepo kabisa.
“Hassan…. Ha….Tembo… tupo hatarini Tembo, tuokoe tafadhali tuokoe tunakufa..” Mamamia akajikaza huku akihema juu juu vilevile akazungumza. Kauli hiyo ikamzidishia Tembo imani kuwa Mamamia bado ana mashetani kichwani.
 
SEHEMU YA 78


“Tembo, yaani mimi,wewe, Brenda, na mganga.. wote tutakufa huyo Tuntufye akiamka.. tunakufa Tembo..” alilalamika zaidi. Tembo akasikia jina ambalo aliwahi kulisikia mahali.
“Tuntu ndo nani..” akauliza.
“Alikupa ajira toka kuzimu.. alikuajiri wewe nawe ukatuajiri sisi.. Tembo hakuna muda wa kupoteza hapa. Muda umekwisha Tembo tutakufa.”
“Sasa nafanyaje mimi, nani kaniajiri umesema..aah huyu Tuntu ye yukwapi?” akaanza kuuliza maswali ya kipumbavu Tembo…
Mamamia akamnyanyua, na hapo akina Brenda na Beatrce wakawasili. Brenda akamweleza Tembo kwa kifupi kisa na mkasa na nini hatma yao!!
Tembo akapagawa!!!
Hofu ya kifo ikamwingia na yeye…
Upesi zikachukuliwa pikipiki na kuelekea nyumba aliyokuwa akiishi Tembo zamani, nyumba ambayo Tuntu alimpatia ajira kewa mara ya kwanza. Kwenye kile kitanda alitakiwa akatoe vitu ambavyo vcinatakiwa kuchomwa moto, likiwemo na lile godoro alilokuwa amelilalia siku hiyo.
Tembo akaongoza msafara… wakaifikia nyumba yakiwa yamebaki masaa mawili tu Tuntu ainuke tenma na kuwapa adhabu kuu.
“ANAYEISHI HUMU AMEFIWA AMESAFIRI KWENDA MSIBANI….” Wakapewa jibu hilo na mpangaji mwingine.
Wote kwa pamoja wakachoka, na lilikuwa limebaki saa moja na dakika kadhaa!!!
ITAENDELEA!!!
Umeme unazingua sana nd’o maana inakuja bila ratiba!!!
SHARE KWA WINGI.... ukurasa wetu bado una tatizo... wengine waweze kuiona
 
SEHEMU YA 79, 80, 81 na 82


Mamamia akamnyanyua, na hapo akina Brenda na Beatrce wakawasili. Brenda akamweleza Tembo kwa kifupi kisa na mkasa na nini hatma yao!!
Tembo akapagawa!!!
Hofu ya kifo ikamwingia na yeye…
Upesi zikachukuliwa pikipiki na kuelekea nyumba aliyokuwa akiishi Tembo zamani, nyumba ambayo Tuntu alimpatia ajira kewa mara ya kwanza. Kwenye kile kitanda alitakiwa akatoe vitu ambavyo vcinatakiwa kuchomwa moto, likiwemo na lile godoro alilokuwa amelilalia siku hiyo.
Tembo akaongoza msafara… wakaifikia nyumba yakiwa yamebaki masaa mawili tu Tuntu ainuke tenma na kuwapa adhabu kuu.
“ANAYEISHI HUMU AMEFIWA AMESAFIRI KWENDA MSIBANI….” Wakapewa jibu hilo na mpangaji mwingine.
Wote kwa pamoja wakachoka, na lilikuwa limebaki saa moja na dakika kadhaa!!!
*****
SIMU ya Athumani au maarufu kama Bichwa haikuwa inapatikana. Muda ulizidi kwenda na mganga akizidi kupiga simu kuwa hapatakuwa na namna ya kumkwepa Tuntu iwapo atainuka kabla godoro halijachomwa moto. Na makorokoro yaliyoko chini ya kitanda hayajaondolewa.
Bichwa ndiye alikuwa mmiliki wa chumba kile baada ya Tembo kuhama. Na taarifa ilikuwa kwamba ameenda msibani kijijini kwao, simu haikuwa inapatikana. Tembo alitamani walau atokee jirani mmoja ambaye atamkumbuka kuwa aliwahi kuishi katika chumba kile lakini haikuwa hivyo. Kila mpangaji alikuwa mgeni machoni pake.
Wasichana wakawa wanamtazama Tembo aweze kufanya maamuzi ya busara ili waweze kulikwepa janga lililopo mbele yao.
“Kama vipi tuvunje!!” Tembo akatamka kwa sauti ya juu huku akiwa haonekani kujiamini hata kidogo. Mamamia akakubaliana na wazo la Tembo, lakini wakati huohuo mpangaji mmoja akatoka katika chumba chake. Alikuwa mama mtu mzima akiwa ameifunga kanga yake katika mtindo wa lubega.
Macho yake makubwa yakawatazama akina Tembo, akalamba midomo yake kisha bila kutoa salamu yoyote akaanza kuporomosha maswali na kashfa hata asiwape nafasi moja ya kujibu.
Lafudhi yake pekee ilitosha kumtambulisha kuwa alikuwa mzaramo. Kama hiyo haitoshi mama huyo alipaza sauti juu akamuita mwenzake kwa jina la mama Zulfa.
Huyu sasa alikuwa kiboko zaidi yake, alidandia treni kwa mbele lakini moto wake ulikuwa wa ajabu.
“Kione kifupiii eti nyooo tuvunje kama vipi, mi nimekisikia tu nikawa nangoja nini kitafuata, uvunje mlango kwa misingi gani. Kama mnadaiana ni nyie hukohuko, Athumani katukabidhi chumba chake kikiwa kimefungwa na atatkikuta hivihivi kikiwa kimefungwa, ona na kile kingine kimepauka miguu kinaunga mkono eti nyoo tuvunje, mwone manyonyo yake hovyooo, mijitu sijui ya wapi hii. Hata salamu haitoi. Ona litumbo lake, tena mtupishege msije kuwa mnataka kuzalia katika hiko chumba cha Athumani wa watu…..” mama mtu mzima alizidi kuropoka na hapo yule kiboko yao akampokea sasa.
“…ona mimacho yake imerendemka kwa husda mnazotaka kuleta kwa Athumani wa watu. Mbona hamkuja alipokuwa hapa, mmetegea ametoweka nd’o vitumbo mbele, na kianaumne chenu lisuruali linazidi mwili. Mwone shati lake kama kaja mjini na lifti za magari ya mkaa vile mweusii, likipara ka tako la mtoto mdogo vibaka wakubwa nyie….” Yule dada asiye na haya huku akipoandisha macho na kushusha aliwapayukia akina Tembo.
Tembo, Brenda na Beatrice walibaki kuduwaa wasijue na kufanya, lakini Mamamia alishavurugika kichwani. Na yale matusi yakamchanganya zaidi, akachomoka upesi akamvamia yule dada aliyedandia treni kwa mbele. Akamdaka vyema shingo yake.
Tembo akabaki kushuhudia timbwili. Yule mama mtu mzima akajisogeza aweze kuingilia, Mamamia akamuona… akamdaka ile kanga yake upesi akaivuta ghafla.
Ebwana eeh!! Tuliokuwepo nd’o tulifaidi zaidi, wewe msomaji endelea kupatia picha katika maandishi.
Shanga kama nane katika kiuno cha yule mama zikaonekana, akashindwa aidha ayazibe manyonyo yake ama azibe huko chini. Akimbie ndani ama aendelee kusimama.
Mamamia akaendelea kutoa kipigo kwa dada mvamia treni kwa mbele. Kilikuwa kipigo cha kimyakimya lakini kitakatifu.
Muda ulizidi kwenda kasi, ugomvi nao ukachukua dakika zaidi.
Mamamia alikuwa na wazo kichwani mwake, wazo hili lilikuja wakati anapigana na yule mwanadada. Akajaribu bahati yake ya mwisho kabisa kama kweli aliwazalo litafanya kazi.
Upesi akamuachia yule dada pale chini, akamvamia yule mama mwenye mwili mkubwa na shanga zake kiunoni.
Aliamini kabisa kuwa yule mama akiwa na timamu zake hawezi kummudu, hivyo akiwa yu uchi hajielewi elewi nd’o ilikuwa nafasi ya kipekee.
Mamamia akamrukia na kumsukumia katika mlango wa chumba cha Athumani bichwa.
Kama vile ameyaona yaliyo mbele yake, ikawa vile. Mlango wa nyumba ya uswahili ukaporomoka kwa uzito wa yule mama kibonge.
Zilikuwa zimebaki dakika takribani dakika kumi na tano mambo yaharibike.
Baada ya kuangukia mle ndani mlango ukiwa umevunjika ndipo likazuka balaa jingine la mwaka.
Chumba kile kilichofungwa kwa kufuli kabisa, ndani yake pakitegemewa kuwa tupu. Haikuwa hivyo!! Kitu kikakurupuka kisha zikasikika kelele kuu za kiume.
“Mamaaaaaaa….”
Si Mamamia wala yule mama kibonge wa kuwa uchi aliyekuwa jasiri katika hili. Kila mmoja akapiga mayowe, lakini aliyeogopa zaidi alikuwa mama kibonge. Kwani alikuwa anatazamana ana kwa ana na Athumani Bichwa ambaye anasadikika kuwa amefiwa na ameenda msibani.
Kwa hiyo moja kwa moja mama kibonge akaamini kuwa ule ni mzimu wa Athumani, tena mzimu wenyewe ulikuwa umevaa chupi tu.
Mama kibonge akazirai pale pale.
Athumani bichwa yeye akawa ameduwaa hata asikumbuke kuwa yupo na kichupi tu.
Mamamia alivyotoka mbio, akina Brenda nao wakataka kuunganisha naye lakini Tembo akawahi kumdaka mkono.
“Tembo kuna mzimu humo…. Mzimu una chupi tu….” Mamamia akapayuka, mashuhuda wengine waliokuwa pale kushuhudia ugomvi ule wakavutiwa na maelezo yale, wakaanza kujisogeza pale katika kile chumba hata yule dada aliyepewa kipigo na Mamamia naye akasogea jirani. Wakati huu akiwa mpole sana.
Wengi wao waliogopa kuingia mle ndani kutokana na kusikia habari za mzimu wa Bichwa ndani ya chumba chake. Lakini Tembo na wenzake walilazimika kuingia kwa sababu walihitaji sana kutoa makorokoro chini ya kitanda ili yasije kuwakuta mabaya mzimu wa Tuntu ukiamka tena.
Tembo na akina Mamamia wote wakaingia, yule dada mnyonge wa Mamamia naye akaunga tela akatazame huo mzimu pia amtazame na shoga yake ambaye alikuwa amepoteza fahamu.
Hakujua kama anajiingiza katika mkumbo asioujua.
“Bichwa…..” Tembo akamuita jamaa aliyekuwa ameduwaa na kichupi. Athumani hakugeuka alibaki kuwa ameangalia chini tu huku akiwa ameganda kama sanamu.
Upepo mkali ulivuma kupitia madirishani, ilikuwa ni kama dalili ya mvua. Wasshabiki walikuwa wameongezeka nje ya mlango lakini wakihofia kuingia ndani ya kile chumba. Hadi pale mjumbe wa nyumba kumi kumi alipoingia mle ndani kujua kulikoni.
Hata yeye alikuwa ameingia wakati mbaya sana. Ni bora hata asingefika kabisa.
Mvua kubwa ikaanza kunyesha….. mvua iliyodumu kwa dakika takribani kumi na tano tu kisha ikakoma.
“Wewe Bichwa imekuwaje upo ndani ya chumba hiki na umefungiwa kwa nje?” mjumbe akamuhoji Bichwa….. safari hii Bichwa alikuwa amevaa nguo zake huku akiwatoa hofu kuwa yeye sio mzimu bali kuna madeni alikuwa anayakwepa nd’o kisa cha kujifungia ndani kwa mtindo ule. Akamtaja na aliyemfungia kuwa ni rafiki yake.
Zile kelele za umati hazikusikika tena. Mjumbe akaamini kuwa mvua ile itakluwa imewakimbiza pale. Mama kibonge naye alikuwa amezinduka, hivyo ndani ya chumba kile wakawepo watu nane. Wanaume watatu na wanawake watano.
“Mi naomba nikapumzike jamani…..” Mama kibonge akaomba, mjumbe akawasihi kuwa hakuna ambaye anatoweka pale hadi wajue namna ya kuukarabati mlango wa Athumani.
Wakati huo zilishapita dakika zaidi ya arobaini tangu ule muda walioungoja utimie na haukutimia. Brenda akahisi yule mganga ni mwongo kabisa aliyewaingiza katika aibu kuu. Akatamani kumpigia simu amkaripie lakini akajipa muda zaidi mpaka atakapokuwa peke yake.
“Nitaukarabati mimi..” Mamamia akamaliza mzozo. Hilo likapitishwa na kila mmoja akatakiwa kuondoka. Hapo ndipo lilipotokea la kutokea.
Wanane hawa walipotoka nje ya kile chumba wakajikuta katika mji wasioufahamu, mji ulikuwa umechangamka sana kila mmoja na shughuli zake huku wakizungumza lugha waliyoijua wao tu. Vitu walivyokuwa wanauza hata havikueleweka eleweka, lakini walikuwa na furaha sana.
Mjumbe akataka kurudi katika chumba cha Athumani Bichwa kwa uoga lakini akafadhaika kabisa.
KILE CHUMBA HAKIKUWEPO TENA………badala yake akakutana na watu wakiwa wametingwa na biashara zao za bidhaa zisizofahamika.
“Tuko wapi hapa eeeh!” Mjumbe akamuuliza Tembo ambaye alikuwa amekodoa macho na mdomo wake ukiwa wazi. Hakujibiwa!!
“Tembooooo……we Munyama weweeee!!! Munyama mukubwa kamba fedha… baba lao hiloooo…” ikasikika sauti kwa mbali ikimwita Tembo kwa manjonjo makubwa.
Tembo akaona hii nd’o nafasi ya kupata mwenyeji na kumuuliza hapo ni wapi na imekuwaje wapo hapo.
Tembo akatilia maanani sauti ilipotokea….
Naam! Akakutana na sura aliyokuwa anaifahamu vyema kabisa… hamu ya kumjua mwenyeji wake ikakoma. Akaanza kutetemeka wakati mwanadada yule mwenye tabasamu pana usoni akizidi kumsogelea.
Alikuwa ni ASIA DIGITALI!!
Mungu wangu tupo kuzimu!!! Tembo akajisemea, Brenda akamsikia.
“Unathemaje Hathani…hapa kudhimu….. mama weee” Kithembe akapagawa, na hapo mkojo wa moto kabisa ukapenya katika chupi yake.
***Haya sasa, THE RETURN OF ASIA DIGITALI!!!
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA 83


Mungu wangu tupo kuzimu!!! Tembo akajisemea, Brenda akamsikia.
“Unathemaje Hathani…hapa kudhimu….. mama weee” Kithembe akapagawa, na hapo mkojo wa moto kabisa ukapenya katika chupi yake.
“Karibu kwangu Tembo…..” Asia alizungumza huku akiwa anarembua macho yake. Mchomo wa wivu ukapenya katika moyo wa Brenda ila alipokumbuka kuwa yupo kuzimu hofu ikarejea. Lakini akakiri kuwa hakika alikuwa anampenda Tembo.
Asia alimshika mkono Tembo na kuongozana naye hadi katika chumba kikubwa chenye uwazi sehemu kubwa na sehemu moja ikiwa na meza pamoja na viti. Tembo na wennzake wote wakaketi.
“Wanadamu wapumbavu sana ninyi….. pumbavu kabisa nasema.” Asia alikuwa kama anayezungumza peke yake!! Hakuna aliyemjibu wote walikuwa wanatetemeka.
“Ooooh!! Halafu mimi naye nasahau kabisa kuwa ninyi ni wageni wangu hata maji sijawakaribisha…. Tembo waulize wenzako kinywaji gani wanapendelea kwanza. Au ngoja… kila mmoja ataje kinywaji anachopendelea…. Ila zisiwe pombe tu maana hapa haziruhusiwi kabisa.” Asia akazungusha macho yake kwa wageni wake.
“Mama Ashura….” Akaita, yule mama mwenye shanga kiunoni akaduwaa Asia amemjuaje. Asia hakujali akamalizia, “Unatumia kinywaji gani…”
“Chochote tu mama yangu!!” akajibu kinyonge huku akiifinyafinya mikono yake.
“Na wengine mliobakia…” akahoji. Wote wakatoa jibu kama la mama Ashura kasoro Brenda ambaye alileta kizaazaa.
“Mi thinywi kitu….”
“Unasema….” Asia akamuuliza kwa sauti ya upole.
“Thinywi chochote.. “
“Kwanini haunywi..”
“Thjithkii tu….”
Asia akatulia huku akimtafakari Brenda na ile ongea yake.
“Thjithkii kunywa chochote..” Kamuigiza anavyoongea huku akiwa ameibana pua yake.
 
SEHEMU YA 84


Asia akaondoka huku akizidi kusikitika na kusema ‘wanadamu…wanadamu…’
“Tembo huyu ni nani?” hatimaye Mamamia alimuuliza, Tembo akajikohoza kidogo kisha akamjibu kuwa anaitwa Asia. Jina hilo lilikuwa geni kwa Mamamia. Akataka kuuliza zaidi lakini akamwona Asia akitembea kwa maringo na nyuma yake wakifuata watu wanne na sahani kubwa.
Wakalitua katika meza… harufu isiyoeleweka ikatawala eneo lile.
Asia akatabasamu kisha akaunyanyua uso wake na kuwatazama wageni wake zamu kwa zamu. Walikuwa wameduwaa tu, labda walikuwa wanaishangaa ile sahani kwa jinsi ilivyokuwa kubwa.
“Funua!!... wewe hapo nd’o utafunua na utawapakulia wenzako chakula” aliamrisha Asia kisha akamnyanyua Brenda kwa mkono mmoja akasimama wima, akamtanguliza mikono yake ikashika ule mfuniko. Asia akamwamuru afunue!!
Ebwana eeh! Tembo akaruka kule, Mamamia huko, Brenda huku na wale wageni wengine kila mmoja akajitetea kivyake kwa mayowe makubwa.
“He! Sitaki kuamini yaani kumbe waoga hivyo… kweli nyie hamna njaa kabisa. sasa nini cha kuwaogopesha hapa hebu acheni ujinga njooni mezani jamani….” Asia ambaye kwa mara ya kwanza alizama katika kicheko kikubwa sana hatimaye alizungumza.
Hakika kila mmoja alikuwa na haki ya kupagawa, kwenye ile sahani kubwa ya maajabu alikuwa amelala yule mganga wa jadi ambaye alifanya jitihada za kutaka kumtokomeza Tuntufye Kanyenye kwa kumtoa kafara Asia Digitali.
Bora ungekuwa ni mwili wenye uhai….. huu haukuwa na uhai na ulikuwa umetapakaa damu haswa. Brenda akawa analia kama mtoto mdogo!!
 
SEHEMU YA 85




“Wanadamu wapumbavu sana nyie, ona sasa mmenikasirisha bure tu mimi.” Asia alilalama kama hafurahii kinachoenda kutokea na kinachoendelea kutokea.
Kisha ghafla akachomoa upanga unaowaka kwa makali yake. Sasa hakuwa katika kucheka tena.
“Mnaupenda utajiri wa bure bure bila kujua namna ya kuuheshimu pumbavu nyie…” Asia akabwata kisha bila mtu yeyote kutarajia aliruka juu na kutua juu ya mwili wa yule mama kibonge.
“kiherehere chako kuja pasipokuhusu kimekuponza…” alisema hayo kisha akauzungusha ule upanga mara moja kwa nguvu ya ajabu.
Mkono mmoja ukachomoka. Mama akapoteza fahamu!! Damu ikaruka juu kama bomba lililo pasuka.
Brenda aliyekuwa jirani na yule mama akapiga mayowe makubwa huku Mamamia yeye akiuziba mdomo wake.
“Hassan Tembo…….. naitwa Tuntufye Kanyenye, Tuntu. Nipo hapa kukufanya uchukie uhai wako, nipo hapa kukufanya uchukiwe na hao uliowapatia ajira, watakuchukia sana na watakutesa sana lakini amini kuwa hautakufa kirahisi. Na kama ukifa basi nitakufuata hukohuko utakapoenda pumbavu wewe….. halafu na wewe hapo” akamgeukia Brenda, “Yule mpumbavu aliyekupeleka kwa huyo mganga mkashirikiana kutaka kuniangamiza mtasaidiana naye kujuta. Nitakung’oa mikono, miguu na hivyo vimatiti vyako kifuani….shenzi kabisa!!” uso wa Asia ulikuwa umeiva haswa wakati anatoa karipio hili, panga linalochuruzika damu likiwa mikononi mwake. Hakuwa katika masihara tena!!
Hapa ndipo Tembo akatambua kuwa huyu hakuwa Asia bali Tuntu katika mwili wa Asia. Kifo chake akakiona kipo jirani kabisa kufika.
Tembo naye akajikojolea!!
Kwa mkono mmoja, Asia akaushika mguu wa yule mama aliyekatwa mkono. Akaanza kuuburuta kuelekea katika pori dogo mbele yake.
Wakabakia viumbe saba wanaotetemeka ajabu!!
Pakiwa kimya hakuna hata mmoja anayemsemesha mwenzake!!
Alichoahidi Tuntu katika mwili wa Asia kikaanza kutimia.
Mateso bila chuki!!
 
Back
Top Bottom